Traduction des sens du Noble Coran - La traduction swahili - 'Abd Allah Muhammad et Nâsir Khamîs

Numéro de la page:close

external-link copy
98 : 10

فَلَوۡلَا كَانَتۡ قَرۡيَةٌ ءَامَنَتۡ فَنَفَعَهَآ إِيمَٰنُهَآ إِلَّا قَوۡمَ يُونُسَ لَمَّآ ءَامَنُواْ كَشَفۡنَا عَنۡهُمۡ عَذَابَ ٱلۡخِزۡيِ فِي ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا وَمَتَّعۡنَٰهُمۡ إِلَىٰ حِينٖ

Imani haikuwafaa watu wa mji wowote walioamini walipoishuhudia adhabu isipokuwa watu wa mji wa Yunus mwana wa Matta. Kwani wao walipohakikisha kwamba adhabu ni yenye kuwashukia, walirejea kwa Mwenyezi Mungu kwa kutubia kidhati; na ulipofunuka ukweli wa toba yao, Mwenyezi Mungu aliwaondolea adhabu ya hizaya baada ya kuwa karibu na wao, na Akawaacha ulimwenguni wakisterehe mpaka muda wao wa kuishi kukoma. info
التفاسير:

external-link copy
99 : 10

وَلَوۡ شَآءَ رَبُّكَ لَأٓمَنَ مَن فِي ٱلۡأَرۡضِ كُلُّهُمۡ جَمِيعًاۚ أَفَأَنتَ تُكۡرِهُ ٱلنَّاسَ حَتَّىٰ يَكُونُواْ مُؤۡمِنِينَ

Na lau Mola wako, ewe Mtume, Aliwatakia Imani watu wa duniani wote, wangaliyaamini, kwa umoja wao, yale uliyokuja nayo, lakini Yeye ana hekima katika hilo. Yeye Anamuongoza Anayemtaka na Anampoteza Anayemtaka, kulingana na hekima Yake, na haliko kwenye uwezo wako jambo la kuwatendesha nguvu watu juu ya kuamini. info
التفاسير:

external-link copy
100 : 10

وَمَا كَانَ لِنَفۡسٍ أَن تُؤۡمِنَ إِلَّا بِإِذۡنِ ٱللَّهِۚ وَيَجۡعَلُ ٱلرِّجۡسَ عَلَى ٱلَّذِينَ لَا يَعۡقِلُونَ

Haikuwa nafsi yoyote ni yenye kumuamini Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa idhini Yake na taufiki Yake. Basi usiisumbue nafsi yako katika hilo, kwani mambo yao yako kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu Ataajaalia adhabu na hizaya kwa wale ambao hawayatii akilini maamrisho Yake na makatazo Yake. info
التفاسير:

external-link copy
101 : 10

قُلِ ٱنظُرُواْ مَاذَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ وَمَا تُغۡنِي ٱلۡأٓيَٰتُ وَٱلنُّذُرُ عَن قَوۡمٖ لَّا يُؤۡمِنُونَ

Sema, ewe Mtume, kuwaambia watu wako, «Fikirini na mzingatie kwa yaliyomo mbinguni na ardhini miongoni mwa aya za Mwenyezi Mungu zilizo waziwazi.» Lakini aya, mazingatio na Mitume wenye kuwaonya waja wa Mwenyezi Mungu adhabu Yake, vyote hivyo havikuwa ni vyenye kuwanufaisha watu wasioamini chochote katika hivyo, kwa sababu ya kupa mgongo kwao na ujeuri wao. info
التفاسير:

external-link copy
102 : 10

فَهَلۡ يَنتَظِرُونَ إِلَّا مِثۡلَ أَيَّامِ ٱلَّذِينَ خَلَوۡاْ مِن قَبۡلِهِمۡۚ قُلۡ فَٱنتَظِرُوٓاْ إِنِّي مَعَكُم مِّنَ ٱلۡمُنتَظِرِينَ

Je, hawa wanangojea isipokuwa hiyo siku watakapoishuhudia adhabu ya Mwenyezi Mungu mfano wa siku za wakale wao waliokanusha waliopita kabla yao? Sema, ewe Mtume, «Ingojeeni adhabu ya Mwenyezi Mungu; hakika mimi ni mwenye kuingojea pamoja na nyinyi kuteswa kwenu.» info
التفاسير:

external-link copy
103 : 10

ثُمَّ نُنَجِّي رُسُلَنَا وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْۚ كَذَٰلِكَ حَقًّا عَلَيۡنَا نُنجِ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ

Kisha tutawaokoa Mitume wetu na wale walioamini pamoja na wao. Na kama tulivyowaokoa hao tutakuokoa wewe, ewe Mtume, na waliokuamini wewe kwa wema utokao kwetu na rehema. info
التفاسير:

external-link copy
104 : 10

قُلۡ يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ إِن كُنتُمۡ فِي شَكّٖ مِّن دِينِي فَلَآ أَعۡبُدُ ٱلَّذِينَ تَعۡبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ وَلَٰكِنۡ أَعۡبُدُ ٱللَّهَ ٱلَّذِي يَتَوَفَّىٰكُمۡۖ وَأُمِرۡتُ أَنۡ أَكُونَ مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ

Sema, ewe Mtume, kuwaambia watu hawa, «Iwapo muko kwenye shaka juu ya usawa wa Dini yangu ambayo nimewaitia kwayo, nayo ni Uislamu, na juu ya uthabiti wangu na kujikita kwangu juu yake, pamoja ya kuwa nyinyi muna matumaini ya kuniepusha nayo, basi mimi sitamuabudu katika hali yoyote ile, yoyote miongoni mwa wale mnaowaabudu mkajifanyia masanamu na mizimu, lakini namuabudu Mwenyezi Mungu, Peke Yake, Mwenye kuwafisha na kuzitwaa roho zenu, na nimeamrishwa niwe ni miongoni mwa wenye kumuamini na wenye kufuata Sheria Zake kivitendo.» info
التفاسير:

external-link copy
105 : 10

وَأَنۡ أَقِمۡ وَجۡهَكَ لِلدِّينِ حَنِيفٗا وَلَا تَكُونَنَّ مِنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ

Na ujisimamishe imara, ewe Mtume, juu ya dini ya Uislamu, hali ya kulingana sawa juu yake, usiwe ni mwenye kupotoka na kuwa kando nayo ukaelekea kwenye Uyahudi au Unaswara wala kumuabudu asiyekuwa Yeye. Wala usiwe ni miongoni mwa wale wanaoshirikisha, katika ibada ya Mola wao, waungu na wale wanaodai kuwa wanafanana na Yeye, kwani ufanyapo hilo utakuwa ni miongoni mwa watakaoangamia. Maneno haya ingawa anaambiwa Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, pia wanaambiwa umma wote. info
التفاسير:

external-link copy
106 : 10

وَلَا تَدۡعُ مِن دُونِ ٱللَّهِ مَا لَا يَنفَعُكَ وَلَا يَضُرُّكَۖ فَإِن فَعَلۡتَ فَإِنَّكَ إِذٗا مِّنَ ٱلظَّٰلِمِينَ

Wala usiwaombe, ewe Mtume, wasiokuwa Mwenyezi Mungu miongoni mwa mizimu na masanamu, kwani wao hawanufaishi wala hawadhuru. Na ufanyapo hilo na ukawaomba wasiokuwa Mwenyezi Mungu, hapo wewe utakuwa ni miongoni mwa wenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu, wenye kujidhulumu nafsi zao kwa ushirikina na kufanya maasia. Maneno haya ingawa anaambiwa Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, pia wanaambiwa umma wote. info
التفاسير: