Bản dịch ý nghĩa nội dung Qur'an - 斯瓦西里语翻译 - 阿里·穆哈辛·拜拉瓦尼

Al-Muzzammil

external-link copy
1 : 73

يَٰٓأَيُّهَا ٱلۡمُزَّمِّلُ

Ewe uliye jifunika! info

Ewe uliye jigubika kwa nguo zako!

التفاسير:

external-link copy
2 : 73

قُمِ ٱلَّيۡلَ إِلَّا قَلِيلٗا

Kesha usiku kucha, ila kidogo tu! info

Inuka kwa ajili ya Swala usiku kucha, ila kidogo tu!

التفاسير:

external-link copy
3 : 73

نِّصۡفَهُۥٓ أَوِ ٱنقُصۡ مِنۡهُ قَلِيلًا

Nusu yake, au ipunguze kidogo. info

Simama nusu ya usiku, au punguza kidogo katika hiyo nusu mpaka ifikie thuluthi,

التفاسير:

external-link copy
4 : 73

أَوۡ زِدۡ عَلَيۡهِ وَرَتِّلِ ٱلۡقُرۡءَانَ تَرۡتِيلًا

Au izidishe - na soma Qur'ani kwa utaratibu na utungo. info

Au zidisha kwenye nusu mpaka ifikie thuluthi mbili. Na soma Qur'ani kwa pole pole ukibainisha harufi, na pa kusita usite, pasiwe na nuksani yoyote.

التفاسير:

external-link copy
5 : 73

إِنَّا سَنُلۡقِي عَلَيۡكَ قَوۡلٗا ثَقِيلًا

ka Hakika Sisi tutakuteremshia uli nzito. info

Ewe Mtume! Hakika Sisi tutakuteremshia Qur'ani yenye kukusanya amri, na makatazo, na takalifu nzito nzito.

التفاسير:

external-link copy
6 : 73

إِنَّ نَاشِئَةَ ٱلَّيۡلِ هِيَ أَشَدُّ وَطۡـٔٗا وَأَقۡوَمُ قِيلًا

Hakika kuamka usiku kunawafikiana zaidi na moyo, na maneno yake yanatua zaidi. info

Hakika ibada zinazo fanywa usiku zinaganda zaidi katika moyo wa mtu, na zinabainika zaidi ulimini, na zinasibu vyema zaidi, kuliko visomo vya ibada za mchana.

التفاسير:

external-link copy
7 : 73

إِنَّ لَكَ فِي ٱلنَّهَارِ سَبۡحٗا طَوِيلٗا

Kwani hakika mchana una shughuli nyingi. info

Hakika mchana unakuwa na mambo mengi ya kukuhangaisha kutafuta maslaha ya maisha yako, na kushughulika na mambo ya kufikisha Ujumbe. Basi jiwekee nafsi yako faragha ya usiku kwa ajili ya kumuabudu Mola wako Mlezi.

التفاسير:

external-link copy
8 : 73

وَٱذۡكُرِ ٱسۡمَ رَبِّكَ وَتَبَتَّلۡ إِلَيۡهِ تَبۡتِيلٗا

Na lidhukuru jina la Mola wako Mlezi, na ujitolee kwake kwa ukamilifu. info

Na pitisha ulimini mwako kudhukuru jina la Mola aliye kuumba na kukulea, na mkhusishe Yeye tu kwa ibada kwa ukamilifu.

التفاسير:

external-link copy
9 : 73

رَّبُّ ٱلۡمَشۡرِقِ وَٱلۡمَغۡرِبِ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ فَٱتَّخِذۡهُ وَكِيلٗا

Mola Mlezi wa mashariki na magharibi, hapana mungu isipo kuwa Yeye, basi mfanye kuwa Mtegemewa wako. info

Yeye ndiye Mwenye kumiliki mashariki na magharibi, hapana wa kuabudiwa kwa haki isipo kuwa Yeye. Basi mfanye Yeye tu ndiye wa kukutosha katika mambo yako yote, ndiye wa kutegemewa peke yake kama alivyo ahidi.

التفاسير:

external-link copy
10 : 73

وَٱصۡبِرۡ عَلَىٰ مَا يَقُولُونَ وَٱهۡجُرۡهُمۡ هَجۡرٗا جَمِيلٗا

Na vumilia hayo wayasemayo, na jitenge nao kwa vizuri. info

Na vumilia upuuzi wanao usema, na jitenge nao kwa moyo wako, na nenda kinyume na vitendo vyao, pamoja na kuwapuuza, na kuacha kujilipizia.

التفاسير:

external-link copy
11 : 73

وَذَرۡنِي وَٱلۡمُكَذِّبِينَ أُوْلِي ٱلنَّعۡمَةِ وَمَهِّلۡهُمۡ قَلِيلًا

Na niache Mimi na hao wanao kanusha, walio neemeka; na wape muhula kidogo! info

Niachilie Mimi hao wanao kadhibisha, wenye kuneemeshwa, na uwape muhula muda mfupi.

التفاسير:

external-link copy
12 : 73

إِنَّ لَدَيۡنَآ أَنكَالٗا وَجَحِيمٗا

Hakika Sisi tunazo pingu nzito na Moto unao waka kwa ukali kabisa! info

Huko Akhera tumewawekea wanao kadhibisha pingu nzito, na Moto wa kuunguza,

التفاسير:

external-link copy
13 : 73

وَطَعَامٗا ذَا غُصَّةٖ وَعَذَابًا أَلِيمٗا

Na chakula kinacho kwama kooni, na adhabu inayo umiza. info

Na chakula kinacho sakama kooni, hakimezeki, na adhabu yenye uchungu mkali usio stahamilika.

التفاسير:

external-link copy
14 : 73

يَوۡمَ تَرۡجُفُ ٱلۡأَرۡضُ وَٱلۡجِبَالُ وَكَانَتِ ٱلۡجِبَالُ كَثِيبٗا مَّهِيلًا

Siku ambayo ardhi itatikiswa na milima pia, na milima itakuwa kama tifutifu la mchanga. info

Siku itakapo tikisika ardhi na milima kwa mtikiso mkubwa mno, na milima ikawa mirundu ya mchanga ulio tapanyika, baada ya kuwa mawe magumu yaliyo shikamana.

التفاسير:

external-link copy
15 : 73

إِنَّآ أَرۡسَلۡنَآ إِلَيۡكُمۡ رَسُولٗا شَٰهِدًا عَلَيۡكُمۡ كَمَآ أَرۡسَلۡنَآ إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ رَسُولٗا

Hakika Sisi tumemtuma kwenu Mtume aliye shahidi juu yenu, kama tulivyo mtuma Mtume kwa Firauni. info

Enyi watu wa Makka! Hakika Sisi tumekutumieni Muhammad kuwa ni Mtume wa kukushuhudilieni Siku ya Kiyama kwa kukubali na kukataa, kama tulivyo mtuma Musa kwa Firauni awe ni Mtume.

التفاسير:

external-link copy
16 : 73

فَعَصَىٰ فِرۡعَوۡنُ ٱلرَّسُولَ فَأَخَذۡنَٰهُ أَخۡذٗا وَبِيلٗا

Lakini Firauni alimuasi huyo Mtume, basi tukamshika mshiko wa mateso. info

Firauni akamkataa huyo Mtume, basi tukamshika kwa mshiko wa nguvu!

التفاسير:

external-link copy
17 : 73

فَكَيۡفَ تَتَّقُونَ إِن كَفَرۡتُمۡ يَوۡمٗا يَجۡعَلُ ٱلۡوِلۡدَٰنَ شِيبًا

Basi nyinyi mkikufuru, mtawezaje kujikinga na Siku ambayo itawafanya watoto wadogo waote mvi? info

Basi mkikufuru mtajikinga vipi na adhabu ya Siku ambayo kwa kitisho chake itawafanya vijana wawe vikongwe wasio na nguvu?

التفاسير:

external-link copy
18 : 73

ٱلسَّمَآءُ مُنفَطِرُۢ بِهِۦۚ كَانَ وَعۡدُهُۥ مَفۡعُولًا

Hapo mbingu zitapasuka! Ahadi yake itakuwa imetekelezwa. info

Mbingu juu ya nguvu zake na ukubwa wake, Siku hiyo zitapasukilia mbali kwa shida zake na vitisho vyake. Na ahadi ya Mwenyezi Mungu ni lazima itokee, hapana hivi wala hivi.

التفاسير:

external-link copy
19 : 73

إِنَّ هَٰذِهِۦ تَذۡكِرَةٞۖ فَمَن شَآءَ ٱتَّخَذَ إِلَىٰ رَبِّهِۦ سَبِيلًا

Kwa hakika hili ni kumbusho. Mwenye kutaka atashika njia ya kwendea kwa Mola wake Mlezi. info

Hakika Aya hizi zinazo taja ahadi ya Mwenyezi Mungu ni mawaidha. Kwa hivyo mwenye kutaka kunafiika kwazo ataishika njia ya kumwendea Mola wake Mlezi kwa kuchamngu na kunyenyekea.

التفاسير:

external-link copy
20 : 73

۞ إِنَّ رَبَّكَ يَعۡلَمُ أَنَّكَ تَقُومُ أَدۡنَىٰ مِن ثُلُثَيِ ٱلَّيۡلِ وَنِصۡفَهُۥ وَثُلُثَهُۥ وَطَآئِفَةٞ مِّنَ ٱلَّذِينَ مَعَكَۚ وَٱللَّهُ يُقَدِّرُ ٱلَّيۡلَ وَٱلنَّهَارَۚ عَلِمَ أَن لَّن تُحۡصُوهُ فَتَابَ عَلَيۡكُمۡۖ فَٱقۡرَءُواْ مَا تَيَسَّرَ مِنَ ٱلۡقُرۡءَانِۚ عَلِمَ أَن سَيَكُونُ مِنكُم مَّرۡضَىٰ وَءَاخَرُونَ يَضۡرِبُونَ فِي ٱلۡأَرۡضِ يَبۡتَغُونَ مِن فَضۡلِ ٱللَّهِ وَءَاخَرُونَ يُقَٰتِلُونَ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِۖ فَٱقۡرَءُواْ مَا تَيَسَّرَ مِنۡهُۚ وَأَقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتُواْ ٱلزَّكَوٰةَ وَأَقۡرِضُواْ ٱللَّهَ قَرۡضًا حَسَنٗاۚ وَمَا تُقَدِّمُواْ لِأَنفُسِكُم مِّنۡ خَيۡرٖ تَجِدُوهُ عِندَ ٱللَّهِ هُوَ خَيۡرٗا وَأَعۡظَمَ أَجۡرٗاۚ وَٱسۡتَغۡفِرُواْ ٱللَّهَۖ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمُۢ

Hakika Mola wako Mlezi anajua ya kuwa hakika wewe unakesha karibu na thuluthi mbili za usiku, na nusu yake, na thuluthi yake. Na baadhi ya watu walio pamoja nawe kadhaalika. Na Mwenyezi Mungu ndiye anaye ukadiria usiku na mchana. Anajua kuwa hamwezi kuweka hisabu, basi amekusameheni. Basi someni kilicho chepesi katika Qur'ani. Anajua ya kuwa baadhi yenu watakuwa wagonjwa, na wengine wanasafiri katika ardhi wakitafuta fadhila ya Mwenyezi Mungu, na wengine wanapigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo someni kilicho chepesi humo, na mshike Swala, na toeni Zaka, na mkopesheni Mwenyezi Mungu mkopo mwema. Na kheri yoyote mnayo itanguliza kwa ajili ya nafsi zenu mtaikuta kwa Mwenyezi Mungu, imekuwa bora zaidi, na ina thawabu kubwa sana. Na mtakeni msamaha Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu. info

Hakika Mola wako Mlezi anajua kwamba wewe, Muhammad, unakesha pengine akali kuliko thuluthi mbili za usiku, na mara nyengine unakesha nusu ya usiku, na pia wanakesha baadhi ya masahaba zako kama ukeshavyo wewe. Na hapana anaye weza kuukadiria urefu wa usiku na mchana, na kudhibiti saa zake, ila Mwenyezi Mungu. Yeye anajua kuwa hamwezi kuhisabu baraabara kila sehemu katika sehemu za usiku na mchana. Kwa hivyo amekukhafifishieni. Basi someni katika Swala kilicho chepesi katika Qur'ani. Yeye anajua kuwa watakuwepo kati yenu walio wagonjwa, ambao watapata taabu kukesha usiku; na wengine wamo safarini kwa ajili ya biashara na kazi, wakitafuta riziki ya Mwenyezi Mungu. Na wengine wanapigana Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kulitukuza Neno lake. Basi someni kilicho chepesi katika Qur'ani, na zishikeni baraabara faridha za Swala, na toeni Zaka iliyo kuwajibikieni, na mkopesheni Mwenyezi Mungu mkopo mwema, kwa kuwapa mafakiri kwa khiari juu ya hayo yaliyo kulazimuni. Na chochote cha kheri mnacho kitanguliza kwa ajili ya nafsi zenu, mtakuta thawabu zake kwa Mwenyezi Mungu zimekuwa bora zaidi kuliko hicho mlicho kiacha na kukitoa, na malipo mema zaidi. Na mtakeni msamaha Mwenyezi Mungu kwa vitendo viovu na kwa upungufu katika vitendo vyema. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe madhambi ya Waumini, na ni Mwenye kuwarehemu.

التفاسير: