Қуръони Карим маъноларининг таржимаси - Савоҳилийча таржима - Али Муҳсин ал-Бервааний

Бет рақами:close

external-link copy
89 : 11

وَيَٰقَوۡمِ لَا يَجۡرِمَنَّكُمۡ شِقَاقِيٓ أَن يُصِيبَكُم مِّثۡلُ مَآ أَصَابَ قَوۡمَ نُوحٍ أَوۡ قَوۡمَ هُودٍ أَوۡ قَوۡمَ صَٰلِحٖۚ وَمَا قَوۡمُ لُوطٖ مِّنكُم بِبَعِيدٖ

Na enyi watu wangu! Kukhalifiana nami kusikupelekeeni hata mkasibiwa kama walivyo sibiwa watu wa Nuhu, au watu wa Hud, au watu wa Saleh. Na watu wa Lut' si mbali nanyi. info

Na enyi watu! Hizi khitilafu ziliopo baina yangu na nyinyi zisikupelekeeni kufanya inda na mkashikilia ukafiri, hata yakakupateni yaliyo wapata kaumu ya Nuhu, na kaumu ya Huud, na kaumu ya Swaleh. Na wala zama na pahala pa kaumu Lut' na maangamizo yao si mbali nanyi! Basi zingatieni yasikusibuni yaliyo wasibu hao.

التفاسير:

external-link copy
90 : 11

وَٱسۡتَغۡفِرُواْ رَبَّكُمۡ ثُمَّ تُوبُوٓاْ إِلَيۡهِۚ إِنَّ رَبِّي رَحِيمٞ وَدُودٞ

Na ombeni msamaha kwa Mola wenu Mlezi, tena tubuni kwake. Hakika Mola wangu Mlezi ni Mwenye kurehemu na Mwenye upendo. info

Na mtakeni Mwenyezi Mungu akusameheni madhambi yenu, na rejeeni kwake kwa majuto mkiomba maghfira kila mtendapo dhambi. Hakika Mola wangu Mlezi ni mwingi wa rehema, ni mwenye mapenzi. Huwasamehe wenye kutubu, na anawapenda wenye kurejea kwake.

التفاسير:

external-link copy
91 : 11

قَالُواْ يَٰشُعَيۡبُ مَا نَفۡقَهُ كَثِيرٗا مِّمَّا تَقُولُ وَإِنَّا لَنَرَىٰكَ فِينَا ضَعِيفٗاۖ وَلَوۡلَا رَهۡطُكَ لَرَجَمۡنَٰكَۖ وَمَآ أَنتَ عَلَيۡنَا بِعَزِيزٖ

Wakasema: Ewe Shua'ibu! Mengi katika hayo unayo yasema hatuyafahamu. Na sisi tunakuona huna nguvu kwetu. Lau kuwa si jamaa zako tunge kupiga mawe, wala wewe si mtukufu kwetu. info

Wakasema: Ewe Shua'ibu! Mengi unayo yasema sisi hatuyafahamu! Na sisi tunakuhakikishia kuwa sisi tunakuona wewe dhaifu, huna nguvu zozote za kujitetea, wala kutukinaisha tukitaka kukutenda unayo yachukia. Na lau kuwa si kwa wema wetu kwa jamaa zako, kwani wao wanafuata dini yetu, tungeli kuulia mbali kwa kukupiga mawe. Na wewe si mtukufu kati yetu hata tukutukuze, na tukuhishimu, na tukukirimu na tuache kukuuwa kwa mawe! Ni wema tunao wafanyia jamaa zako tu ndio unao tuzuia tusikuuwe.

التفاسير:

external-link copy
92 : 11

قَالَ يَٰقَوۡمِ أَرَهۡطِيٓ أَعَزُّ عَلَيۡكُم مِّنَ ٱللَّهِ وَٱتَّخَذۡتُمُوهُ وَرَآءَكُمۡ ظِهۡرِيًّاۖ إِنَّ رَبِّي بِمَا تَعۡمَلُونَ مُحِيطٞ

Akasema: Enyi watu wangu! Kwani jamaa zangu ni watukufu zaidi kwenu kuliko Mwenyezi Mungu? Na Yeye mmemueka nyuma ya migongo yenu! Hakika Mola wangu Mlezi ni Mwenye kuyazunguka yote mnayo yatenda. info

Akasema Shua'ibu: Enyi watu wangu! Hivyo jamaa zangu ndio wanastahiki kufanyiwa wema kuliko Mwenyezi Mungu. Wao mnawakumbuka, na mkataka kunifanyia jamala mimi kwa ajili yao. Lakini Yeye mmemsahau na mkamfanya kama kitu kilicho tupiliwa mbali nyuma ya migongo yenu! Hakika Mola Mlezi wangu ni Mwenye kuyazunguka yote mnayo yafanya kwa kuyajua, hapana linalo fichikana kwake katika vitendo vyenu, na atakuhisabieni kwavyo hata ikiwa nyinyi mtasahau.

التفاسير:

external-link copy
93 : 11

وَيَٰقَوۡمِ ٱعۡمَلُواْ عَلَىٰ مَكَانَتِكُمۡ إِنِّي عَٰمِلٞۖ سَوۡفَ تَعۡلَمُونَ مَن يَأۡتِيهِ عَذَابٞ يُخۡزِيهِ وَمَنۡ هُوَ كَٰذِبٞۖ وَٱرۡتَقِبُوٓاْ إِنِّي مَعَكُمۡ رَقِيبٞ

Na enyi watu wangu! Fanyeni mwezayo, na mimi pia ninafanya. Karibuni mtajua ni nani itakaye mfikia adhabu ya kumhizi, na nani aliye mwongo. Na ngojeni, mimi pia ninangoja pamoja nanyi. info

Enyi watu wangu! Tendeni mnayo weza nyinyi kuyatenda. Kama hamsikilizi nasaha zangu, mimi naendelea kushikilia kutenda kinyume na vitendo vyenu. Na hapo tutakuja jua ni nani kati yetu ataye fikiwa na adhabu ya kumfedhehi na kumdhalilisha, na ni nani kati yetu ni mwongo - mimi ninaye kuonyeni na adhabu, au nyinyi mnao nionya kunifukuza katika mji wenu? Ngojeeni nini litatokea, na mimi nangojea pamoja nanyi.

التفاسير:

external-link copy
94 : 11

وَلَمَّا جَآءَ أَمۡرُنَا نَجَّيۡنَا شُعَيۡبٗا وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مَعَهُۥ بِرَحۡمَةٖ مِّنَّا وَأَخَذَتِ ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ ٱلصَّيۡحَةُ فَأَصۡبَحُواْ فِي دِيَٰرِهِمۡ جَٰثِمِينَ

Na ilipo fika amri yetu, tulimwokoa Shua'ibu na wale walio amini pamoja naye kwa rehema yetu. Na ukelele uliwanyakua walio dhulumu, na wakapambaukiwa majumbani mwao wamekufa kifudifudi! info

Ilipo kuja amri yetu ya kuwaadhibu na kuwaangamiza, tulimwokoa Shua'ibu na walio amini pamoja naye wasipate adhabu na maangamizo. Kuokoka kwao kulikuwa kutokana na rehema iliyo tokana nasi. Ukelele uliwatwaa watu wa Madyana, na tetemeko la kuteketeza, wakapambaukiwa wamekwisha jifia katika majumba yao, wamelala kifudifudi, hawatukusiki hata kidogo!

التفاسير:

external-link copy
95 : 11

كَأَن لَّمۡ يَغۡنَوۡاْ فِيهَآۗ أَلَا بُعۡدٗا لِّمَدۡيَنَ كَمَا بَعِدَتۡ ثَمُودُ

Kama kwamba hawakuwamo humo. Zingatia walivyo angamia watu wa Madyana, kama walivyo angamia watu wa Thamud! info

Mambo yakawishia, na athari zao zikapotea. Wakawa kama kwamba hawajapata kukaa katika majumba yao! Hali yao ikatamka ya kumzindua kila mwenye akili apate kuzingatia! Zingatia basi maangamizo ya Madyana, na vipi walivyo baidika na rehema ya Mwenyezi Mungu kama walivyo baidika watu wa Thamud kabla yao!

التفاسير:

external-link copy
96 : 11

وَلَقَدۡ أَرۡسَلۡنَا مُوسَىٰ بِـَٔايَٰتِنَا وَسُلۡطَٰنٖ مُّبِينٍ

Na hakika tulimtuma Musa pamoja na Ishara zetu na uthibitisho ulio wazi info

Na hakika tulimtuma Musa na tukamuunga mkono kwa miujiza yenye kuonyesha ukweli wake, na uthibitisho ulio wazi wenye nguvu juu ya nafsi.

التفاسير:

external-link copy
97 : 11

إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ وَمَلَإِيْهِۦ فَٱتَّبَعُوٓاْ أَمۡرَ فِرۡعَوۡنَۖ وَمَآ أَمۡرُ فِرۡعَوۡنَ بِرَشِيدٖ

Kwa Firauni na waheshimiwa wake. Lakini wao walifuata amri ya Firauni, na amri ya Firauni haikuwa yenye uwongofu. info

Tulimtuma ende kwa Firauni na wakuu katika watu wake. Firauni akamkanya Musa na akawaamrisha watu wake wamfuate yeye Firauni katika ukafiri wake. Wakenda kinyume na amri ya Musa! Wala amri ya Firauni haikuwa ni nyoofu yenye matokea mema hata istahiki kufuatwa.

التفاسير: