Wakipokea thawabu na takrima wanazo pewa na Mola wao Mlezi. Hakika hao kabla ya hapo walikuwa duniani ni wenye kufanya mambo mazuri kwa kutimiza waliyo takiwa wayafanye.
Basi naapa kwa Mola Mlezi wa mbingu na ardhi kwamba hakika yote hayo mnayo yakanya kuwa, yaani kufufuliwa, kulipwa, kuadhibiwa wanao kadhibisha, na kuwalipa thawabu wachamngu, yote hayo bila ya shaka ni ya kweli thaabiti kama hivyo kusema kwenu ambako hamna shaka nako kuwa mnasema.
Unakijua kisa cha Malaika, wageni wa hishima wa Ibrahim? Pale walipo ingia kwake na wakamtolea Salamu, na yeye akawajibu kwa Salamu, na kuwambia kuwa ni watu asio wajua.
Pale walipo ingia kwake na wakamtolea Salamu, na yeye akawajibu kwa Salamu, na kuwambia kuwa ni watu asio wajua.
Akahisi katika nafsi yake khofu kuwaogopa. Wakasema: Usiogope. Na wakampa bishara kuwa atapata mwana mwenye ilimu nzuri.
Akatokea mkewe akipiga kelele alipo isikia ile bishara, akijipiga uso wake kwa mkono wake, kwa kuona muhali hayo na kustaajabu, na akasema: Mimi ni kizee, na tasa. Itakuwaje nizae?
Wakasema: Hivyo ndivyo alivyo kwisha hukumu Mola wako Mlezi. Hakika Yeye ni Mwenye hikima katika kila anayo hukumu, ni Mwenye ujuzi ambaye hapana linalo fichikana kwake lolote.
Tukamchukua yeye na hao anao jitapia kwao, tukawatumbukiza baharini, naye ni mwenye kuyatenda hayo ya ukafiri na inda anayo laumiwa kwayo.
Na katika kisa cha Thamudi ipo Ishara. Walipo ambiwa: Stareheni katika majumba yenu kwa muda maalumu. Wakajivuna na wakatakabari wasifuate amri ya Mola wao Mlezi. Basi radi ikawaangamiza nao wanaiona kwa macho yao inavyo tokea.
Na ardhi tumeikunjua, na Sisi ni wenye kuitengeneza vizuri kama kitanda. Aya hii tukufu inaashiria maana za kitaalamu nyingi; miongoni mwazo ni kwamba Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taa'la ameumba ulimwengu huu mkunjufu kwa nguvu. Na Yeye ni Muweza kwa atakayo. Na maana ya mbingu katika Aya hii ni kila kilicho juu ya kitu na kikakifunika. Basi kila kilicho zunguka sayari na nyota na mkusanyiko wa jua katika sehemu hii inayo onekana ya ulimwengu kimetanda kupita inavyo kadirika na akili, wala haiwezi kupimika. Kwani masafa yao hukisiwa kwa mamilioni ya miaka ya mwangaza. Na mwaka mmoja wa mwangaza kwa ilivyo thibiti kwa ilimu za kisasa katika karne hii ya ishirini ni masafa yanayo kwenda mwangaza kwa mbio za kilomita 300,000 kwa nukta moja ya dakika. Na ibara ya Aya tukufu (Na hakika Sisi ndio twenye kuutanua) inaashiria hayo, yaani kutanda huko kwa ulimwengu kunako staajabisha tangu kuumbwa kwake. Kama vile vile kuwa kukunjuka huko kungali kunaendelea, na hayo sayansi ya sasa imethibitisha vile vile. Na imejuulikana kwa nadhariya ya kutanda ambayo katika mwanzo mwanzo wa karne hii imethibiti kuwa ni kweli kiilimu, na ufupi wake ni kuwa ulimwengu unaendelea kukua na kupanuka, na kila sayari za mbinguni zinajitenga wenyewe kwa wenyewe.
Wala msimfanye mungu mwengine kuwa pamoja na Mwenyezi Mungu. Hakika mimi nimekujieni kwa amri ya Mwenyezi Mungu kukuonyeni kwa uwazi matokeo ya ushirikina.
Hivyo ndivyo ilivyo kuwa hali ya mataifa yote kwa Mitume wao. Hakuja Mtume kwa watu wa kabla ya kaumu yako ila walimwita: Mchawi au mwendawazimu.
Sitaki kwao riziki, kwani Mimi si mhitaji kwa walimwengu wote; wala sitaki wanilishe, kwani Mimi ndiye ninaye lisha, wala silishwi.
Hakika hao walio jidhulumu nafsi zao kwa ukafiri na kukanusha wana fungu lao la adhabu mfano wa fungu la wenzao katika kaumu zilizo kwisha pita. Basi wasifanye haraka kuhimiza adhabu ishuke kabla ya wakati wake.