ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - មជ្ឈមណ្ឌលបកប្រែរ៉ូវ៉ាដ

លេខ​ទំព័រ:close

external-link copy
122 : 3

إِذۡ هَمَّت طَّآئِفَتَانِ مِنكُمۡ أَن تَفۡشَلَا وَٱللَّهُ وَلِيُّهُمَاۗ وَعَلَى ٱللَّهِ فَلۡيَتَوَكَّلِ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ

Makundi mawili miongoni mwenu yalipoingiwa na woga kuwa watashindwa - na hali Mwenyezi Mungu ndiye Mlinzi wao. Na kwa Mwenyezi Mungu tu, na wategemee Waumini. info
التفاسير:

external-link copy
123 : 3

وَلَقَدۡ نَصَرَكُمُ ٱللَّهُ بِبَدۡرٖ وَأَنتُمۡ أَذِلَّةٞۖ فَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ لَعَلَّكُمۡ تَشۡكُرُونَ

Na Mwenyezi Mungu alishawanusuru huko Badri hali ya kuwa nyinyi ni wanyonge. Basi mcheni Mwenyezi Mungu ili mpate kushukuru. info
التفاسير:

external-link copy
124 : 3

إِذۡ تَقُولُ لِلۡمُؤۡمِنِينَ أَلَن يَكۡفِيَكُمۡ أَن يُمِدَّكُمۡ رَبُّكُم بِثَلَٰثَةِ ءَالَٰفٖ مِّنَ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةِ مُنزَلِينَ

Ulipowaambia Waumini: Je, haiwatoshi kwamba Mola wenu Mlezi awasaidie kwa Malaika elfu tatu walioteremshwa? info
التفاسير:

external-link copy
125 : 3

بَلَىٰٓۚ إِن تَصۡبِرُواْ وَتَتَّقُواْ وَيَأۡتُوكُم مِّن فَوۡرِهِمۡ هَٰذَا يُمۡدِدۡكُمۡ رَبُّكُم بِخَمۡسَةِ ءَالَٰفٖ مِّنَ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةِ مُسَوِّمِينَ

Kwani! Ikiwa mtavumilia na mkamcha Mungu, na hata maadui wakiwajia mara hii, basi hapo Mola wenu Mlezi atawasaidia kwa Malaika elfu tano wenye alama maalumu. info
التفاسير:

external-link copy
126 : 3

وَمَا جَعَلَهُ ٱللَّهُ إِلَّا بُشۡرَىٰ لَكُمۡ وَلِتَطۡمَئِنَّ قُلُوبُكُم بِهِۦۗ وَمَا ٱلنَّصۡرُ إِلَّا مِنۡ عِندِ ٱللَّهِ ٱلۡعَزِيزِ ٱلۡحَكِيمِ

Na Mwenyezi Mungu hakufanya haya isipokuwa iwe ni bishara kwenu, na ili nyoyo zenu zipate kutua kwa hilo. Na nusura haitoki isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu, Mwenye Nguvu, Mwenye hekima. info
التفاسير:

external-link copy
127 : 3

لِيَقۡطَعَ طَرَفٗا مِّنَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ أَوۡ يَكۡبِتَهُمۡ فَيَنقَلِبُواْ خَآئِبِينَ

Ili akate sehemu katika wale waliokufuru, au awahizi; wapate kurejea nyuma hali ya kuwa wameambulia patupu. info
التفاسير:

external-link copy
128 : 3

لَيۡسَ لَكَ مِنَ ٱلۡأَمۡرِ شَيۡءٌ أَوۡ يَتُوبَ عَلَيۡهِمۡ أَوۡ يُعَذِّبَهُمۡ فَإِنَّهُمۡ ظَٰلِمُونَ

Wewe huna chochote katika jambo hili. Ama atawakubalia toba au atawaadhibu, kwani wao hakika ni madhaalim. info
التفاسير:

external-link copy
129 : 3

وَلِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۚ يَغۡفِرُ لِمَن يَشَآءُ وَيُعَذِّبُ مَن يَشَآءُۚ وَٱللَّهُ غَفُورٞ رَّحِيمٞ

Na ni vya Mwenyezi Mungu vyote vilivyo katika mbingu na vilivyo katika ardhi. Yeye humfutia dhambi amtakaye na humwadhibu amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta dhambi, Mwenye kurehemu. info
التفاسير:

external-link copy
130 : 3

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَأۡكُلُواْ ٱلرِّبَوٰٓاْ أَضۡعَٰفٗا مُّضَٰعَفَةٗۖ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ لَعَلَّكُمۡ تُفۡلِحُونَ

Enyi mlioamini! Msile riba mkizidisha juu kwa juu. Na mcheni Mwenyezi Mungu ili mpate kufaulu. info
التفاسير:

external-link copy
131 : 3

وَٱتَّقُواْ ٱلنَّارَ ٱلَّتِيٓ أُعِدَّتۡ لِلۡكَٰفِرِينَ

Na ucheni Moto ambao umeandaliwa kwa ajili ya makafiri. info
التفاسير:

external-link copy
132 : 3

وَأَطِيعُواْ ٱللَّهَ وَٱلرَّسُولَ لَعَلَّكُمۡ تُرۡحَمُونَ

Na mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume ili mpate kurehemewa. info
التفاسير: