ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - មជ្ឈមណ្ឌលបកប្រែរ៉ូវ៉ាដ

លេខ​ទំព័រ:close

external-link copy
92 : 3

لَن تَنَالُواْ ٱلۡبِرَّ حَتَّىٰ تُنفِقُواْ مِمَّا تُحِبُّونَۚ وَمَا تُنفِقُواْ مِن شَيۡءٖ فَإِنَّ ٱللَّهَ بِهِۦ عَلِيمٞ

Kamwe hamtaufikia wema mpaka mtoe katika vile mnavyovipenda. Na kitu chochote mnachokitoa, basi hakika Mwenyezi Mungu anakijua. info
التفاسير:

external-link copy
93 : 3

۞ كُلُّ ٱلطَّعَامِ كَانَ حِلّٗا لِّبَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ إِلَّا مَا حَرَّمَ إِسۡرَٰٓءِيلُ عَلَىٰ نَفۡسِهِۦ مِن قَبۡلِ أَن تُنَزَّلَ ٱلتَّوۡرَىٰةُۚ قُلۡ فَأۡتُواْ بِٱلتَّوۡرَىٰةِ فَٱتۡلُوهَآ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ

Kila chakula kilikuwa halali kwa Wana wa Israili isipokuwa kile alichojiharamishia Israili mwenyewe kabla ya kuteremshwa Taurati. Sema: Ileteni Taurati, na muisome ikiwa nyinyi ni wakweli. info
التفاسير:

external-link copy
94 : 3

فَمَنِ ٱفۡتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ ٱلۡكَذِبَ مِنۢ بَعۡدِ ذَٰلِكَ فَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلظَّٰلِمُونَ

Na mwenye kumzulia uongo Mwenyezi Mungu baada ya hayo, basi hao ndio madhalimu. info
التفاسير:

external-link copy
95 : 3

قُلۡ صَدَقَ ٱللَّهُۗ فَٱتَّبِعُواْ مِلَّةَ إِبۡرَٰهِيمَ حَنِيفٗاۖ وَمَا كَانَ مِنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ

Sema: Mwenyezi Mungu amesema kweli. Basi fuateni mila ya Ibrahim mwongofu, wala hakuwa miongoni mwa washirikina. info
التفاسير:

external-link copy
96 : 3

إِنَّ أَوَّلَ بَيۡتٖ وُضِعَ لِلنَّاسِ لَلَّذِي بِبَكَّةَ مُبَارَكٗا وَهُدٗى لِّلۡعَٰلَمِينَ

Hakika, Nyumba ya kwanza waliowekewa watu kwa ibada ni ile iliyo Bakka, iliyobarikiwa na yenye uwongofu kwa walimwengu. info
التفاسير:

external-link copy
97 : 3

فِيهِ ءَايَٰتُۢ بَيِّنَٰتٞ مَّقَامُ إِبۡرَٰهِيمَۖ وَمَن دَخَلَهُۥ كَانَ ءَامِنٗاۗ وَلِلَّهِ عَلَى ٱلنَّاسِ حِجُّ ٱلۡبَيۡتِ مَنِ ٱسۡتَطَاعَ إِلَيۡهِ سَبِيلٗاۚ وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ ٱللَّهَ غَنِيٌّ عَنِ ٱلۡعَٰلَمِينَ

Ndani yake kuna Ishara zilizo wazi - masimamio ya Ibrahim. Na mwenye kuingia humo, anakuwa na amani. Na kwa ajili ya Mwenyezi Mungu imewawajibikia watu wahiji kwenye Nyumba hiyo, kwa yule awezaye njia ya kuiendea. Na atakayekufuru, basi hakika Mwenyezi Mungu si mhitaji kwa walimwengu. info
التفاسير:

external-link copy
98 : 3

قُلۡ يَٰٓأَهۡلَ ٱلۡكِتَٰبِ لِمَ تَكۡفُرُونَ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ وَٱللَّهُ شَهِيدٌ عَلَىٰ مَا تَعۡمَلُونَ

Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Kwa nini mnazikufuru ishara za Mwenyezi Mungu, na ilhali Mwenyezi Mungu ni Shahidi kwa yote mnayoyatenda? info
التفاسير:

external-link copy
99 : 3

قُلۡ يَٰٓأَهۡلَ ٱلۡكِتَٰبِ لِمَ تَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ مَنۡ ءَامَنَ تَبۡغُونَهَا عِوَجٗا وَأَنتُمۡ شُهَدَآءُۗ وَمَا ٱللَّهُ بِغَٰفِلٍ عَمَّا تَعۡمَلُونَ

Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Kwa nini mnamzuilia Njia ya Mwenyezi Mungu aliyeamini mkiitakia ipotoke, ilhali nyinyi mnashuhudia? Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na mnayoyatenda. info
التفاسير:

external-link copy
100 : 3

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِن تُطِيعُواْ فَرِيقٗا مِّنَ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَٰبَ يَرُدُّوكُم بَعۡدَ إِيمَٰنِكُمۡ كَٰفِرِينَ

Enyi mlioamini! Mkilitii kundi katika wale waliopewa Kitabu, watawarudisha baada ya kuamini kwenu muwe makafiri. info
التفاسير: