Ewe Mtume! Waambie hao washirikina: Yupo yeyote katika hao mlio wafanya washirika wa Mwenyezi Mungu mkawaabudu, awezaye kuanzisha kuumba tangu mwanzo, na tena akarejea tena baada ya kwisha toweka? Hapana shaka watashindwa kujibu! Basi hapo tena waambie: Allah, Mwenyezi Mungu, tu peke yake, ndiye anaye anzisha kuumba kutokana na kuto kuwepo, na tena viumbe vikitoweka huvirejesha. Vipi basi nyinyi mnaiacha Imani?