Firo maanaaji al-quraan tedduɗo oo - Eggo e ɗemngal Swahili - Ali Muhsin Alberwani.

Tonngoode hello ngoo:close

external-link copy
79 : 12

قَالَ مَعَاذَ ٱللَّهِ أَن نَّأۡخُذَ إِلَّا مَن وَجَدۡنَا مَتَٰعَنَا عِندَهُۥٓ إِنَّآ إِذٗا لَّظَٰلِمُونَ

Akasema: Mwenyezi Mungu apishe mbali kumshika yeyote yule isipo kuwa tuliye mkuta naye kitu chetu. Hivyo basi tutakuwa wenye kudhulumu. info

Wala haikufalia kwa Yusuf kuvunja mpango alio mkubalia Mwenyezi Mungu, na kumwachia nduguye atoke mkononi mwake. Kwa hivyo maombi yao hayakumlainisha kitu. Akawajibu jawabu mkato, kwa kuwaambia: Mimi najilinda kwa Mwenyezi Mungu isije nafsi yangu ikadhulumu kwa kumzuia yeyote yule isipo kuwa yule yule tuliye mkuta nayo mali yetu. Tukimchukua mwenginewe kwa kumuadhibu tutakuwa katika hao walio vuka mipaka kwa kumshika asiye na makosa kwa madhambi ya mwovu.

التفاسير:

external-link copy
80 : 12

فَلَمَّا ٱسۡتَيۡـَٔسُواْ مِنۡهُ خَلَصُواْ نَجِيّٗاۖ قَالَ كَبِيرُهُمۡ أَلَمۡ تَعۡلَمُوٓاْ أَنَّ أَبَاكُمۡ قَدۡ أَخَذَ عَلَيۡكُم مَّوۡثِقٗا مِّنَ ٱللَّهِ وَمِن قَبۡلُ مَا فَرَّطتُمۡ فِي يُوسُفَۖ فَلَنۡ أَبۡرَحَ ٱلۡأَرۡضَ حَتَّىٰ يَأۡذَنَ لِيٓ أَبِيٓ أَوۡ يَحۡكُمَ ٱللَّهُ لِيۖ وَهُوَ خَيۡرُ ٱلۡحَٰكِمِينَ

Walipo kata tamaa naye wakenda kando kunong'ona. Mkubwa wao akasema: Je! Hamjui ya kwamba baba yenu amechukua ahadi kwenu kutokana na Mwenyezi Mungu, na kabla ya hapo mlimkosa katika agano lenu juu ya Yusuf? Basi mimi sitotoka nchi hii mpaka baba yangu anipe ruhusa au Mwenyezi Mungu anihukumie. Na Yeye ndiye Mbora wa mahakimu. info

Ilipo katika tamaa yao, wakavunjika moyo kukubaliwa maombi yao, wakenda pembeni peke yao wakishauriana juu ya msimamo wao na baba yao. Ilipo ishia shauri kwa mkubwa wao mwenye kupanga mambo yao, aliwaambia: Haikufalieni kuisahau ahadi ya kiapo mliyo mpa baba yenu ya kuwa mtamhifadhi ndugu yenu mpaka mrudi naye, wala mlivyo fungana naye kabla yake kuwa mtamlinda Yusuf, na hayo mkayavunja! Kwa hivyo mimi nitabaki Misri wala sitotoka ila afahamu baba yetu ukweli wa hali hii, na akaniachilia nirejee kwake, au Mwenyezi Mungu anihukumie kurejea kwa hishima, na akanisahilishia njia kwa sababu yoyote ile. Na Yeye ndiye Mbora wa uadilifu kuliko mahakimu wote.

التفاسير:

external-link copy
81 : 12

ٱرۡجِعُوٓاْ إِلَىٰٓ أَبِيكُمۡ فَقُولُواْ يَٰٓأَبَانَآ إِنَّ ٱبۡنَكَ سَرَقَ وَمَا شَهِدۡنَآ إِلَّا بِمَا عَلِمۡنَا وَمَا كُنَّا لِلۡغَيۡبِ حَٰفِظِينَ

Rudini kwa baba yenu, na mwambieni: Ee baba yetu! Mwanao ameiba. Na sisi hatutoi ushahidi ila kwa tunayo yajua. Wala sisi hatukuwa wenye kuhifadhi mambo ya ghaibu. info

Rejeeni nyinyi kwa baba yenu, na msimulieni kisa chote hichi. Na mwambieni: Mkono wa mwanao ulikunjuka akakiiba kikopo cha mfalme, na kimekutikana katika bahasha yake. Kwa huo wizi wake ndio ameshikwa. Nasi hatukwambii ila tuliyo yaona, na wala sisi hatukuwa tunajua yaliyo fichikana katika hukumu ya Mwenyezi Mungu pale tulipo kutaka nawe ukatupa tumhifadhi na turejee naye kwako kama tulivyo ahidiana na tukafungana. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mbora wa uadilifu kuliko mahakimu wote.

التفاسير:

external-link copy
82 : 12

وَسۡـَٔلِ ٱلۡقَرۡيَةَ ٱلَّتِي كُنَّا فِيهَا وَٱلۡعِيرَ ٱلَّتِيٓ أَقۡبَلۡنَا فِيهَاۖ وَإِنَّا لَصَٰدِقُونَ

Na waulize watu wa mji tulio kuwako, na msafara tulio kuja nao. Na hakika sisi tunasema kweli. info

Na ikiwa wewe una shaka na haya tunayo kwambia mtume mtu akuletee ushahidi wa watu wa Misri. Na pia wewe mwenyewe waulize wasafiri wenzetu tulio rudi nao, ipate kudhihiri kuwa sisi hatuna lawama. Nasi tunakuhakikishia kuwa sisi ni wakweli katika haya tuyasemayo.

التفاسير:

external-link copy
83 : 12

قَالَ بَلۡ سَوَّلَتۡ لَكُمۡ أَنفُسُكُمۡ أَمۡرٗاۖ فَصَبۡرٞ جَمِيلٌۖ عَسَى ٱللَّهُ أَن يَأۡتِيَنِي بِهِمۡ جَمِيعًاۚ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلۡعَلِيمُ ٱلۡحَكِيمُ

Akasema: Bali nafsi zenu zimekushawishini kwenye jambo fulani. Subira ni njema! Asaa Mwenyezi Mungu akaniletea wote pamoja. Hakika Yeye ni Mjuzi Mwenye hikima. info

Wakarejea wana walio baki kwa Yaa'qub. Wakamueleza kama alivyo wausia kaka yao mkubwa. Khabari ile ikamtibua huzuni zake, zikazidi kwa kumpoteza mwanawe wa pili. Wala hakutua nafsi yake kwa kuwa wao hawana makosa ya kusabibisha kupotea kwake, naye angali na machungu kwa waliyo mfanyia Yusuf. Akapiga ukelele kwa kuwatuhumu akiwaambia: Niya yenu haikusalimika katika kumhifadhi mwanangu, lakini nafsi zenu zimekuchocheeni mumpoteze kama mlivyo mpoteza nduguye. Lau kuwa nyinyi hamkutoa fatwa ya kuwa mwizi ashikwe afanywe mtumwa kuwa ndiyo adabu ya mwizi huyo Mheshimiwa asingeli mshika mwanangu, wala asingeli baki kaka yenu huko Misri. Lakini mimi sina hila ila kustahamili katika msiba wangu kwa maliwaza mema, huku nikitaraji kwa Mwenyezi Mungu anirudishie wanangu wote. Kwani Yeye ndiye Mwenye ujuzi ulio zunguka hali yangu na hali zao. Na Yeye ndiye Mwenye hikima yenye kushinda, na kwa hiyo ndio hunitendea na hunipangia.

التفاسير:

external-link copy
84 : 12

وَتَوَلَّىٰ عَنۡهُمۡ وَقَالَ يَٰٓأَسَفَىٰ عَلَىٰ يُوسُفَ وَٱبۡيَضَّتۡ عَيۡنَاهُ مِنَ ٱلۡحُزۡنِ فَهُوَ كَظِيمٞ

Naye akajitenga nao, na akasema: Ah! Masikini Yusuf! Na macho yake yakawa meupe kwa huzuni aliyo kuwa akiizuia. info

Akadhikika kwa waliyo yasema, akajitenga nao, kashughulika na msiba wake na huzuni kumkosa Yusuf. Macho yake yakafanya kiza kwa wingi wa huzuni, naye akiificha sana. Huzuni kubwa huleta ugonjwa wa macho unao itwa GLOKOMA, na weupe huzidi mpaka mtu mwisho anakuwa kipofu.

التفاسير:

external-link copy
85 : 12

قَالُواْ تَٱللَّهِ تَفۡتَؤُاْ تَذۡكُرُ يُوسُفَ حَتَّىٰ تَكُونَ حَرَضًا أَوۡ تَكُونَ مِنَ ٱلۡهَٰلِكِينَ

Wakasema: Wallahi! Huachi kumkumbuka Yusuf mpaka uwe mgonjwa au uwe katika walio hiliki. info

Siku zikapita na Yaa'qub kazama katika majonzi yake. Wanawe wakaogopa isije kuwa khatari. Wakamkabili kumtaka apunguze huzuni yake, nao wako baina ya kumwonea huruma na kuchukia kuwa bado yu ngali akimkumbuka Yusuf wakamwambia: Kama hukujipunguzia nafsi yako hapana shaka kumkumbuka Yusuf kutakuzidishia machungu yako yakukondeshe mpaka ukaribie kufa, au ufe khasa!

التفاسير:

external-link copy
86 : 12

قَالَ إِنَّمَآ أَشۡكُواْ بَثِّي وَحُزۡنِيٓ إِلَى ٱللَّهِ وَأَعۡلَمُ مِنَ ٱللَّهِ مَا لَا تَعۡلَمُونَ

Akasema: Hakika mimi namshitakia Mwenyezi Mungu sikitiko langu na huzuni yangu. Na ninajua kwa Mwenyezi Mungu msiyo yajua nyinyi. info

Maneno yao hayakumuathiri hata chembe. Akawajibu kwa kusema: Mimi sikukushitakieni, wala sikukutakeni mnipunguzie machungu yangu! Mimi sina ila Mwenyezi Mungu tu wa kumnyenyekea na kumshitakia dhiki zangu nzito na nyepesi. Wala siwezi kumficha hayo wala lolote nisilo liweza, kwani mimi natambua wema wake wa kutenda na ukunjufu wa rehema yake, jambo ambalo nyinyi hamlijui!

التفاسير: