ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - អាលី ម៉ុហសុីន អាល់ពើវ៉ានី

លេខ​ទំព័រ:close

external-link copy
34 : 4

ٱلرِّجَالُ قَوَّٰمُونَ عَلَى ٱلنِّسَآءِ بِمَا فَضَّلَ ٱللَّهُ بَعۡضَهُمۡ عَلَىٰ بَعۡضٖ وَبِمَآ أَنفَقُواْ مِنۡ أَمۡوَٰلِهِمۡۚ فَٱلصَّٰلِحَٰتُ قَٰنِتَٰتٌ حَٰفِظَٰتٞ لِّلۡغَيۡبِ بِمَا حَفِظَ ٱللَّهُۚ وَٱلَّٰتِي تَخَافُونَ نُشُوزَهُنَّ فَعِظُوهُنَّ وَٱهۡجُرُوهُنَّ فِي ٱلۡمَضَاجِعِ وَٱضۡرِبُوهُنَّۖ فَإِنۡ أَطَعۡنَكُمۡ فَلَا تَبۡغُواْ عَلَيۡهِنَّ سَبِيلًاۗ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلِيّٗا كَبِيرٗا

Wanaume ni wasimamizi wa wanawake, kwa kufadhiliwa na Mwenyezi Mungu baadhi yao juu ya baadhi, na kwa mali yao wanayo yatoa. Basi wanawake wema ni wale wenye kut'ii na wanao jilinda hata katika siri kwa kuwa Mwenyezi Mungu ameamrisha wajilinde. Na ambao mnachelea kutoka katika ut'iifu wanasihini, muwahame katika malazi na wapigeni. Wakikut'iini msiwatafutie njia ya kuwaudhi bure. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye aliye juu na Mkuu. info

Wanaume wana haki ya kuwaangalia na kuwachunga wanawake, na kuwasimamia katika mambo yao kwa vile Mwenyezi Mungu amewapa wao wanaume sifa za kuweza kuisimamia haki hii, na kwa kuwa wao ndio wanao hangaika na kufanya juhudi ya kutafuta mali ya kuutumilia ukoo mzima. Basi wanawake wema wanakuwa ni wat'iifu kwa Mwenyezi Mungu na waume zao. Ni wenye kuhifadhi vyote ambavyo waume zao hawavioni kwa sababu Mwenyezi Mungu ameamrisha vihifadhiwe, na kwa kuwapa wao tawfiki. Na wanawake wanao onyesha kuanza uasi wanasihini kwa maneno yenye kuathiri. Kama hawakusikia tenganeni nao kitandani. Hawakusikia, watieni adabu kwa pigo dogo, si la kuwajuruhi wala kuwadhalilisha. Wakirejea kwenye ut'iifu wenu kwa njia mojapo katika hizi tatu basi msiwatafutie kisababu cha kuwatesa zaidi kuliko haya. Hakika Mwenyezi Mungu yuko juu yenu, naye atakupatilizeni pindi mkiwaudhi wake zenu au mkawafanyia jeuri.

التفاسير:

external-link copy
35 : 4

وَإِنۡ خِفۡتُمۡ شِقَاقَ بَيۡنِهِمَا فَٱبۡعَثُواْ حَكَمٗا مِّنۡ أَهۡلِهِۦ وَحَكَمٗا مِّنۡ أَهۡلِهَآ إِن يُرِيدَآ إِصۡلَٰحٗا يُوَفِّقِ ٱللَّهُ بَيۡنَهُمَآۗ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلِيمًا خَبِيرٗا

Na mkichelea kutakuwapo mfarakano baina ya mke na mume basi pelekeni muamuzi kutokana na jamaa za mume, na muamuzi kutokana na jamaa za mke. Wakitaka mapatano Mwenyezi Mungu atawawezesha. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mwenye khabari. info

Pindi pakitokea kukhitalifiana baina ya mke na mume, na mkakhofia kutokea kufarikiana kutako leta t'alaka, chagueni waamuzi wawili. Mmoja kutokana na upande wa mume na mwengine upande wa mke. Wakitaka kusuluhiana Mwenyezi Mungu atawawafikisha wafikilie lilio kheri kwa wote wawili, nako ama kukaa kwa wema au kuachana kwa ihsani. Hakika Mwenyezi Mungu anachungua kila kitu cha waja wake, kilicho dhihiri na kilicho fichikana.

التفاسير:

external-link copy
36 : 4

۞ وَٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ وَلَا تُشۡرِكُواْ بِهِۦ شَيۡـٔٗاۖ وَبِٱلۡوَٰلِدَيۡنِ إِحۡسَٰنٗا وَبِذِي ٱلۡقُرۡبَىٰ وَٱلۡيَتَٰمَىٰ وَٱلۡمَسَٰكِينِ وَٱلۡجَارِ ذِي ٱلۡقُرۡبَىٰ وَٱلۡجَارِ ٱلۡجُنُبِ وَٱلصَّاحِبِ بِٱلۡجَنۢبِ وَٱبۡنِ ٱلسَّبِيلِ وَمَا مَلَكَتۡ أَيۡمَٰنُكُمۡۗ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُحِبُّ مَن كَانَ مُخۡتَالٗا فَخُورًا

Muabuduni Mwenyezi Mungu wala msimshirikishe na chochote. Na wafanyieni wema wazazi wawili na jamaa na mayatima na masikini na jirani wa karibu na jirani wa mbali, na rafiki wa ubavuni na mpita njia, na walio milikiwa na mikono yenu ya kulia. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wenye kiburi wanao jifakhiri, info

Nanyi muabuduni Mwenyezi Mungu peke yake, wala msimfanyie washirika katika Ungu na kuabudiwa. Na watendeeni wema wazazi wenu bila ya taksiri yoyote, na pia jamaa zenu, na mayatima, na walio fakirika kwa sababu ya kuemewa au kupata masaibu katika mali yao, na jirani mliye karibiana naye kwa nasaba, na jirani mtu mbali, na mwenzio katika kazi au njia au majlisi, na msafiri mhitaji asiye kuwa na kituo katika nchi maalumu, na watumwa wenu wanaume na wanawake mlio wamiliki. Hakika Mwenyezi Mungu hampendi anaye jipa ubora juu ya watu wengine, na hawachukulii watu kwa huruma, na anakithirisha kujisifu mwenyewe kwa kujifakhiri.

التفاسير:

external-link copy
37 : 4

ٱلَّذِينَ يَبۡخَلُونَ وَيَأۡمُرُونَ ٱلنَّاسَ بِٱلۡبُخۡلِ وَيَكۡتُمُونَ مَآ ءَاتَىٰهُمُ ٱللَّهُ مِن فَضۡلِهِۦۗ وَأَعۡتَدۡنَا لِلۡكَٰفِرِينَ عَذَابٗا مُّهِينٗا

Ambao wanafanya ubakhili na wanaamrisha watu ubakhili, na wanaficha fadhila alizo wapa Mwenyezi Mungu. Na tumewaandalia makafiri adhabu ya fedheha, info

Hao ndio wanao ongeza juu ya takaburi na tafakhuri yao ila ya kuwafanyia watu ubakhili kwa mali yao na juhudi yao. Tena ikawa wanawataka watu wafanye ubakhili kama wao. Kazi yao ni kukhofia neema na fadhila ya Mwenyezi Mungu isiwatoke. Kwa hivyo, basi, hawajifai wenyewe wala hawawafai watu. Wapinzani kama hao tumekwisha waandalia adhabu ya kutia machungu na ya kudhalilisha.

التفاسير: