Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Abdullah Muhammad & Naser Khamis

Page Number: 169:151 close

external-link copy
156 : 7

۞ وَٱكۡتُبۡ لَنَا فِي هَٰذِهِ ٱلدُّنۡيَا حَسَنَةٗ وَفِي ٱلۡأٓخِرَةِ إِنَّا هُدۡنَآ إِلَيۡكَۚ قَالَ عَذَابِيٓ أُصِيبُ بِهِۦ مَنۡ أَشَآءُۖ وَرَحۡمَتِي وَسِعَتۡ كُلَّ شَيۡءٖۚ فَسَأَكۡتُبُهَا لِلَّذِينَ يَتَّقُونَ وَيُؤۡتُونَ ٱلزَّكَوٰةَ وَٱلَّذِينَ هُم بِـَٔايَٰتِنَا يُؤۡمِنُونَ

«Na utujaalie ni miongoni mwa wale uliowaandikia matendo mema ulimwenguni na Akhera. Sisi tumerejea kwako hali ya kutubia.» Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Akasema kumwambia Mūsā, «Adhabu yangu nitampatiliza kwayo ninayemtaka miongoni mwa viumbe wangu, kama nilivyowapatiliza hawa niliowapatia katika watu wako, na rehema yangu imewaenea viumbe wangu wote, nitawaandikia wale wanaomcha Mwenyezi Mungu na kuogopa mateso Yake, wakazitekeleza faradhi Zake na wakayaepuka mambo ya kumuasi, na wale ambao wao wanaziamini dalili za tawhīd (kumpwekesha Mwenyezi Mungu) na hoja zake. info
التفاسير:

external-link copy
157 : 7

ٱلَّذِينَ يَتَّبِعُونَ ٱلرَّسُولَ ٱلنَّبِيَّ ٱلۡأُمِّيَّ ٱلَّذِي يَجِدُونَهُۥ مَكۡتُوبًا عِندَهُمۡ فِي ٱلتَّوۡرَىٰةِ وَٱلۡإِنجِيلِ يَأۡمُرُهُم بِٱلۡمَعۡرُوفِ وَيَنۡهَىٰهُمۡ عَنِ ٱلۡمُنكَرِ وَيُحِلُّ لَهُمُ ٱلطَّيِّبَٰتِ وَيُحَرِّمُ عَلَيۡهِمُ ٱلۡخَبَٰٓئِثَ وَيَضَعُ عَنۡهُمۡ إِصۡرَهُمۡ وَٱلۡأَغۡلَٰلَ ٱلَّتِي كَانَتۡ عَلَيۡهِمۡۚ فَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ بِهِۦ وَعَزَّرُوهُ وَنَصَرُوهُ وَٱتَّبَعُواْ ٱلنُّورَ ٱلَّذِيٓ أُنزِلَ مَعَهُۥٓ أُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡمُفۡلِحُونَ

Rehema hii nitawaandikia wale wanaomuogopa Mwenyezi Mungu na kujiepusha na mambo ya kumuasi, na wanaomfuata Mtume aliye Nabii, ambaye hasomi wala haandiki, naye ni Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani imshukiye, ambaye wanazipata sifa zake na mambo yake yaandikwa huko kwao katika Taurati na Injili; anawaamrisha kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kumtii na kila lijulikanalo kuwa ni lema, na anawakataza ushirikina na maasia na kila lijulikanalo kuwa ni baya, na anawahalalishia vizuri vya vyakula na vinywaji na kuoana, na anawaharamishla vichafu vya hivyo kama nyama ya nguruwe na vile ambavyo walikuwa wakijihalalishia miongoni mwa vyakula na vinywaji ambavyo aliviharamisha Mwenyezi Mungu, na anawaondolea wao mambo magumu waliokalifishwa nayo kama kukata mahali pa najisi nguoni, kuzichoma moto ngawira, ulazimu wa kisasi juu ya aliyeua kwa kukusudia au kwa kukosea. Basi wale ambao walimuamini Nabii asiyejua kuandika wala kusoma kilichoandikwa, Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani imshukiye, na wakaukubali unabii wake, wakamheshimu, wakamtukuza na wakamuhami na wakaifuata Qur’ani aliyoteremshiwa, wakaufuata mwendo wake kivitendo, hao ni wenye kufaulu kwa kupata yale ambayo Mwenyezi Mungu Aliwaahidi waja wake Waumini. info
التفاسير:

external-link copy
158 : 7

قُلۡ يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ إِنِّي رَسُولُ ٱللَّهِ إِلَيۡكُمۡ جَمِيعًا ٱلَّذِي لَهُۥ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۖ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ يُحۡيِۦ وَيُمِيتُۖ فَـَٔامِنُواْ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِ ٱلنَّبِيِّ ٱلۡأُمِّيِّ ٱلَّذِي يُؤۡمِنُ بِٱللَّهِ وَكَلِمَٰتِهِۦ وَٱتَّبِعُوهُ لَعَلَّكُمۡ تَهۡتَدُونَ

Waambie, ewe Mtume, watu wote, «Mimi ni mjumbe wa Mwenyezi Mungu kwenu nyote, si kwa baadhi yenu bila ya wengine, Ambaye ni wake ufalme wa mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake. Haifai kuelekezwa uungu na ibada isipokuwa Kwake, zilizotukuka sifa Zake, Mwenye uwezo wa kupatisha viumbe, kuwaondosha na kuwafufua. Basi muaminini Mwenyezi Mungu na kubalini upweke Wake, na muaminini Mtume Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani imshukiye, Nabii asiyesoma wala kwandika, anayemuamini Mwenyezi Mungu na yale aliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wake na yale waliyoteremshiwa manabii kabla yake; Mfuateni Mtume huyu na jilazimisheni kuyafanya anayowaamrisha kwayo ya kumtii Mwenyezi Mungu kwa kutaraji muafikiwe kufuata njia iliyolingana sawa.» info
التفاسير:

external-link copy
159 : 7

وَمِن قَوۡمِ مُوسَىٰٓ أُمَّةٞ يَهۡدُونَ بِٱلۡحَقِّ وَبِهِۦ يَعۡدِلُونَ

Na miongoni mwa Wana wa Isrāīl wanaotokana na jamaa za Mūsā kuna kundi la watu ambao wanasimama imara juu ya haki, wanawaongoza watu kwenye hiyo haki na wanafanya usawa katika kutoa uamuzi katika mambo yao. info
التفاسير: