કુરઆન મજીદના શબ્દોનું ભાષાંતર - સ્વાહિલી ભાષામાં અનુવાદ - અલી મોહસીન અલ્ બર્વાની

પેજ નંબર:close

external-link copy
92 : 4

وَمَا كَانَ لِمُؤۡمِنٍ أَن يَقۡتُلَ مُؤۡمِنًا إِلَّا خَطَـٔٗاۚ وَمَن قَتَلَ مُؤۡمِنًا خَطَـٔٗا فَتَحۡرِيرُ رَقَبَةٖ مُّؤۡمِنَةٖ وَدِيَةٞ مُّسَلَّمَةٌ إِلَىٰٓ أَهۡلِهِۦٓ إِلَّآ أَن يَصَّدَّقُواْۚ فَإِن كَانَ مِن قَوۡمٍ عَدُوّٖ لَّكُمۡ وَهُوَ مُؤۡمِنٞ فَتَحۡرِيرُ رَقَبَةٖ مُّؤۡمِنَةٖۖ وَإِن كَانَ مِن قَوۡمِۭ بَيۡنَكُمۡ وَبَيۡنَهُم مِّيثَٰقٞ فَدِيَةٞ مُّسَلَّمَةٌ إِلَىٰٓ أَهۡلِهِۦ وَتَحۡرِيرُ رَقَبَةٖ مُّؤۡمِنَةٖۖ فَمَن لَّمۡ يَجِدۡ فَصِيَامُ شَهۡرَيۡنِ مُتَتَابِعَيۡنِ تَوۡبَةٗ مِّنَ ٱللَّهِۗ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلِيمًا حَكِيمٗا

Na haiwi Muumini kumuuwa Muumini ila kwa kukosea. Na mwenye kumuuwa Muumini kwa kukosea basi amkomboe mtumwa aliye Muumini, na atoe diya kuwapa jamaa za maiti, isipo kuwa waache wenyewe kuwa ni sadaka. Na akiwa ni jamaa wa maadui zenu, hali yeye ni Muumini, basi ni kumkomboa mtumwa aliye Muumini. Na akiwa ni miongoni wa watu ambao pana ahadi baina yenu na wao basi wapewe diya watu wake na akombolewe mtumwa Muumini. Na asiye pata, basi afunge miezi miwili mfululizo, kuwa ni toba kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi na Mwenye hikima. info

Kuwagawa wanaafiki namna hii ni kwa ajili ya kutoka shakani, ili Muumini asimuuwe Muumini mwenziwe kwa kumdhania kuwa ni mnaafiki. Na haijuzu kumuuwa Muumini ila kwa kukosea, bila ya kukusudia. Na katika hali ya kumuuwa Muumini kwa kukosea akiwa anaishi chini ya utawala wa dola ya Kiislamu, basi atatoa muuwaji diya kuwapa walio fiwa kuwa ni fidia kwa mtu waliye mkosa, na tena amkomboe mtumwa aliye Muumini iwe ni kuwafidia umma wa Kiislamu kwa walicho kosa. Kwani kumkomboa Muumini ni kama kumhuisha mtu kwa kumpatia uhuru. Inakuwa kwa kukomboa shingo ya Muumini ni kuulipa umma wa Kiislamu kwa walicho kosa. Ikiwa aliye uliwa yumo katika watu ambao wana mapatano ya amani na Waislamu, basi yapasa kumpa uhuru mtumwa na kuwalipa watu wa maiti diya, kwani inakuwa hawaichukui hiyo diya kwa kuwaudhi Waislamu kwa sababu ya mapatano yao. Na ikiwa mwenye kuuwa bila ya kukusudia hakupata mtumwa Muumini wa kumkomboa, basi afunge miezi miwili mfululizo, asile mchana hata siku moja. Hayo yawe ni kuitengeza nafsi na kujizoesha kuwa na hadhari zaidi. Na Mwenyezi Mungu Aliye takasika na Aliye tukuka anazijua sana nafsi za watu na niya zao. Naye ni Mwenye hikima, anajua kuzipanga adhabu zake. "Kuulipa" kwa kuwa utumwa ni amana ya mtu, na kumkomboa mtumwa ni kumhuisha mtu. Akiuliwa Muumini kwa kukosea, na mwenye kuuwa akakomboa shingo ya Muumini basi huyo amehuisha na kuulipa umma.

التفاسير:

external-link copy
93 : 4

وَمَن يَقۡتُلۡ مُؤۡمِنٗا مُّتَعَمِّدٗا فَجَزَآؤُهُۥ جَهَنَّمُ خَٰلِدٗا فِيهَا وَغَضِبَ ٱللَّهُ عَلَيۡهِ وَلَعَنَهُۥ وَأَعَدَّ لَهُۥ عَذَابًا عَظِيمٗا

Na mwenye kumuuwa Muumini kwa kukusudia, basi malipo yake ni Jahannamu humo atadumu, na Mwenyezi Mungu amemkasirikia, na amemlaani, na amemuandalia adhabu kubwa. info

Hakika mwenye kumuuwa Muumini kwa mauwaji ya kukusudia na kuona ndio ndivyo mauwaji hayo, Jaza yake inayo lingana na ukhalifu huo ni kuingizwa Motoni milele, na kughadhibikiwa na Mwenyezi Mungu na afukuzwe kutokana na rehema yake. Na Mwenyezi Mungu amemtengezea Akhera adhabu kubwa, kwani kitendo hichi ndio ukhalifu mkubwa kabisa katika dunia.

التفاسير:

external-link copy
94 : 4

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِذَا ضَرَبۡتُمۡ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ فَتَبَيَّنُواْ وَلَا تَقُولُواْ لِمَنۡ أَلۡقَىٰٓ إِلَيۡكُمُ ٱلسَّلَٰمَ لَسۡتَ مُؤۡمِنٗا تَبۡتَغُونَ عَرَضَ ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا فَعِندَ ٱللَّهِ مَغَانِمُ كَثِيرَةٞۚ كَذَٰلِكَ كُنتُم مِّن قَبۡلُ فَمَنَّ ٱللَّهُ عَلَيۡكُمۡ فَتَبَيَّنُوٓاْۚ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ بِمَا تَعۡمَلُونَ خَبِيرٗا

Enyi mlio amini! Mnapo safiri katika Njia ya Mwenyezi Mungu basi hakikisheni, wala msimwambie anaye kutoleeni salamu: Wewe si Muumini; kwa kutaka manufaa ya maisha ya dunia hii, hali ya kuwa kwa Mwenyezi Mungu zipo ghanima nyingi. Hivyo ndivyo mlivyo kuwa nyinyi zamani, na Mwenyezi Mungu akakuneemesheni. Basi chunguzeni sawa sawa. Hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda info

Kutahadhari msije mkamuuwa Muumini ni waajibu katika wakati wa kwenda vitani. Mkisafiri kwa ajili ya Jihadi ya Njia ya Mwenyezi Mungu jijuvyeni hakika ya hao mnao pigana nao kabla ya kupambana. Je, hao wamesilimu au bado ni washirikina. Wala msimwambie anaye kutoleeni salamu kuwa ni ishara ya amani: Wewe si Muumini, kwa kuwa mnataka kumnyang'anya mali yake na kondoo wake. Bali ipokeeni salamu yake, kwani kwa Mwenyezi Mungu amekuahidini kupata ngawira nyingi nyenginezo. Na nyinyi, enyi Waumini! Mlikuwa hivyo hivyo katika ukafiri kabla ya hayo, na Mwenyezi Mungu amekuhidini. Basi hakikisheni mambo ya hao mnao wakuta. Na Mwenyezi Mungu anajua baraabara, na hapana chochote kinacho fichikana kwake. Na Yeye hakika ni Mwenye kuhisabu kwa mujibu wa ujuzi wake.

التفاسير: