ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - អាលី ម៉ុហសុីន អាល់ពើវ៉ានី

លេខ​ទំព័រ:close

external-link copy
45 : 4

وَٱللَّهُ أَعۡلَمُ بِأَعۡدَآئِكُمۡۚ وَكَفَىٰ بِٱللَّهِ وَلِيّٗا وَكَفَىٰ بِٱللَّهِ نَصِيرٗا

Na Mwenyezi Mungu anawajua vyema maadui zenu. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa ni Mlinzi, na anatosha kuwa ni Mwenye kukunusuruni. info

Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi zaidi kuliko nyinyi kuwajua maadui zenu wa kweli, na anatambua zaidi yaliyo ndani ya nafsi zao. Ulinzi wa Mwenyezi Mungu unakulindeni, na unakuangalieni, na unakutosheni. Basi msitafute ulinzi wa mwenginewe usio kuwa wake. Msaada na nusura yake inakutoshelezeni; basi msiwe kutaka msaada wa mwenginewe.

التفاسير:

external-link copy
46 : 4

مِّنَ ٱلَّذِينَ هَادُواْ يُحَرِّفُونَ ٱلۡكَلِمَ عَن مَّوَاضِعِهِۦ وَيَقُولُونَ سَمِعۡنَا وَعَصَيۡنَا وَٱسۡمَعۡ غَيۡرَ مُسۡمَعٖ وَرَٰعِنَا لَيَّۢا بِأَلۡسِنَتِهِمۡ وَطَعۡنٗا فِي ٱلدِّينِۚ وَلَوۡ أَنَّهُمۡ قَالُواْ سَمِعۡنَا وَأَطَعۡنَا وَٱسۡمَعۡ وَٱنظُرۡنَا لَكَانَ خَيۡرٗا لَّهُمۡ وَأَقۡوَمَ وَلَٰكِن لَّعَنَهُمُ ٱللَّهُ بِكُفۡرِهِمۡ فَلَا يُؤۡمِنُونَ إِلَّا قَلِيلٗا

Miongoni mwa Mayahudi wamo ambao hubadilisha maneno kuyatoa mahala pake, na husema: Tumesikia na tumeasi, na sikia bila ya kusikilizwa. Na husema: "Raai'naa", kwa kuzipotoa ndimi zao ili kuitukana Dini. Na lau kama wangeli sema: Tumesikia na tumet'ii, na usikie na "Undhurna" (Utuangalie), ingeli kuwa ni kheri kwao na sawa zaidi. Lakini Mwenyezi Mungu amewalaani kwa kufuru yao; basi hawaamini ila wachache tu. info

Miongoni mwa Mayahudi kipo kikundi kazi yao kugeuza geuza maana ya maneno. Wao husema kimoyomoyo kumwambia Mtume s.a.w.: Tumesikia hayo maneno, na hatuifati hiyo amri. Na pia husema: Sikia maneno yetu - hukusikia wito. Wakikusudia kwa hayo kumuapiza Mtume. Na husema: Sikia bila ya kusikilizwa. Tamko hilo wanalipindua maana. Muradi wao ni kumuapiza, na wanajidai kuwa muradi wao ni kumwombea dua. Na husema: "Raai'na", wakipindua ndimi zao wakijitia kuwa wanakusudia "Undhurna" yaani "Tuangalie". Wanaonyesha kuwa wanataka uangalizi wake, na kumbe wanakusudia neno la Kiyahudi lenye maana ya "Mpumbavu" ili kuibeza Dini ya Kiislamu. Na lau kuwa wangeli nyooka sawa wakasema: "Tumesikia na tumet'ii" badala ya hiyo kauli yao ya "Tumesikia na tumeasi", na wakasema: "Sikia" na wasiseme "Bila ya kusikilizwa", na wakasema :"Undhurna" yaani "Tuangalie", badala ya "Raa'ina", ingeli kuwa bora kwao kuliko hayo wayasemayo, na ingeli kuwa ndiyo njia ya uadilifu zaidi. Lakini Mwenyezi Mungu amewatoa katika rehema yake kwa ule upinzani wao. Kwa hivyo huwaoni miongoni mwao wanao mwitikia mwenye kuwaitia Imani ila wachache tu.

التفاسير:

external-link copy
47 : 4

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَٰبَ ءَامِنُواْ بِمَا نَزَّلۡنَا مُصَدِّقٗا لِّمَا مَعَكُم مِّن قَبۡلِ أَن نَّطۡمِسَ وُجُوهٗا فَنَرُدَّهَا عَلَىٰٓ أَدۡبَارِهَآ أَوۡ نَلۡعَنَهُمۡ كَمَا لَعَنَّآ أَصۡحَٰبَ ٱلسَّبۡتِۚ وَكَانَ أَمۡرُ ٱللَّهِ مَفۡعُولًا

Enyi mlio pewa Kitabu! Aminini tuliyo yateremsha yenye kusadikisha yale mliyo nayo, kabla hatujazigeuza nyuso tukazipeleka kisogoni, au tukawalaani kama tulivyo walaani watu wa Sabato (Jumaamosi). Na amri ya Mwenyezi Mungu ni lazima ifanyike. info

Enyi mlio pewa Kitabu alicho teremsha Mwenyezi Mungu! Iaminini Qur'ani tuliyo mteremshia Muhammad, inayo sadikisha mliyo nayo, kabla hatujawateremshia adhabu ya kufutwa nyuso zenu zikawa kama visogo, hazina pua, wala macho, wala nyusi. Au tukakutoeni katika rehema yetu kama tulivyo watoa wale walio ikhalifu amri yetu wakatenda waliyo katazwa ya kuvua samaki siku ya mapumziko,(Sabt au Sabato) siku ya Jumaamosi. Na hukumu ya Mwenyezi Mungu ni yenye kutimizwa tu, wala hapana cha kuipinga.

التفاسير:

external-link copy
48 : 4

إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَغۡفِرُ أَن يُشۡرَكَ بِهِۦ وَيَغۡفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَآءُۚ وَمَن يُشۡرِكۡ بِٱللَّهِ فَقَدِ ٱفۡتَرَىٰٓ إِثۡمًا عَظِيمًا

Hakika Mwenyezi Mungu hasamehe kushirikishwa, na husamehe yaliyo duni ya hilo kwa amtakaye. Na anaye mshirikisha Mwenyezi Mungu basi hakika amezua dhambi kubwa. info

Hakika Mwenyezi Mungu hafuti dhambi za ushirikina, kumfanya Yeye ana mshirika yeyote. Na husamehe dhambi zilio chini ya huo ushirikina kwa amtakaye miongoni mwa waja wake. Na mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu basi amemzulia Mwenyezi Mungu na ametenda dhambi kubwa mno isiyo stahiki kusamehewa.

التفاسير:

external-link copy
49 : 4

أَلَمۡ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ يُزَكُّونَ أَنفُسَهُمۚ بَلِ ٱللَّهُ يُزَكِّي مَن يَشَآءُ وَلَا يُظۡلَمُونَ فَتِيلًا

Jee huwaoni wale wanao dai kuwa ati wametakasika? Bali Mwenyezi Mungu humtakasa amtakaye. Na hawatadhulumiwa hata kadiri ya kijiuzi kilichomo ndani ya uwazi wa kokwa ya tende. info

Hustaajabii hali ya hao makafiri wanao zua kwa vitendo vyao? Vitendo vyao viovu wao wanaviona kuwa ni vizuri. Wanajisifu kuwa kwa vitendo hivyo wao wametakasika. Na ni Mwenyezi Mungu tu peke yake ndiye anaye jua jema na baya. Yeye ndiye wa kumtakasa amtakaye, na wala hamdhulumu mtu yeyote kadiri yake hata chembe.

التفاسير:

external-link copy
50 : 4

ٱنظُرۡ كَيۡفَ يَفۡتَرُونَ عَلَى ٱللَّهِ ٱلۡكَذِبَۖ وَكَفَىٰ بِهِۦٓ إِثۡمٗا مُّبِينًا

Tazama vipi wanavyo mzulia uwongo Mwenyezi Mungu, na haya yatosha kuwa dhambi iliyo dhaahiri. info

Vipi watu hawa wanavyo mzulia Mwenyezi Mungu uwongo kwa haya na mengineyo mfano wa haya! Yatosha uwovu ulio wazi kwa huu uwongo wao kuyakashifu maovu yao.

التفاسير:

external-link copy
51 : 4

أَلَمۡ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ أُوتُواْ نَصِيبٗا مِّنَ ٱلۡكِتَٰبِ يُؤۡمِنُونَ بِٱلۡجِبۡتِ وَٱلطَّٰغُوتِ وَيَقُولُونَ لِلَّذِينَ كَفَرُواْ هَٰٓؤُلَآءِ أَهۡدَىٰ مِنَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ سَبِيلًا

Huwaoni wale walio pewa sehemu ya Kitabu? Wanaamini masanamu na Shet'ani! Na wanawasema walio kufuru, kuwa hao wameongoka zaidi katika njia kuliko Walio amini. info

Hebu huwastaajabii hawa walio pewa sehemu ya ujuzi wa Kitabu wanavyo ridhia ibada ya masanamu na Shetani, na wanavyo sema kuwa hao waabuduo masanamu ni afadhali wameongoka kwenye Njia kuliko Waislamu wenye kuamini?

التفاسير: