ترجمة معاني القرآن الكريم - الترجمة السواحلية - علي محسن البرواني

رقم الصفحة:close

external-link copy
34 : 10

قُلۡ هَلۡ مِن شُرَكَآئِكُم مَّن يَبۡدَؤُاْ ٱلۡخَلۡقَ ثُمَّ يُعِيدُهُۥۚ قُلِ ٱللَّهُ يَبۡدَؤُاْ ٱلۡخَلۡقَ ثُمَّ يُعِيدُهُۥۖ فَأَنَّىٰ تُؤۡفَكُونَ

Sema: Je! Yupo katika miungu yenu ya ushirikina aliye anzisha kuumba viumbe, na kisha akavirejesha? Huwaje, basi, mkadanganywa? info

Ewe Mtume! Waambie hao washirikina: Yupo yeyote katika hao mlio wafanya washirika wa Mwenyezi Mungu mkawaabudu, awezaye kuanzisha kuumba tangu mwanzo, na tena akarejea tena baada ya kwisha toweka? Hapana shaka watashindwa kujibu! Basi hapo tena waambie: Allah, Mwenyezi Mungu, tu peke yake, ndiye anaye anzisha kuumba kutokana na kuto kuwepo, na tena viumbe vikitoweka huvirejesha. Vipi basi nyinyi mnaiacha Imani?

التفاسير:

external-link copy
35 : 10

قُلۡ هَلۡ مِن شُرَكَآئِكُم مَّن يَهۡدِيٓ إِلَى ٱلۡحَقِّۚ قُلِ ٱللَّهُ يَهۡدِي لِلۡحَقِّۗ أَفَمَن يَهۡدِيٓ إِلَى ٱلۡحَقِّ أَحَقُّ أَن يُتَّبَعَ أَمَّن لَّا يَهِدِّيٓ إِلَّآ أَن يُهۡدَىٰۖ فَمَا لَكُمۡ كَيۡفَ تَحۡكُمُونَ

Sema: Je! Yupo katika miungu yenu ya ushirikina anaye ongoa kwendea Haki? Sema: Mwenyezi Mungu anaongoa kwendea Haki. Basi, je, anaye stahiki kufuatwa ni yule Mwenye kuongoa kwendea Haki au asiye ongoa ila aongozwe yeye? Basi nyinyi mna nini? Mnahukumu namna gani? info

Ewe Mtume! Waambie hao washirikina: Yupo yeyote katika hao mlio wafanya washirika wa Mwenyezi Mungu mkawaabudu, awezaye kupambanua baina ya uwongofu na upotovu, akawaongoza watu kwenye Njia ya Haki? Wataemewa! Basi, je! Yupi bora kufuatwa - Mwenye kuweza kuongoa kwendea Haki au asiye weza hata kujiongoa nafsi yake? Naye huyo hawezi kumwongoa mtu, ila yeye anahitaji mtu wa kumwongoa. Hao ndio kama wakuu wa makafiri, mapadri na mamonaki ambao ndio mmewafanya ni waola mkamuacha Mwenyezi Mungu!! Nini basi kilicho kupelekeeni kukengeuka hata mkawashirikisha hawa na Mwenyezi Mungu? Na nini hali ya ajabu iliyo kusukumeni kwenye hizo hukumu na sharia za kigeni?

التفاسير:

external-link copy
36 : 10

وَمَا يَتَّبِعُ أَكۡثَرُهُمۡ إِلَّا ظَنًّاۚ إِنَّ ٱلظَّنَّ لَا يُغۡنِي مِنَ ٱلۡحَقِّ شَيۡـًٔاۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمُۢ بِمَا يَفۡعَلُونَ

Na wengi wao hawafuati ila dhana tu. Na dhana haifai kitu mbele ya haki. Hakika Mwenyezi Mungu anajua yote wanayo yatenda. info

Wengi wa washirikina hawafuati katika itikadi zao ila dhana potovu zisio kuwa na dalili zozote! Na kwa jumla, dhana haifidi kitu, wala haiwezi kuwa ni badala ya kuijua Haki, na khasa ikiwa dhana yenyewe ni ya kuzua tu, kama hizi dhana za washirikina. Na hakika Mwenyezi Mungu anayajua vyema wayafanyayo wakuu wa ukafiri na wafuasi wao, naye atawalipa kwa hayo.

التفاسير:

external-link copy
37 : 10

وَمَا كَانَ هَٰذَا ٱلۡقُرۡءَانُ أَن يُفۡتَرَىٰ مِن دُونِ ٱللَّهِ وَلَٰكِن تَصۡدِيقَ ٱلَّذِي بَيۡنَ يَدَيۡهِ وَتَفۡصِيلَ ٱلۡكِتَٰبِ لَا رَيۡبَ فِيهِ مِن رَّبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ

Na haiwezekani Qur'ani hii kuwa imetungwa na haitoki kwa Mwenyezi Mungu. Lakini hii inasadikisha yaliyo tangulia, na ni mfafanuo wa Kitabu kisicho na shaka ndani yake, kutokana na Mola Mlezi wa viumbe vyote. info

Haiwezi kutokea kuwa hii Qur'ani aizue mtu yeyote, kwani katika kuwa haiwezi kuigwa, na katika uwongofu wake, na hukumu zake, hayumkini kuwa itoke kwa yeyote isipo kuwa kwa Mwenyezi Mungu tu. Nayo inasadikisha Vitabu vya mbinguni vilivyo tangulia katika mambo ya Haki yaliyo tajwa humo, na inaweka wazi yaliyo kwisha andikwa na kuthibitishwa katika mambo ya hakika na sharia. Hapana shaka kuwa Qur'ani hii ina cheo maalumu kwa Mwenyezi Mungu, nayo ni muujiza ambao hapana mtu anaye weza kuleta mfano wake.

التفاسير:

external-link copy
38 : 10

أَمۡ يَقُولُونَ ٱفۡتَرَىٰهُۖ قُلۡ فَأۡتُواْ بِسُورَةٖ مِّثۡلِهِۦ وَٱدۡعُواْ مَنِ ٱسۡتَطَعۡتُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ

Je! Ndiyo wanasema ameizua? Sema: Hebu leteni sura moja mfano wake na muwaite (kukusaidieni) muwawezao, isipo kuwa Mwenyezi Mungu, ikiwa nyinyi mnasema kweli. info

Bali hawa washirikina wanasema: Muhammad kaizua hii Qur'ani mwenyewe! Ewe Mtume! Waambie: Ikiwa hii Qur'ani ni kazi ya mwanaadamu, basi nyinyi leteni Sura moja tu mfano wake, na muwatake muwatakao, isipo kuwa Mwenyezi Mungu, waje kukusaidieni; ikiwa nyinyi ni wasema kweli katika madai yenu kuwa hii Qur'ani nimeitunga mimi.

التفاسير:

external-link copy
39 : 10

بَلۡ كَذَّبُواْ بِمَا لَمۡ يُحِيطُواْ بِعِلۡمِهِۦ وَلَمَّا يَأۡتِهِمۡ تَأۡوِيلُهُۥۚ كَذَٰلِكَ كَذَّبَ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡۖ فَٱنظُرۡ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلظَّٰلِمِينَ

Bali wameyakanusha wasio yaelewa ilimu yake kabla hayajawajia maelezo yake. Kadhaalika walio kabla yao walikanusha vile vile. Basi angalia jinsi ulivyo kuwa mwisho wa madhaalimu hao. info

Bali hawa washirikina wamekimbilia kuikadhibisha Qur'ani bila ya kuzingatia, wakajua yaliomo ndani yake! Wao wenyewe hawakutazama mna nini, wala hawakusita kuitafuta tafsiri yake, na kutaka kuelewa hukumu zake kwa kuwauliza wenginewe! Na kukadhibisha namna hii bila ya ujuzi, ndivyo walivyo wakanusha makafiri wa kaumu za zamani Mitume wao na Vitabu vyao! Basi, ewe mwanaadamu! Angalia yaliishiaje mambo ya walio kadhibisha walio tangulia. Waliachiliwa mbali na wakateketezwa kwa adhabu! Na huu ndio mwendo wa Mwenyezi Mungu kwa mfano wa hao.

التفاسير:

external-link copy
40 : 10

وَمِنۡهُم مَّن يُؤۡمِنُ بِهِۦ وَمِنۡهُم مَّن لَّا يُؤۡمِنُ بِهِۦۚ وَرَبُّكَ أَعۡلَمُ بِٱلۡمُفۡسِدِينَ

Na miongoni mwao wapo wanao iamini, na miongoni mwao wapo wasio iamini. Na Mola wako Mlezi anawajua vyema mafisadi. info

Na miongoni mwa hawa wakanushao wapo ambao watakuja iamini Qur'ani baada ya kuyafahamu yaliyomo ndani yake, na wakayaelewa maana yake. Na kipo miongoni mwao kikundi ambacho hakiamini wala hakiachi upotovu wake! Na Allah Subhanahu wa Taa'la anawajua vyema wakanushao mafisadi, na atawalipa kwa vitendo vyao.

التفاسير:

external-link copy
41 : 10

وَإِن كَذَّبُوكَ فَقُل لِّي عَمَلِي وَلَكُمۡ عَمَلُكُمۡۖ أَنتُم بَرِيٓـُٔونَ مِمَّآ أَعۡمَلُ وَأَنَا۠ بَرِيٓءٞ مِّمَّا تَعۡمَلُونَ

Na wakikukanusha wewe, sema: Mimi nina a'mali yangu, na nyinyi mna a'mali yenu. Nyinyi hamna jukumu kwa niyatendayo, wala mimi sina jukumu kwa myatendayo. info

Na ewe Mtume! Wakishikilia kuendelea na kukukadhibisha baada ya kuwadhihirikia wazi dalili za Unabii wako, basi wewe waambie: Hakika mimi nitalipwa kwa a'mali yangu,(vitendo vyangu); na nyinyi mtalipwa kwa a'mali yenu kama itakavyo kuwa. Na mimi naendelea na Wito wangu, na nyinyi hamtahisabiwa kwa a'mali yangu, wala mimi sitahisabiwa kwa a'mali yenu. Basi nyinyi fanyeni mpendavyo. Na Mwenyezi Mungu atamlipa kila mtu kwa aliyo yachuma.

التفاسير:

external-link copy
42 : 10

وَمِنۡهُم مَّن يَسۡتَمِعُونَ إِلَيۡكَۚ أَفَأَنتَ تُسۡمِعُ ٱلصُّمَّ وَلَوۡ كَانُواْ لَا يَعۡقِلُونَ

Na wapo miongoni mwao wanao kusikiliza. Je, wewe unaweza kuwafanya viziwi wasikie ijapo kuwa hawafahamu? info

Na katika hawa makafiri wapo wanao kusikiliza wewe, Mtume, pale unapo waita wafuate Dini ya Mwenyezi Mungu, na hali nyoyo zao zimefungwa hazikubali Wito wako. Basi wewe huwezi kuwafanya hawa viziwi wakusikie na waongoke. Na khasa ilivyo kuwa juu ya uziwi wao, hawafahamu uyasemayo.

التفاسير: