ترجمة معاني القرآن الكريم - الترجمة السواحلية - علي محسن البرواني

رقم الصفحة:close

external-link copy
90 : 23

بَلۡ أَتَيۡنَٰهُم بِٱلۡحَقِّ وَإِنَّهُمۡ لَكَٰذِبُونَ

Bali tumewaletea Haki, na kwa yakini hao ni waongo. info

Hakika Sisi tumewabainishia Haki kwa ndimi za Mitume, na wao ni waongo katika kila jambo linalo khitalifu na Haki hii.

التفاسير:

external-link copy
91 : 23

مَا ٱتَّخَذَ ٱللَّهُ مِن وَلَدٖ وَمَا كَانَ مَعَهُۥ مِنۡ إِلَٰهٍۚ إِذٗا لَّذَهَبَ كُلُّ إِلَٰهِۭ بِمَا خَلَقَ وَلَعَلَا بَعۡضُهُمۡ عَلَىٰ بَعۡضٖۚ سُبۡحَٰنَ ٱللَّهِ عَمَّا يَصِفُونَ

Mwenyezi Mungu hana mwana yeyote, wala hanaye mungu mwengine. Inge kuwa hivyo basi kila mungu angeli chukua alivyo umba, na baadhi yao wangeli washinda wengine. Mwenyezi Mungu ameepukana na sifa wanazo msifu. info

Mwenyezi Mungu hakumchukua yeyote kuwa ni mwanawe. Yeye ametakasikia na hayo. Wala hana mshirika. Angeli kuwa na mshirika basi kila mmoja wao angejipa madaraka ya pekee kwa alivyo viumba, na vikawa ndio milki yake, na wangeli gombana wenyewe kwa wenyewe kama wanavyo onekana wafalme wanavyo fanya. Na ulimwengu ungeli fisidika kwa mizozano hiyo. Basi Mwenyezi Mungu ametakasika na hayo wayasemayo washirikina yanayo kwenda kinyume na Haki.

التفاسير:

external-link copy
92 : 23

عَٰلِمِ ٱلۡغَيۡبِ وَٱلشَّهَٰدَةِ فَتَعَٰلَىٰ عَمَّا يُشۡرِكُونَ

Mjuzi wa siri na dhaahiri, na ametukuka juu ya hayo wanayo mshirikisha nayo. info

Na Yeye amevizunguka vitu vyote kwa kuvijua. Anajua tusiyo yaona na tunayo yaona. Mwenyezi Mungu ametakasika na hayo wanayo mnasibisha nayo makafiri kuwa ati ana washirika.

التفاسير:

external-link copy
93 : 23

قُل رَّبِّ إِمَّا تُرِيَنِّي مَا يُوعَدُونَ

Sema: Mola wangu Mlezi! Ukinionyesha adhabu waliyo ahidiwa, info

Ewe Nabii! Sema: Ukiwateremshia adhabu ulio waahidi hapa duniani nami nipo pamoja nao,

التفاسير:

external-link copy
94 : 23

رَبِّ فَلَا تَجۡعَلۡنِي فِي ٱلۡقَوۡمِ ٱلظَّٰلِمِينَ

Mola wangu Mlezi! Usinijaalie katika watu madhaalimu hao. info

Basi nakuomba usinifanye mwenye kuadhibiwa pamoja na makafiri waasi.

التفاسير:

external-link copy
95 : 23

وَإِنَّا عَلَىٰٓ أَن نُّرِيَكَ مَا نَعِدُهُمۡ لَقَٰدِرُونَ

Na hakika Sisi ni waweza wa kukuonyeshsa tuliyo waahidi. info

Na Sisi tunaweza kwa utimilivu kukuonyesha adhabu tulio waahidi ikiwateremkia. Basi wewe tuwa ujue kuwa tutashinda.

التفاسير:

external-link copy
96 : 23

ٱدۡفَعۡ بِٱلَّتِي هِيَ أَحۡسَنُ ٱلسَّيِّئَةَۚ نَحۡنُ أَعۡلَمُ بِمَا يَصِفُونَ

Kinga maovu kwa kutenda yaliyo mema zaidi. Sisi tunajua wayasemayo. info

Wewe endelea na wito wako, na ukabili uovu wao kwa vitendo vilivyo vizuri kama kusamehe au vyenginevyo. Na Sisi tunajua vyema wanakutaja vipi wewe, na wanavyo usema kwa ubaya huo wito wako kwa uwovu na uzushi. Na Sisi tutawalipa kwa hayo.

التفاسير:

external-link copy
97 : 23

وَقُل رَّبِّ أَعُوذُ بِكَ مِنۡ هَمَزَٰتِ ٱلشَّيَٰطِينِ

Na sema: Mola wangu Mlezi! Najikinga kwako na wasiwasi wa mashet'ani. info

Nawe sema: Ewe Mola Mlezi! Najilinda kwako na wasiwasi wa mashetani wasiniingilie katika nafsi yangu kwa vitendo visio kupendeza.

التفاسير:

external-link copy
98 : 23

وَأَعُوذُ بِكَ رَبِّ أَن يَحۡضُرُونِ

Na najikinga kwako, Mola wangu Mlezi, wasinikaribie. info

Na ewe Mola Mlezi! Najilinda kwako wasiwe nami katika kitendo chochote ili kitendo hicho kiwe kimetakasika, safi, kwa ajili ya ridhaa yako tukufu.

التفاسير:

external-link copy
99 : 23

حَتَّىٰٓ إِذَا جَآءَ أَحَدَهُمُ ٱلۡمَوۡتُ قَالَ رَبِّ ٱرۡجِعُونِ

Mpaka yanapo mfikia mmoja wao mauti, husema: Mola wangu Mlezi! Nirudishe. info

Wanaendelea kuwakanusha mpaka utapo fika wakati wa kufa mmoja wao hujuta na akasema: Ewe Mola wangu Mlezi! Nirudishe duniani.

التفاسير:

external-link copy
100 : 23

لَعَلِّيٓ أَعۡمَلُ صَٰلِحٗا فِيمَا تَرَكۡتُۚ كَلَّآۚ إِنَّهَا كَلِمَةٌ هُوَ قَآئِلُهَاۖ وَمِن وَرَآئِهِم بَرۡزَخٌ إِلَىٰ يَوۡمِ يُبۡعَثُونَ

Ili nitende mema sasa badala ya yale niliyo yaacha. Wapi! Hii ni kauli aisemayo yeye tu. Na nyuma yao kipo kizuizi mpaka siku watapo fufuliwa. info

Ili nipate kufanya a'mali njema katika mali au wakati nilio acha. Wala ombi lake halitokubaliwa. Kwani haya ni maneno anayasema bila ya faida, hayakubaliwi. Na pindi akikubaliwa hatotenda kitu. Na juu ya yote hatorudi kabisa! Kwani mauti ni kizuizi baina yao na hayo wanayo yatamani mpaka Mwenyezi Mungu atapo wafufua.

التفاسير:

external-link copy
101 : 23

فَإِذَا نُفِخَ فِي ٱلصُّورِ فَلَآ أَنسَابَ بَيۡنَهُمۡ يَوۡمَئِذٖ وَلَا يَتَسَآءَلُونَ

Basi litapo pulizwa baragumu hapo hautakuwapo ujamaa baina yao siku hiyo, wala hawataulizana. info

Ukifika wakati wa kufufuliwa tutawafufua kutoka makaburini kwao. Na hayo ni kwa mfano wa kupulizwa tarumbeta watafufuka nao wamefarikiana. Hapana mtu utaomfaa ujamaa wake na fulani. (Ujamaa Kiswahili maana yake makhusiano ya nasaba, sio usoshalisti.) Wala hapana mtu atae muomba mtu kitu cha kumfaa. Kwani kila mmoja wao siku hiyo atakuwa kashughulika na lake.

التفاسير:

external-link copy
102 : 23

فَمَن ثَقُلَتۡ مَوَٰزِينُهُۥ فَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡمُفۡلِحُونَ

Ama wale ambao mizani zao zitakuwa nzito, hao ndio wenye kufanikiwa. info

A'mali (Vitendo) ndio mizani ya kupimia. Mwenye Imani nzuri na vitendo vyema atakuwa na uzito katika mizani ya Mwenyezi Mungu. Hao ndio walio fuzu.

التفاسير:

external-link copy
103 : 23

وَمَنۡ خَفَّتۡ مَوَٰزِينُهُۥ فَأُوْلَٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ خَسِرُوٓاْ أَنفُسَهُمۡ فِي جَهَنَّمَ خَٰلِدُونَ

Na wale ambao mizani zao zitakuwa nyepesi, hao ndio walio zitia khasarani nafsi zao, na katika Jahannamu watadumu. info

Na asiye kuwa na thawabu au vitendo vyenye uzito mbele ya Mwenyezi Mungu, hao ndio walio zikhasiri nafsi zao kwa kuziuza kwa Shetani. Nao wataadhibiwa Motoni, wadumu humo.

التفاسير:

external-link copy
104 : 23

تَلۡفَحُ وُجُوهَهُمُ ٱلنَّارُ وَهُمۡ فِيهَا كَٰلِحُونَ

Moto utababua nyuso zao, nao watakuwa na nyuso zilizo kunjana. info

Moto utawababua nyuso zao, nazo zitakuwa zimekunjana kwa uwovu wa mwisho wao.

التفاسير: