ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - មជ្ឈមណ្ឌលបកប្រែរ៉ូវ៉ាដ

លេខ​ទំព័រ:close

external-link copy
141 : 3

وَلِيُمَحِّصَ ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَيَمۡحَقَ ٱلۡكَٰفِرِينَ

Na pia ili Mwenyezi Mungu awasafishe walioamini na awafutilie mbali makafiri. info
التفاسير:

external-link copy
142 : 3

أَمۡ حَسِبۡتُمۡ أَن تَدۡخُلُواْ ٱلۡجَنَّةَ وَلَمَّا يَعۡلَمِ ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ جَٰهَدُواْ مِنكُمۡ وَيَعۡلَمَ ٱلصَّٰبِرِينَ

Je, mnadhani kwamba mtaingia Peponi ilhali Mwenyezi Mungu hajawajua wale miongoni mwenu waliopigana Jihadi, na akawajua waliosubiri? info
التفاسير:

external-link copy
143 : 3

وَلَقَدۡ كُنتُمۡ تَمَنَّوۡنَ ٱلۡمَوۡتَ مِن قَبۡلِ أَن تَلۡقَوۡهُ فَقَدۡ رَأَيۡتُمُوهُ وَأَنتُمۡ تَنظُرُونَ

Na nyinyi mlikuwa mkiyatamani mauti kabla hamjakutana nayo. Basi sasa mmekwisha yaona na huku mnayatazama. info
التفاسير:

external-link copy
144 : 3

وَمَا مُحَمَّدٌ إِلَّا رَسُولٞ قَدۡ خَلَتۡ مِن قَبۡلِهِ ٱلرُّسُلُۚ أَفَإِيْن مَّاتَ أَوۡ قُتِلَ ٱنقَلَبۡتُمۡ عَلَىٰٓ أَعۡقَٰبِكُمۡۚ وَمَن يَنقَلِبۡ عَلَىٰ عَقِبَيۡهِ فَلَن يَضُرَّ ٱللَّهَ شَيۡـٔٗاۚ وَسَيَجۡزِي ٱللَّهُ ٱلشَّٰكِرِينَ

Na Muhammad si isipokuwa Mtume tu. Wamekwisha pita kabla yake Mitume. Je, akifa au akiuawa, mtageuka mrudi kwa visigino vyenu? Na atakayegeuka akarudi kwa visigino vyake, basi huyo hatamdhuru kitu Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu atawalipa wanaoshukuru. info
التفاسير:

external-link copy
145 : 3

وَمَا كَانَ لِنَفۡسٍ أَن تَمُوتَ إِلَّا بِإِذۡنِ ٱللَّهِ كِتَٰبٗا مُّؤَجَّلٗاۗ وَمَن يُرِدۡ ثَوَابَ ٱلدُّنۡيَا نُؤۡتِهِۦ مِنۡهَا وَمَن يُرِدۡ ثَوَابَ ٱلۡأٓخِرَةِ نُؤۡتِهِۦ مِنۡهَاۚ وَسَنَجۡزِي ٱلشَّٰكِرِينَ

Na haikuwa kwa nafsi kufa isipokuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu kama ilivyoandikiwa muda wake. Na mwenye kutaka malipo ya duniani, tutampa kwayo. Na mwenye kutaka malipo ya Akhera tutampa kwayo. Na tutawalipa wenye kushukuru. info
التفاسير:

external-link copy
146 : 3

وَكَأَيِّن مِّن نَّبِيّٖ قَٰتَلَ مَعَهُۥ رِبِّيُّونَ كَثِيرٞ فَمَا وَهَنُواْ لِمَآ أَصَابَهُمۡ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ وَمَا ضَعُفُواْ وَمَا ٱسۡتَكَانُواْۗ وَٱللَّهُ يُحِبُّ ٱلصَّٰبِرِينَ

Na ni Manabii wangapi waliopigana vita pamoja nao Waumini wenye ikhlasi wengi! Na hawakulegea kwa yaliyowapata katika Njia ya Mwenyezi Mungu, wala hawakudhoofika wala hawakusalimu amri. Na Mwenyezi Mungu huwapenda wanaosubiri. info
التفاسير:

external-link copy
147 : 3

وَمَا كَانَ قَوۡلَهُمۡ إِلَّآ أَن قَالُواْ رَبَّنَا ٱغۡفِرۡ لَنَا ذُنُوبَنَا وَإِسۡرَافَنَا فِيٓ أَمۡرِنَا وَثَبِّتۡ أَقۡدَامَنَا وَٱنصُرۡنَا عَلَى ٱلۡقَوۡمِ ٱلۡكَٰفِرِينَ

Na haikuwa kauli yao isipokuwa walisema: Mola wetu Mlezi! Tufutie dhambi zetu na kupita kwetu kiasi katika mambo yetu, na isimamishe imara miguu yetu na utunusuru dhidi ya kaumu ya makafiri. info
التفاسير:

external-link copy
148 : 3

فَـَٔاتَىٰهُمُ ٱللَّهُ ثَوَابَ ٱلدُّنۡيَا وَحُسۡنَ ثَوَابِ ٱلۡأٓخِرَةِۗ وَٱللَّهُ يُحِبُّ ٱلۡمُحۡسِنِينَ

Basi Mwenyezi Mungu akawapa malipo ya duniani na malipo bora ya Akhera. Na Mwenyezi Mungu anawapenda wafanyao mema. info
التفاسير: