Traduction des sens du Noble Coran - La traduction swahili - 'Abd Allah Muhammad et Nâsir Khamîs

external-link copy
59 : 10

قُلۡ أَرَءَيۡتُم مَّآ أَنزَلَ ٱللَّهُ لَكُم مِّن رِّزۡقٖ فَجَعَلۡتُم مِّنۡهُ حَرَامٗا وَحَلَٰلٗا قُلۡ ءَآللَّهُ أَذِنَ لَكُمۡۖ أَمۡ عَلَى ٱللَّهِ تَفۡتَرُونَ

Sema, ewe Mtume, kuwaambia hawa wanaokataa wahyi, «Nipeni habari juu ya hii riziki ya wanyama, mimea na vitu vizuri ambavyo Mwenyezi Mungu Amewaumbia nyinyi, mkajihalalishia baadhi ya hivyo na mkajiharamishia vinginevyo.» Waambie, «Je, Mwenyezi Mungu Amewaruhusu hilo au mnaongea maneno ya ubatilifu ya kumzulia Mwenyezi Mungu na mnasema urongo?» Hakika wao wanaongea maneno ya ubatilifu ya kumzulia Mwenyezi Mungu na wanasema urongo. info
التفاسير: