Traduction des sens du Noble Coran - La traduction swahili - 'Abd Allah Muhammad et Nâsir Khamîs

Numéro de la page:close

external-link copy
15 : 10

وَإِذَا تُتۡلَىٰ عَلَيۡهِمۡ ءَايَاتُنَا بَيِّنَٰتٖ قَالَ ٱلَّذِينَ لَا يَرۡجُونَ لِقَآءَنَا ٱئۡتِ بِقُرۡءَانٍ غَيۡرِ هَٰذَآ أَوۡ بَدِّلۡهُۚ قُلۡ مَا يَكُونُ لِيٓ أَنۡ أُبَدِّلَهُۥ مِن تِلۡقَآيِٕ نَفۡسِيٓۖ إِنۡ أَتَّبِعُ إِلَّا مَا يُوحَىٰٓ إِلَيَّۖ إِنِّيٓ أَخَافُ إِنۡ عَصَيۡتُ رَبِّي عَذَابَ يَوۡمٍ عَظِيمٖ

Na wasomewapo washirikina aya za Mwenyezi Mungu zilizo wazi tulizokuteremshia wewe, ewe Mtume, husema wale ambao hawaogopi Hesabu wala hawatarajii malipo wala hawaamini Siku ya kufufuliwa na kuhuishwa, «Lete qur’ani isiyokuwa hii, au tugeuze hii Qur’ani: uifanye halali kuwa haramu na haramu kuwa halali, ahadi kuwa onyo na onyo kuwa ahadi, na uondoe yaliyomo ndani yake ya kukashifu waungu wetu na kuzifanya za kipumbavu akili zetu.» Waambie, ewe Mtume,»Hilo haliko kwangu. Kwani mimi nafuata, katika kila ninalowaamrisha na ninalowakataza, yale ambayo Mola wangu Ameniteremshia na kuniamrisha kwayo. Mimi naogopa kutoka kwa Mwenyezi Mungu, nikienda kinyume na amri Yake, adhabu ya siku iliyo kubwa , nayo ni Siku ya Kiyama. info
التفاسير:

external-link copy
16 : 10

قُل لَّوۡ شَآءَ ٱللَّهُ مَا تَلَوۡتُهُۥ عَلَيۡكُمۡ وَلَآ أَدۡرَىٰكُم بِهِۦۖ فَقَدۡ لَبِثۡتُ فِيكُمۡ عُمُرٗا مِّن قَبۡلِهِۦٓۚ أَفَلَا تَعۡقِلُونَ

Waambie, ewe Mtume, «Lau Mwenyezi Mungu Alitaka, singaliwasomea hii Qur’ani, wala Mwenyezi Mungu Hangaliwajulisha nayo. Basi jueni kuwa hiyo ni haki itokayo kwa Mwenyezi Mungu. Kwani nyinyi mnajua kwamba mimi nimekaa na nyinyi muda mrefu kabla Mola wangu Hajauleta wahyi wa hiyo (Qur’ani) kwangu, na kabla sijaisoma kwenu. Basi hamtumii akili zenu kwa kuzingatia na kufikiri?» info
التفاسير:

external-link copy
17 : 10

فَمَنۡ أَظۡلَمُ مِمَّنِ ٱفۡتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ كَذِبًا أَوۡ كَذَّبَ بِـَٔايَٰتِهِۦٓۚ إِنَّهُۥ لَا يُفۡلِحُ ٱلۡمُجۡرِمُونَ

Hapana yoyote mwenye udhalimu mkubwa zaidi kuliko yule aliyemzulia Mwenyezi Mungu urongo au akazikanusha aya Zake. Hakika ni kwamba hawatafuzu waliowakanusha Manabii wa Mwenyezi Mungu na Mitume Wake wala hawatafaulu. info
التفاسير:

external-link copy
18 : 10

وَيَعۡبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ مَا لَا يَضُرُّهُمۡ وَلَا يَنفَعُهُمۡ وَيَقُولُونَ هَٰٓؤُلَآءِ شُفَعَٰٓؤُنَا عِندَ ٱللَّهِۚ قُلۡ أَتُنَبِّـُٔونَ ٱللَّهَ بِمَا لَا يَعۡلَمُ فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَلَا فِي ٱلۡأَرۡضِۚ سُبۡحَٰنَهُۥ وَتَعَٰلَىٰ عَمَّا يُشۡرِكُونَ

Na hawa wanaomshirikisha Mwenyezi Mungu na asiyekuwa Yeye wanaviabudu visivyowadhuru chochote wala kuwanufaisha ulimwenguni wala Akhera, na wanasema, «Sisi tunawaabudu wao ili watuombee mbele ya Mwenyezi Mungu.» Waambie, ewe Mtume, «Je, mnampa habari Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, jambo Asilolijua, katika mbingu au katika ardhi, kuhusu mambo ya waombezi hawa?» Kwa hakika lau kulikuwa na waombezi katika hizo wa kuwaombea nyinyi mbele Yake, Angalikuwa na ujuzi zaidi kuhusu wao kuliko nyinyi.» Kwani Mwenyenyezi Mungu, Aliyetukuka, Ameepukana na wanachokifanya washirikina hawa cha kushirikisha kwao, katika ibada Yake, vitu visivyodhuru wala kunufaisha. info
التفاسير:

external-link copy
19 : 10

وَمَا كَانَ ٱلنَّاسُ إِلَّآ أُمَّةٗ وَٰحِدَةٗ فَٱخۡتَلَفُواْۚ وَلَوۡلَا كَلِمَةٞ سَبَقَتۡ مِن رَّبِّكَ لَقُضِيَ بَيۡنَهُمۡ فِيمَا فِيهِ يَخۡتَلِفُونَ

Watu walikuwa kwenye dini moja, nayo ni Uislamu, kisha wakatafautiana baada ya hapo, wakakufuru baadhi yao na wengine wakasimama imara juu ya haki. Na lau kwamba si neno lilitangulia kutoka kwa Mwenyezi Mungu la kuwapa muhula wenye kuasi na kutowafanyia haraka kuwapatiliza kwa madhambi yao, basi wangaliamuliwa baina yao kwa kuwaangamiza watu wa ubatilifu miongoni mwao na kuwaokoa watu wa ukweli. info
التفاسير:

external-link copy
20 : 10

وَيَقُولُونَ لَوۡلَآ أُنزِلَ عَلَيۡهِ ءَايَةٞ مِّن رَّبِّهِۦۖ فَقُلۡ إِنَّمَا ٱلۡغَيۡبُ لِلَّهِ فَٱنتَظِرُوٓاْ إِنِّي مَعَكُم مِّنَ ٱلۡمُنتَظِرِينَ

Na makafiri hawa wakaidi wanasema «Basi si ateremshiwe Muhammad ujuzi, dalili na miujiza inayoonekana, kutoka kwa Mola wake, ambayo kwayo tutajua kuwa yeye yuko juu ya haki katika yale anayoyasema.» Waambie, ewe Mtume, «Hakuna ajuwaye ghayb (yasioonekena) isipokuwa ni Mwenyezi Mungu. Akitaka (kufanya wanayoyataka) Atafanya na akitaka (kutofanya) hatafanya. Basi ngojeni, enyi watu, uamuzi wa Mwenyezi Mungu baina yetu na nyinyi wa kuyaharakisha mateso Yake kwa wakosa kati yetu na kumnusuru mwenye haki; mimi nalingojea hilo. info
التفاسير: