ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - មជ្ឈមណ្ឌលបកប្រែរ៉ូវ៉ាដ

external-link copy
104 : 3

وَلۡتَكُن مِّنكُمۡ أُمَّةٞ يَدۡعُونَ إِلَى ٱلۡخَيۡرِ وَيَأۡمُرُونَ بِٱلۡمَعۡرُوفِ وَيَنۡهَوۡنَ عَنِ ٱلۡمُنكَرِۚ وَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡمُفۡلِحُونَ

Na uwepo umma miongoni mwenu wanaoilingania heri, na wanaamrisha mema na wanakataza maovu. Na hao ndio waliofaulu.[1] info

[1] Watu katika kubadilisha maovu na kuamrisha mema wako katika daraja tatu: 1. Kilicho lazima juu ya wanachuoni ni kuwatanabahisha viongozi na watawala, na kuwahimiza kwenye njia ya elimu. 2. Na kinachowalazimu watawala ni kuyabadilisha kwa nguvu zao na mamlaka yao. 3. Na kinachowalazimu watu waliosalia ni kuwajulisha viongozi na watawala baada ya wao kuyakataza kwa kauli. (Tafsir Ibn Attwiyya)

التفاسير: