[1] Haki yake ya kumcha ni kwamba atiiwe wala asiasiwe, na ashukuriwe wala asikufuriwe, na akumbukwe wala asisahauliwe. (Ibn Taymiya)
[1] Watu katika kubadilisha maovu na kuamrisha mema wako katika daraja tatu: 1. Kilicho lazima juu ya wanachuoni ni kuwatanabahisha viongozi na watawala, na kuwahimiza kwenye njia ya elimu. 2. Na kinachowalazimu watawala ni kuyabadilisha kwa nguvu zao na mamlaka yao. 3. Na kinachowalazimu watu waliosalia ni kuwajulisha viongozi na watawala baada ya wao kuyakataza kwa kauli. (Tafsir Ibn Attwiyya)