ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាswahili - អាប់ឌុលឡោះ ម៉ូហាំម៉ាត់ និងណាសៀរ ខមុីស

លេខ​ទំព័រ:close

external-link copy
101 : 3

وَكَيۡفَ تَكۡفُرُونَ وَأَنتُمۡ تُتۡلَىٰ عَلَيۡكُمۡ ءَايَٰتُ ٱللَّهِ وَفِيكُمۡ رَسُولُهُۥۗ وَمَن يَعۡتَصِم بِٱللَّهِ فَقَدۡ هُدِيَ إِلَىٰ صِرَٰطٖ مُّسۡتَقِيمٖ

Na vipi mtamkufuru Mwenyezi Mungu, enyi Waumini, ilhali mnasomewa aya za Qur’ani, na Mtume wa Mwenyezi Mungu, Muhammad , rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, anazifikisha aya hizo kwenu? Na yoyote atakayetegemea kwa Mwenyezi Mungu, akashikamana na Qur’ani na mafundisho ya Mtume (Sunnah), basi huyo ameafikiwa kufuata njia iliyo wazi na mpango uliolingana sawa. info
التفاسير:

external-link copy
102 : 3

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱتَّقُواْ ٱللَّهَ حَقَّ تُقَاتِهِۦ وَلَا تَمُوتُنَّ إِلَّا وَأَنتُم مُّسۡلِمُونَ

Enyi ambao mumemuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mkazifuata Sheria Zake, muogopeni Mwenyezi Mungu kwa namna inavyopasa mumuogope. Nako ni Atiiwe wala Asiasiwe, Ashukuriwe wala asikufuriwe na Akumbukwe wala Asisahauliwe. Na dumuni katika kushikamana na Uislamu wenu mpaka mwisho wa uhai wenu, ili mkutane na Mwenyezi Mungu na nyinyi muko katika hali hiyo. info
التفاسير:

external-link copy
103 : 3

وَٱعۡتَصِمُواْ بِحَبۡلِ ٱللَّهِ جَمِيعٗا وَلَا تَفَرَّقُواْۚ وَٱذۡكُرُواْ نِعۡمَتَ ٱللَّهِ عَلَيۡكُمۡ إِذۡ كُنتُمۡ أَعۡدَآءٗ فَأَلَّفَ بَيۡنَ قُلُوبِكُمۡ فَأَصۡبَحۡتُم بِنِعۡمَتِهِۦٓ إِخۡوَٰنٗا وَكُنتُمۡ عَلَىٰ شَفَا حُفۡرَةٖ مِّنَ ٱلنَّارِ فَأَنقَذَكُم مِّنۡهَاۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ ٱللَّهُ لَكُمۡ ءَايَٰتِهِۦ لَعَلَّكُمۡ تَهۡتَدُونَ

Shikamaneni nyote na Kitabu cha Mola wenu na uongofu wa Mtume wenu, wala msitende ambayo yatapelekea kutengana kwenu. Na ikumbukeni neema kubwa ambayo Mwenyezi Mungu Amewaneemesha nayo, pindi mlipokuwa, enyi Waumini, kabla ya Uislamu ni maadui, Mwenyezi Mungu Akazikusanya nyoyo zenu juu ya kumpenda Yeye na kumpenda Mtume Wake, na akatia ndani ya nyoyo zenu mahaba ya kupendana wenyewe kwa wenyewe, hapo mkawa, kwa fadhila Zake, ni ndugu mpedanao. Na mlikuwa kwenye ukingo wa moto wa Jahanamu, Mwenyezi Mungu Akawaongoza kwa Uislamu na Akawaokoa na Moto. Na kama Mwenyezi Mungu Alivyowafunulia wazi alama za imani iliyo sahihi, hivyo hivyo Anawabainishia yote yale ambayo ndani yake muna kutengenea kwenu, mpate kuongoka kweye njia ya uongofu na mpate kuiandama ili msipotee mkaiepuka. info
التفاسير:

external-link copy
104 : 3

وَلۡتَكُن مِّنكُمۡ أُمَّةٞ يَدۡعُونَ إِلَى ٱلۡخَيۡرِ وَيَأۡمُرُونَ بِٱلۡمَعۡرُوفِ وَيَنۡهَوۡنَ عَنِ ٱلۡمُنكَرِۚ وَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡمُفۡلِحُونَ

Na kiweko miongoni mwenu, enyi Waumini, kikundi kitakacholingania katika kheri, kiamrishe mema, nayo ni yale yanayojulikana uzuri wake kisheria na kiakili, na kikataze maovu, nayo ni yale yanayojulikana uovu wake kisheria na kiakili. Na hao ndio watakaofaulu kupata Pepo zenye neema. info
التفاسير:

external-link copy
105 : 3

وَلَا تَكُونُواْ كَٱلَّذِينَ تَفَرَّقُواْ وَٱخۡتَلَفُواْ مِنۢ بَعۡدِ مَا جَآءَهُمُ ٱلۡبَيِّنَٰتُۚ وَأُوْلَٰٓئِكَ لَهُمۡ عَذَابٌ عَظِيمٞ

Na wala msiwe, enyi Waumini, kama waliopewa vitabu, ambao ulizuka uadui kati yao na kuchukiana, wakatengana makundi na vyama mbalimbali na wakatafautiana kwenye misingi ya dini yao baada ya haki kuwa wazi kwao. Na hao wanastahili adhabu kubwa iumizayo. info
التفاسير:

external-link copy
106 : 3

يَوۡمَ تَبۡيَضُّ وُجُوهٞ وَتَسۡوَدُّ وُجُوهٞۚ فَأَمَّا ٱلَّذِينَ ٱسۡوَدَّتۡ وُجُوهُهُمۡ أَكَفَرۡتُم بَعۡدَ إِيمَٰنِكُمۡ فَذُوقُواْ ٱلۡعَذَابَ بِمَا كُنتُمۡ تَكۡفُرُونَ

Siku ya Kiyama zitakuwa nyeupe nyuso za watu wema ambao wamemuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na wakafuata amri Yake; na zitakuwa nyeusi nyuso za watu waovu kati ya wale waliomkanusha Mtume Wake na wakaasi amri Yake. Basi wale ambao nyuso zao zitakuwa nyeusi wataambiwa kwa kulaumiwa, «Je, mumekufuru baada ya kuamini kwenu, mkachagua ukafiri mkaacha Imani? Basi ionjeni adhabu kwa sababu ya ukafiri wenu.» info
التفاسير:

external-link copy
107 : 3

وَأَمَّا ٱلَّذِينَ ٱبۡيَضَّتۡ وُجُوهُهُمۡ فَفِي رَحۡمَةِ ٱللَّهِۖ هُمۡ فِيهَا خَٰلِدُونَ

Ama wale ambao nyuso zao zitakuwa nyeupe kwa mn’garo wa neema na kwa yale mema ambayo walipewa bishara nayo, wao watakuwa katika Pepo ya Mwenyezi Mungu na starehe zake. Wao watasalia humo, hawatatoka humo milele. info
التفاسير:

external-link copy
108 : 3

تِلۡكَ ءَايَٰتُ ٱللَّهِ نَتۡلُوهَا عَلَيۡكَ بِٱلۡحَقِّۗ وَمَا ٱللَّهُ يُرِيدُ ظُلۡمٗا لِّلۡعَٰلَمِينَ

Hizi ni aya za Mwenyezi Mungu na hoja Zake zenye kung’ara, tunakusomea na kukusimulia, ewe Mtume, kwa ukweli na yakini. Na Mwenyezi Mungu Hakuwa ni mweye kumdhulumu yoyote katika viumbe Wake wala si mwenye kupunguza chochote katika vitendo vyao, kwani Yeye ni Hakimu Mwenye uadilifu Asiyedhulumu. info
التفاسير: