Traduction des sens du Noble Coran - La traduction swahili - 'Abd Allah Muhammad et Nâsir Khamîs

Numéro de la page:close

external-link copy
71 : 10

۞ وَٱتۡلُ عَلَيۡهِمۡ نَبَأَ نُوحٍ إِذۡ قَالَ لِقَوۡمِهِۦ يَٰقَوۡمِ إِن كَانَ كَبُرَ عَلَيۡكُم مَّقَامِي وَتَذۡكِيرِي بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ فَعَلَى ٱللَّهِ تَوَكَّلۡتُ فَأَجۡمِعُوٓاْ أَمۡرَكُمۡ وَشُرَكَآءَكُمۡ ثُمَّ لَا يَكُنۡ أَمۡرُكُمۡ عَلَيۡكُمۡ غُمَّةٗ ثُمَّ ٱقۡضُوٓاْ إِلَيَّ وَلَا تُنظِرُونِ

Wasimulie, ewe Mtume, makafiri wa Maka habari ya Nūḥ, amani imshukiye, pamoja na watu wake alipowaambia, «Ikiwa imekuwa ni uzito kwenu kukaa kwangu na nyinyi kuwakumbusha hoja za Mwenyezi Mungu na dalili Zake, basi ni kwa Mwenyezi Mungu ndio mategemeo yangu, na matumaini yangu yako Kwake Yeye. Basi tayarisheni mambo yenu na waiteni washirika wenu, kisha msiyafanye mambo yenu yafichike bali yawe waziwazi yenye kuonekana, kisha amueni juu yangu mateso na mabaya mnayoyaweza wala msinipe muhula wa saa moja ya mchana. info
التفاسير:

external-link copy
72 : 10

فَإِن تَوَلَّيۡتُمۡ فَمَا سَأَلۡتُكُم مِّنۡ أَجۡرٍۖ إِنۡ أَجۡرِيَ إِلَّا عَلَى ٱللَّهِۖ وَأُمِرۡتُ أَنۡ أَكُونَ مِنَ ٱلۡمُسۡلِمِينَ

«Mkiupuuza mwito wangu, basi sikuwaomba malipo, kwa kuwa thawabu zangu ziko kwa Mwenyezi Mungu na malipo yangu yako juu Yake, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake, Peke Yake hakuna mwenye ushirika na Yeye, na nimeamrishwa niwe miongoni mwa wenye kufuata hukumu Yake.» info
التفاسير:

external-link copy
73 : 10

فَكَذَّبُوهُ فَنَجَّيۡنَٰهُ وَمَن مَّعَهُۥ فِي ٱلۡفُلۡكِ وَجَعَلۡنَٰهُمۡ خَلَٰٓئِفَ وَأَغۡرَقۡنَا ٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَاۖ فَٱنظُرۡ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلۡمُنذَرِينَ

Basi wakamkanusha Nūḥ, watu wake katika yale Aliyowaitia kwayo kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo tulimuokoa Yeye na waliokuwa na Yeye kwenye jahazi, na tukawafanya wao washikilie nafasi ya waliokanusha katika ardhi, na tukawazamisha wale waliokataa hoja zetu. Hivyo basi, fikiria, ewe Mtume, namna ulivyokuwa mwisho wa watu wale ambao Mtume wao Aliwaonya adhabu ya Mwenyezi Mungu na mateso Yake? info
التفاسير:

external-link copy
74 : 10

ثُمَّ بَعَثۡنَا مِنۢ بَعۡدِهِۦ رُسُلًا إِلَىٰ قَوۡمِهِمۡ فَجَآءُوهُم بِٱلۡبَيِّنَٰتِ فَمَا كَانُواْ لِيُؤۡمِنُواْ بِمَا كَذَّبُواْ بِهِۦ مِن قَبۡلُۚ كَذَٰلِكَ نَطۡبَعُ عَلَىٰ قُلُوبِ ٱلۡمُعۡتَدِينَ

Kisha tukatuma, baada ya Nūḥ, Mitume kwenda kwa watu wao (Hūd, Ṣāliḥ„ Ibrāhīm, Lūṭ„ Shu'ayb na wengineo), kila Mtume Alikuja kwa watu wake kwa miujiza yenye kuonesha dalili ya utume Wake na ukweli wa yale aliyowaitia. Hawakuwa ni wenye kuyaamini wala kuyafanya yale ambayo watu wa Nūḥ na waliowatangulia miongoni mwa ummah waliopita. Na kama alivyopiga mhuri Mwenyezi Mungu juu ya nyoyo za hawa watu wasiamini, hivyo ndivyo anavyopiga mhuri juu ya nyoyo za wanaofanana na wao kati ya waliokuwa baada yao, miongoni mwa wale ambao walivuka mipaka ya Mwenyezi Mungu na wakaenda kinyume na yale, ambayo Mitume wao waliwaitia kwayo, ya kumtii Yeye, ikiwa ni mateso kwao kwa sababu ya matendo yao ya uasi. info
التفاسير:

external-link copy
75 : 10

ثُمَّ بَعَثۡنَا مِنۢ بَعۡدِهِم مُّوسَىٰ وَهَٰرُونَ إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ وَمَلَإِيْهِۦ بِـَٔايَٰتِنَا فَٱسۡتَكۡبَرُواْ وَكَانُواْ قَوۡمٗا مُّجۡرِمِينَ

Kisha tukawatuma, baada Mitume hao, Mūsā na Hārūn, amani iwashukie, kwenda kwa Fir'awn na watukufu wa watu wake, wakiwa na miujiza yenye kuonesha dalili ya ukweli wao, wakafanya kiburi kwa kukataa kuikubali haki na wakawa ni watu washirikina, wahalifu na wakanushaji. info
التفاسير:

external-link copy
76 : 10

فَلَمَّا جَآءَهُمُ ٱلۡحَقُّ مِنۡ عِندِنَا قَالُوٓاْ إِنَّ هَٰذَا لَسِحۡرٞ مُّبِينٞ

Huo ukweli, ambao Alikuja nao Mūsā, ulipomfikia Fir'awn na watu wake, walisema, «Hakika miujiza aliyokuja nayo Mūsā ni uchawi mtupu ulio waziwazi.» info
التفاسير:

external-link copy
77 : 10

قَالَ مُوسَىٰٓ أَتَقُولُونَ لِلۡحَقِّ لَمَّا جَآءَكُمۡۖ أَسِحۡرٌ هَٰذَا وَلَا يُفۡلِحُ ٱلسَّٰحِرُونَ

Mūsā aliwaambia akiona ajabu kwa maneno yao, «Mnaiyambia haki ilipowajia kuwa ni uchawi? Tazameni sifa za kitu kilichowajia na vilivyomo ndani yake, mtakikuta ni ukweli. Na wachawi hawafaulu wala hawafuzu ulimwenguni wala Akhera.» info
التفاسير:

external-link copy
78 : 10

قَالُوٓاْ أَجِئۡتَنَا لِتَلۡفِتَنَا عَمَّا وَجَدۡنَا عَلَيۡهِ ءَابَآءَنَا وَتَكُونَ لَكُمَا ٱلۡكِبۡرِيَآءُ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَمَا نَحۡنُ لَكُمَا بِمُؤۡمِنِينَ

Fir'awn na kundi lake wakasema kumwambia Mūsā, «Je, umetujia kutuepusha na yale ambayo tuliwakuta nayo wazazi wetu ya kuabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu, mupate kuwa na utukufu na mamlaka, wewe na Hārūn, katika ardhi ya Misri? Basi sisi si wenye kukubali kwamba wawili nyinyi ni Mitume mliotumwa kwetu ili tumuabudu Mwenyezi Mungu, Peke Yake, Asiye na mshirika.» info
التفاسير: