Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Abdullah Muhammad & Naser Khamis

Page Number:close

external-link copy
144 : 7

قَالَ يَٰمُوسَىٰٓ إِنِّي ٱصۡطَفَيۡتُكَ عَلَى ٱلنَّاسِ بِرِسَٰلَٰتِي وَبِكَلَٰمِي فَخُذۡ مَآ ءَاتَيۡتُكَ وَكُن مِّنَ ٱلشَّٰكِرِينَ

Mwenyezi Mungu Akasema, «Ewe Mūsā, Mimi nimekuchagua kati ya watu kwa ujumbe wangu kwa viumbe wangu niliokutuma kwao na kwa kusema kwangu na wewe pasi na mtu wa kati. Basi chukua niliyokupa kati ya maamrisho yangu na makatazo yangu, ushikamane nayo na uyatumie na uwe ni miongoni mwa wenye kumshukuru Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, kwa utume aliokupa na Akakuhusu kwa maneno Yake. info
التفاسير:

external-link copy
145 : 7

وَكَتَبۡنَا لَهُۥ فِي ٱلۡأَلۡوَاحِ مِن كُلِّ شَيۡءٖ مَّوۡعِظَةٗ وَتَفۡصِيلٗا لِّكُلِّ شَيۡءٖ فَخُذۡهَا بِقُوَّةٖ وَأۡمُرۡ قَوۡمَكَ يَأۡخُذُواْ بِأَحۡسَنِهَاۚ سَأُوْرِيكُمۡ دَارَ ٱلۡفَٰسِقِينَ

Na tulimuandikia Mūsā katika Taurati mawaidha ya kila anachokihitajia katika hukumu za Dini yake, ili yapatikane makemeo na mazingatio, na maelezo yanayofafanua mambo ambayo walikalifishwa nayo ya halali na ya haramu, maamrisho na makatazo, visa, mambo ya itikadi, habari na mambo yasiyoonekana. Mwenyezi Mungu Alimwambia, «Basi yashike kwa nguvu.» Yaani, ishike Taurati kwa kwa bidii na hima. «Na uwaamrishe watu wako wazitumie sheria za Mwenyezi Mungu zilizomo humo. Hakika mwenye kushirikisha miongoni mwao na wengineo, mimi nitamuonesha huko Akhera nyumba ya waasi, nayo ni Moto wa Mwenyezi Mungu ambao Ameutayarisha kwa maadui Wake waliyotoka nje ya utiifu Wake.» info
التفاسير:

external-link copy
146 : 7

سَأَصۡرِفُ عَنۡ ءَايَٰتِيَ ٱلَّذِينَ يَتَكَبَّرُونَ فِي ٱلۡأَرۡضِ بِغَيۡرِ ٱلۡحَقِّ وَإِن يَرَوۡاْ كُلَّ ءَايَةٖ لَّا يُؤۡمِنُواْ بِهَا وَإِن يَرَوۡاْ سَبِيلَ ٱلرُّشۡدِ لَا يَتَّخِذُوهُ سَبِيلٗا وَإِن يَرَوۡاْ سَبِيلَ ٱلۡغَيِّ يَتَّخِذُوهُ سَبِيلٗاۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمۡ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا وَكَانُواْ عَنۡهَا غَٰفِلِينَ

Nitazipotoa nyoyo za wenye kufanya kiburi wakaacha kunitii na wenye kuwafanyia watu kiburi pasi na haki zisizielewe hoja na dalili zinazoonesha ukubwa wangu, sheria yangu na hukumu zangu, wawe hawamsikilizi Mtume yoyote kwa kiburi chao. Na wakiona, hawa wenye kuifanyia Imani kiburi, kila alama hawaiyamini, kwa sababu ya kupa mgongo kwao na kupingana kwao na Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. Wakiiyona njia ya uongofu hawaifanyi ni njia, na wakiiyona njia ya upotevu wanaifanya kuwa ni njia na ni dini. Hayo ni kwa sababu ya kukanusha kwao aya za Mwenyezi Mungu na kughafilika kwao kuziangalia na kuyatia akilini maana yake. info
التفاسير:

external-link copy
147 : 7

وَٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا وَلِقَآءِ ٱلۡأٓخِرَةِ حَبِطَتۡ أَعۡمَٰلُهُمۡۚ هَلۡ يُجۡزَوۡنَ إِلَّا مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ

Na wale ambao walizikanusha aya za Mwenyezi Mungu, hoja Zake na kukutana na Mwenyezi Mungu huko Akhera, matendo yao mema yatapomoka kwa sababu ya kukosekana sharti yake, nayo ni kumuamini Mwenyezi Mungu na kukubali kwamba malipo Yake ni kweli. Hawatalipwa huko Akhera isipokuwa malipo ya yale ambayo walikuwa wakiyafanya ulimwenguni ya ukafiri na maasia, nayo ni kukaa milele Motoni. info
التفاسير:

external-link copy
148 : 7

وَٱتَّخَذَ قَوۡمُ مُوسَىٰ مِنۢ بَعۡدِهِۦ مِنۡ حُلِيِّهِمۡ عِجۡلٗا جَسَدٗا لَّهُۥ خُوَارٌۚ أَلَمۡ يَرَوۡاْ أَنَّهُۥ لَا يُكَلِّمُهُمۡ وَلَا يَهۡدِيهِمۡ سَبِيلًاۘ ٱتَّخَذُوهُ وَكَانُواْ ظَٰلِمِينَ

Na walitengeneza watu wa Mūsā, baada ya yeye kuwaacha kwenda kuzungumza na Mola Wake, sanamu wa kigombe asiye na roho anayetoa sauti, kutokana na dhahabu yao, wakamfanya ni muabudiwa. Kwani hawajui kwamba yeye hasemi na wao na hawaongozi wao kwenye kheri yoyote? Walijasiri kufanya jambo hili ovu, wakawa ni wenye kujidhulumu nafsi zao, ni wenye kuweka kitu mahala pasipokuwa pake. info
التفاسير:

external-link copy
149 : 7

وَلَمَّا سُقِطَ فِيٓ أَيۡدِيهِمۡ وَرَأَوۡاْ أَنَّهُمۡ قَدۡ ضَلُّواْ قَالُواْ لَئِن لَّمۡ يَرۡحَمۡنَا رَبُّنَا وَيَغۡفِرۡ لَنَا لَنَكُونَنَّ مِنَ ٱلۡخَٰسِرِينَ

Na walipojuta wale walioabudu kigombe badala ya Mwenyezi Mungu pale aliporudi Mūsā kwao, na wakaona kwamba walipotea njia ya sawa, na waliondoka kwenye dini ya Mwenyezi Mungu, walianza kuukubali uja na kuomba kufutiwa makosa yao wakasema, «Mola wetu Asipoturehemu kwa kukubali toba yetu, na kufinika kwayo madhambi yetu, tutakuwa ni wenye kuangamia ambao matendo yao mema yamepita bure.» info
التفاسير: