ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាswahili - អាប់ឌុលឡោះ ម៉ូហាំម៉ាត់ និងណាសៀរ ខមុីស

លេខ​ទំព័រ:close

external-link copy
23 : 3

أَلَمۡ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ أُوتُواْ نَصِيبٗا مِّنَ ٱلۡكِتَٰبِ يُدۡعَوۡنَ إِلَىٰ كِتَٰبِ ٱللَّهِ لِيَحۡكُمَ بَيۡنَهُمۡ ثُمَّ يَتَوَلَّىٰ فَرِيقٞ مِّنۡهُمۡ وَهُم مُّعۡرِضُونَ

Je, umeona, ewe Mtume, hali ya kustaajabisha zaidi kuliko hali ya hawa Mayahudi, ambao Mwenyezi Mungu Amewapa fungu katika Kitabu wakajua kuwa yale uliyoyaleta ni haki, wanaitwa wafuate yaliyokuja katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu, nacho ni Qur’ani, ili kitoe uamuzi katika mambo waliotafautiana juu yake, kisha wengi wao wanakataa uamuzi huo iwapo haulingani na matamanio yao, kwa kuwa desturi yao ni ni kuipa mgongo haki? info
التفاسير:

external-link copy
24 : 3

ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمۡ قَالُواْ لَن تَمَسَّنَا ٱلنَّارُ إِلَّآ أَيَّامٗا مَّعۡدُودَٰتٖۖ وَغَرَّهُمۡ فِي دِينِهِم مَّا كَانُواْ يَفۡتَرُونَ

kujiepusha huko na haki, sababu yake ni itikadi mbaya walionayo Watu wa Kitabu kwamba wao hawataadhibiwa isipokuwa siku chache. Itikadi hii iliwapelekea wao wamfanyiye ujasiri Mwenyezi Mungu na waidharau Dini Yake na waendelee na dini yao ya batili ambayo walijidanganya nayo nafsi zao. info
التفاسير:

external-link copy
25 : 3

فَكَيۡفَ إِذَا جَمَعۡنَٰهُمۡ لِيَوۡمٖ لَّا رَيۡبَ فِيهِ وَوُفِّيَتۡ كُلُّ نَفۡسٖ مَّا كَسَبَتۡ وَهُمۡ لَا يُظۡلَمُونَ

Vipi hali zao zitakuwa, Atakapowakusanya Mwenyezi Mungu ili wahesabiwe katika Siku isiyo na shaka kuja kwake, nayo ni Siku ya Kiyama, na kila mmoja apate malipo ya aliyoyatenda, na wao bila kudhulumiwa kitu chochote? info
التفاسير:

external-link copy
26 : 3

قُلِ ٱللَّهُمَّ مَٰلِكَ ٱلۡمُلۡكِ تُؤۡتِي ٱلۡمُلۡكَ مَن تَشَآءُ وَتَنزِعُ ٱلۡمُلۡكَ مِمَّن تَشَآءُ وَتُعِزُّ مَن تَشَآءُ وَتُذِلُّ مَن تَشَآءُۖ بِيَدِكَ ٱلۡخَيۡرُۖ إِنَّكَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ

Sema ,ewe Nabii, ukielekea kwa Mola wako kwa dua, «Ewe Ambaye Una ufalme wote, Wewe Ndiye Ambaye Unamtunuku ufalme, mali na umakinifu katika ardhi Umtakaye miongoni mwa waja Wako, na Unauondoa ufalme kutoka kwa Umtakaye. Na Unampa enzi ya ulimwengu na ya Akhera Unayemtaka, na Unamfanya awe na unyonge Unayemtaka. Kheri ipo mikononi mwako. Wewe, Peke Yako, juu ya kila kitu , ni Muweza.» Katika ayah hii pana kuthibitisha sifa ya Mkono kwa Mwenyezi Mungu kwa namna inayonasibiana na Yeye, utakatifu ni Wake. info
التفاسير:

external-link copy
27 : 3

تُولِجُ ٱلَّيۡلَ فِي ٱلنَّهَارِ وَتُولِجُ ٱلنَّهَارَ فِي ٱلَّيۡلِۖ وَتُخۡرِجُ ٱلۡحَيَّ مِنَ ٱلۡمَيِّتِ وَتُخۡرِجُ ٱلۡمَيِّتَ مِنَ ٱلۡحَيِّۖ وَتَرۡزُقُ مَن تَشَآءُ بِغَيۡرِ حِسَابٖ

«Na miongoni mwa dalili za uwezo Wako, ni kuwa Wewe Unautia usiku ndani ya mchana, na Unautia mchana ndani ya uslku, huu ukarefuka na ule ukafupika. Na Unatoa chenye uhai kutoka kwa kilichokufa kisichokuwa na uhai, kama kutoa mazao kutokana na mbegu na kama kumtoa Muumini kutoka kwa kafiri. Na Unatoa kilichokufa kutoka kwa chenye uhai, kama kutoa yai kwenye kuku. Na Unamruzuku Unayemtaka katika waja Wako bila hesabu.» info
التفاسير:

external-link copy
28 : 3

لَّا يَتَّخِذِ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ ٱلۡكَٰفِرِينَ أَوۡلِيَآءَ مِن دُونِ ٱلۡمُؤۡمِنِينَۖ وَمَن يَفۡعَلۡ ذَٰلِكَ فَلَيۡسَ مِنَ ٱللَّهِ فِي شَيۡءٍ إِلَّآ أَن تَتَّقُواْ مِنۡهُمۡ تُقَىٰةٗۗ وَيُحَذِّرُكُمُ ٱللَّهُ نَفۡسَهُۥۗ وَإِلَى ٱللَّهِ ٱلۡمَصِيرُ

Mwenyezi Mungu Anawakataza Waumini kuwafanya makafiri kuwa ni wategemewa, kwa mapenzi na kwa kutaka himaya, badala ya Waumini. Na yoyote mwenye kuwafanya wao ni wategemewa, huyo ameshakuwa mbali na Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu Yuko mbali na yeye. Isipokuwa mkiwa ni madhaifu wenye kuogopa, hapo Mwenyezi Mungu Amewapa ruhusa muwasairi ili kujiepusha na shari lao, mpaka mtakapopata nguvu. Na Mwenyezi Mungu Anawatahadharisha nyinyi na Yeye. basi mcheni na muogopeni. Na Kwake Peke Yake ndio marejeo ya viumbe kwa kuhesabiwa na kulipwa. info
التفاسير:

external-link copy
29 : 3

قُلۡ إِن تُخۡفُواْ مَا فِي صُدُورِكُمۡ أَوۡ تُبۡدُوهُ يَعۡلَمۡهُ ٱللَّهُۗ وَيَعۡلَمُ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۗ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ

Sema, ewe Nabii, Kuwaambia Waumini, «Mkiyaficha yaliyomo ndani ya nyoyo zenu ya kuwafanya makafiri ni wategemewa na wasaidizi au mkiyadhihirisha hayo, hakitafichika chochote katika hayo kwa Mwenyezi Mungu. Kwani ujuzi Wake umezunguka kila kilichoko mbinguni na kilichoko ardhini, na Ana uwezo kamili juu ya kila kitu. info
التفاسير: