Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Abdullah Muhammad & Naser Khamis

Page Number:close

external-link copy
12 : 7

قَالَ مَا مَنَعَكَ أَلَّا تَسۡجُدَ إِذۡ أَمَرۡتُكَۖ قَالَ أَنَا۠ خَيۡرٞ مِّنۡهُ خَلَقۡتَنِي مِن نَّارٖ وَخَلَقۡتَهُۥ مِن طِينٖ

Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Akasema hali ya kumkemea Iblisi kwa kuacha kwake kumsujudia Ādam, «Ni lipi lililokuzuia usisujudu nilipokuamuru?» Iblisi akasema, «Mimi ni bora kuliko yeye, kwa kuwa mimi nimeumbwa kwa moto na yeye ameumbwa kwa udongo.» Akaona kuwa moto ni bora kuliko udongo. info
التفاسير:

external-link copy
13 : 7

قَالَ فَٱهۡبِطۡ مِنۡهَا فَمَا يَكُونُ لَكَ أَن تَتَكَبَّرَ فِيهَا فَٱخۡرُجۡ إِنَّكَ مِنَ ٱلصَّٰغِرِينَ

Mwenyezi Mungu Akasema kumwambia Iblisi, «Shuka kutoka Peponi, kwani haifai kwako kufanya ujeuri humo; toka Peponi, kwani wewe ni miongoni mwa wanyonge waliyo watwevu. info
التفاسير:

external-link copy
14 : 7

قَالَ أَنظِرۡنِيٓ إِلَىٰ يَوۡمِ يُبۡعَثُونَ

Iblisi akasema kumwambia Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka na kuwa juu, alipokata tamaa na rehema Yake, «Nipe muda mpaka Siku ya watu kufufuliwa, ili nipate kumpoteza ninayeweza kumpoteza kati ya wanadamu.» info
التفاسير:

external-link copy
15 : 7

قَالَ إِنَّكَ مِنَ ٱلۡمُنظَرِينَ

Akasema Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, «Wewe ni miongoni mwa wale niliowaandikia kucheleweshwa kipindi chao cha kufa mpaka Mvivio wa Kwanza katika Parapanda pindi viumbe wote watakapokufa.» info
التفاسير:

external-link copy
16 : 7

قَالَ فَبِمَآ أَغۡوَيۡتَنِي لَأَقۡعُدَنَّ لَهُمۡ صِرَٰطَكَ ٱلۡمُسۡتَقِيمَ

Iblisi akasema, Mwenyezi Mungu Amlaani, «Kwa sababu ya kuwa wewe umenipoteza, nitafanya bidii katika kuwapoteza binadamu wawe kando ya njia yako iliyolingana sawa na nitawazuia wao wasiuuandame Uislamu ambao wanasibiana na umbile lao ulilowaumbia. info
التفاسير:

external-link copy
17 : 7

ثُمَّ لَأٓتِيَنَّهُم مِّنۢ بَيۡنِ أَيۡدِيهِمۡ وَمِنۡ خَلۡفِهِمۡ وَعَنۡ أَيۡمَٰنِهِمۡ وَعَن شَمَآئِلِهِمۡۖ وَلَا تَجِدُ أَكۡثَرَهُمۡ شَٰكِرِينَ

«Kisha nitawajia kutoka pande zote na pambizo niwazuie wasiifuate haki, niwapambie batili, niwafanye wavutike na dunia na niwatie shaka kuhusu Akhera. Na hutawapata wengi wa wanadamu ni wenye kukushukuru wewe kwa neema zako.» info
التفاسير:

external-link copy
18 : 7

قَالَ ٱخۡرُجۡ مِنۡهَا مَذۡءُومٗا مَّدۡحُورٗاۖ لَّمَن تَبِعَكَ مِنۡهُمۡ لَأَمۡلَأَنَّ جَهَنَّمَ مِنكُمۡ أَجۡمَعِينَ

Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Akasema, kumwambia Iblisi, «Toka Peponi ukiwa umechukiwa na umefukuzwa. Nitaujaza Moto wa Jahanamu kwa kukuingiza wewe humo na binadamu wote watakaokufuata. info
التفاسير:

external-link copy
19 : 7

وَيَٰٓـَٔادَمُ ٱسۡكُنۡ أَنتَ وَزَوۡجُكَ ٱلۡجَنَّةَ فَكُلَا مِنۡ حَيۡثُ شِئۡتُمَا وَلَا تَقۡرَبَا هَٰذِهِ ٱلشَّجَرَةَ فَتَكُونَا مِنَ ٱلظَّٰلِمِينَ

«Na ewe Ādam, keti wewe pamoja na mke wako Ḥawwā’ Peponi na kuleni matunda yaliyo humo popote mnapotaka na wala msile matunda ya mti huu (Aliwatajia mti huo), mkifanya hilo mtakuwa ni madhalumu wenye kukiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu.» info
التفاسير:

external-link copy
20 : 7

فَوَسۡوَسَ لَهُمَا ٱلشَّيۡطَٰنُ لِيُبۡدِيَ لَهُمَا مَا وُۥرِيَ عَنۡهُمَا مِن سَوۡءَٰتِهِمَا وَقَالَ مَا نَهَىٰكُمَا رَبُّكُمَا عَنۡ هَٰذِهِ ٱلشَّجَرَةِ إِلَّآ أَن تَكُونَا مَلَكَيۡنِ أَوۡ تَكُونَا مِنَ ٱلۡخَٰلِدِينَ

Hapo Shetani aliwashawishi Ādam na Ḥawwā’ ili awatokomeze kwenye kumuasi Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, kwa kula matunda ya mti ule ambao Mwenyezi Mungu Aliwakataza kuula, ili mwisho wao uwe ni kufunukwa na tupu zao zilizokuwa zimesitiriwa. Na akawaambia, katika kujaribu kwake kuwafanyia vitimbi, «Hakika Mola wenu Amewakataza kula matunda ya mti huu ili msipate kuwa Malaika na ili msipate kuwa ni miongoni mwa wenye kuishi milele.» info
التفاسير:

external-link copy
21 : 7

وَقَاسَمَهُمَآ إِنِّي لَكُمَا لَمِنَ ٱلنَّٰصِحِينَ

Na Shetani Aliwaapia Ādam na Ḥawwā’ kwa Mwenyezi Mungu kwamba yeye ni miongoni mwa wale wanaowapa nasaha kwa kuwashauri kula kutoka mti ule, huku yeye ni mrongo katika hilo. info
التفاسير:

external-link copy
22 : 7

فَدَلَّىٰهُمَا بِغُرُورٖۚ فَلَمَّا ذَاقَا ٱلشَّجَرَةَ بَدَتۡ لَهُمَا سَوۡءَٰتُهُمَا وَطَفِقَا يَخۡصِفَانِ عَلَيۡهِمَا مِن وَرَقِ ٱلۡجَنَّةِۖ وَنَادَىٰهُمَا رَبُّهُمَآ أَلَمۡ أَنۡهَكُمَا عَن تِلۡكُمَا ٱلشَّجَرَةِ وَأَقُل لَّكُمَآ إِنَّ ٱلشَّيۡطَٰنَ لَكُمَا عَدُوّٞ مُّبِينٞ

Hapo yeye aliwatia wao ujasiri na akawadanganya wakala kutoka mti huo ambao Mwenyezi Mungu Aliwakataza wasiukaribie. Walipokula kutoka mti huo, ziliwafunuka tupu zao na kikaondoka kile ambacho Mwenyezi Mungu Aliwasitiri nacho kabla ya wao kufanya uhalifu huo, wakawa wanayaambatisha majani ya miti ya Peponi kwenye tupu zao. Hapo Mola wao, Aliyetukuka na kuwa juu, Aliwaita, «Kwani sikuwakataza kula kutoka mti ule na nikawaambia kwamba Shetani, kwenu nyinyi, ni adui ambaye uadui wake uko waziwazi?» Katika aya hii kuna ushahidi kwamba kukaa uchi ni kati ya mambo makubwa na kwamba hilo ni jambo lililokowa lachukiza na linaloendelea kuchukiza katika tabia, na ni ovu kwenye akili za watu. info
التفاسير: