Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Abdullah Muhammad & Naser Khamis

Page Number:close

external-link copy
96 : 7

وَلَوۡ أَنَّ أَهۡلَ ٱلۡقُرَىٰٓ ءَامَنُواْ وَٱتَّقَوۡاْ لَفَتَحۡنَا عَلَيۡهِم بَرَكَٰتٖ مِّنَ ٱلسَّمَآءِ وَٱلۡأَرۡضِ وَلَٰكِن كَذَّبُواْ فَأَخَذۡنَٰهُم بِمَا كَانُواْ يَكۡسِبُونَ

Na lau watu wa miji waliwaamini Mitume wao wakawafuata na kujiepusha na aliyoyakataza Mwenyezi Mungu, Angaliwafungulia Mwenyezi Mungu milango ya heri kwa kila njia. Lakini wao walikanusha, Mwenyezi Mungu Akawatesa kwa adhabu yenye kuangamiza kwa sababu ya ukafiri wao na maasia yao. info
التفاسير:

external-link copy
97 : 7

أَفَأَمِنَ أَهۡلُ ٱلۡقُرَىٰٓ أَن يَأۡتِيَهُم بَأۡسُنَا بَيَٰتٗا وَهُمۡ نَآئِمُونَ

Kwani wanadhani hawa watu wa mijini kuwa wao wameokoka na wamesalimika na adhabu ya Mwenyezi Mungu kuwa haitawafika kipindi cha usiku wakiwa wamelala? info
التفاسير:

external-link copy
98 : 7

أَوَأَمِنَ أَهۡلُ ٱلۡقُرَىٰٓ أَن يَأۡتِيَهُم بَأۡسُنَا ضُحٗى وَهُمۡ يَلۡعَبُونَ

Au kwani wanajiaminisha watu wa mijini kuwa wamesalimika na adhabu ya Mwenyezi Mungu kuwa haitawafika kipindi cha mchana wakiwa wameghafilika, wameshughulika na mambo ya dunia yao? Mwenyezi Mungu Amezihusu nyakati mbili hizi kwa kuzitaja, kwa kuwa mwanadamu nyakati hizi huwa wameghafilika zaidi, kwa hivyo kuja adhabu katika nyakati hizi huwa na kitisho zaidi na ni kali zaidi. info
التفاسير:

external-link copy
99 : 7

أَفَأَمِنُواْ مَكۡرَ ٱللَّهِۚ فَلَا يَأۡمَنُ مَكۡرَ ٱللَّهِ إِلَّا ٱلۡقَوۡمُ ٱلۡخَٰسِرُونَ

Je, wamejiaminisha, watu wa miji iliyokanusha, na vitimbi vya Mwenyezi Mungu kwao na kuwapa Kwake wao muhula, kwa kuwaachilia na yale Aliyowaneemesha nayo katika dunia yao, kwa njia ya kuwatesa sababu ya vitimbi vyao? Basi hawajiaminishi na vitimbi vya Mwenyezi Mungu isipokuwa watu wenye kuangamia. info
التفاسير:

external-link copy
100 : 7

أَوَلَمۡ يَهۡدِ لِلَّذِينَ يَرِثُونَ ٱلۡأَرۡضَ مِنۢ بَعۡدِ أَهۡلِهَآ أَن لَّوۡ نَشَآءُ أَصَبۡنَٰهُم بِذُنُوبِهِمۡۚ وَنَطۡبَعُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمۡ فَهُمۡ لَا يَسۡمَعُونَ

Kwani haikuwafunukia wale waliokaa kwenye nchi baada ya watu wake waliopita kuangamizwa kwa maasia yao, na wakafuata miendo yao, kwamba lau tunataka tungaliwaadhibu kwa makosa yao, kama tulivyowafanyia waliopita kabla yao, na kwamba tutazipiga chapa nyoyo zao, haki isiingie na wasisikie mawaidha wala makumbusho? info
التفاسير:

external-link copy
101 : 7

تِلۡكَ ٱلۡقُرَىٰ نَقُصُّ عَلَيۡكَ مِنۡ أَنۢبَآئِهَاۚ وَلَقَدۡ جَآءَتۡهُمۡ رُسُلُهُم بِٱلۡبَيِّنَٰتِ فَمَا كَانُواْ لِيُؤۡمِنُواْ بِمَا كَذَّبُواْ مِن قَبۡلُۚ كَذَٰلِكَ يَطۡبَعُ ٱللَّهُ عَلَىٰ قُلُوبِ ٱلۡكَٰفِرِينَ

Miji hiyo iliyotangulia kutajwa, nayo ni miji ya watu wa Nūḥ„ Hūd, Ṣāliḥ, Lūṭ, na Shu'ayb, tunakupatia, ewe Mtume, habari zake na zile zinazohusu mambo ya Mitume wa Mwenyezi Mungu waliotumwa kwa watu wa miji hiyo, zinazofanya mazingatio yapatikane kwa wenye kuzingatia na pia makemeo kwa madhalimu. Hakika watu wa miji hiyo walijiwa na Mitume wetu na hoja zilizo wazi juu ya ukweli wao, lakini hawakuwa ni wenye kuyaamini yale waliyokuja nayo hao Mitume kwao kwa sababu ya kupita mipaka kwao na kuikanusha haki. Na mfano Alivyopiga chapa Mwenyezi Mungu kwenye nyoyo za makafiri hawa waliotajwa, Atapiga mhuri kwenye nyoyo za wenye kumkanusha Muhammad (S.A.W.). info
التفاسير:

external-link copy
102 : 7

وَمَا وَجَدۡنَا لِأَكۡثَرِهِم مِّنۡ عَهۡدٖۖ وَإِن وَجَدۡنَآ أَكۡثَرَهُمۡ لَفَٰسِقِينَ

Na hatukuwapata wengi wa watu waliopita kuwa wana uaminifu wala utekelezaji ahadi, na hatukuwapata wengi wao isipokuwa ni watokaji nje ya utiifu wa Mwenyezi Mungu na ufuataji amri Yake. info
التفاسير:

external-link copy
103 : 7

ثُمَّ بَعَثۡنَا مِنۢ بَعۡدِهِم مُّوسَىٰ بِـَٔايَٰتِنَآ إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ وَمَلَإِيْهِۦ فَظَلَمُواْ بِهَاۖ فَٱنظُرۡ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلۡمُفۡسِدِينَ

Kisha tulimtuma, baada ya Mitume waliotangulia kutajwa, Mūsā mwana wa 'Imrān kwa miujiza yetu iliyo wazi aende kwa Fir'awn na watu wake, wakaikataa na kuikanusha kwa udhalimu na upinzani. Tazama kwa mazingatio, namna gani tuliwafanya na tuliwazamisha hadi wa mwisho wao, huku Mūsā na watu wake wakiona? Na huo ndio mwisho wa waharibifu. info
التفاسير:

external-link copy
104 : 7

وَقَالَ مُوسَىٰ يَٰفِرۡعَوۡنُ إِنِّي رَسُولٞ مِّن رَّبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ

Na Mūsā alisema kumwambia Fir'awn akimzungumzia na akimfikishia ujumbe, «Mimi ni mjumbe kutoka kwa Mwenyezi Mungu, Muumba viumbe wote na Mwenye kupanga hali zao na marejeo yao. info
التفاسير: