Fassarar Ma'anonin Alqura'ni - Fassarar Sawahil - Ali Muhsin al-Barwani

Adh-Dhariyat

external-link copy
1 : 51

وَٱلذَّٰرِيَٰتِ ذَرۡوٗا

Naapa kwa pepo zinazo tawanya! info

Ninaapa kwa pepo zinazo timua mawingu, zikayasukuma kwa nguvu, huku zikibeba mizigo mizito ya maji, zikawa zinakwenda kwa wepesi kwa amri ya Mwenyezi Mungu, zikawa zinagawanya riziki kwa ampendaye Mwenyezi Mungu.

التفاسير:

external-link copy
2 : 51

فَٱلۡحَٰمِلَٰتِ وِقۡرٗا

Na zinazo beba mizigo! info

Huku zikibeba mizigo mizito ya maji.

التفاسير:

external-link copy
3 : 51

فَٱلۡجَٰرِيَٰتِ يُسۡرٗا

Na zinazo kwenda kwa wepesi. info

Zikawa zinakwenda kwa wepesi kwa amri ya Mwenyezi Mungu.

التفاسير:

external-link copy
4 : 51

فَٱلۡمُقَسِّمَٰتِ أَمۡرًا

Na zinazo gawanya kwa amri! info

Zikawa zinagawanya riziki kwa ampendaye Mwenyezi Mungu.

التفاسير:

external-link copy
5 : 51

إِنَّمَا تُوعَدُونَ لَصَادِقٞ

Hakika mnayo ahidiwa bila ya shaka ni kweli! info

Hakika hayo mnayo ahidiwa, nayo ya kufufuliwa na mengineyo, ni hakika ya kweli itakayo tokea.

التفاسير:

external-link copy
6 : 51

وَإِنَّ ٱلدِّينَ لَوَٰقِعٞ

Na kwa hakika malipo bila ya shaka yatatokea. info

Na kwamba kwa yakini malipo kwa vitendo vyenu yatakuwa tu hapana hivi wala hivi.

التفاسير:

external-link copy
7 : 51

وَٱلسَّمَآءِ ذَاتِ ٱلۡحُبُكِ

Naapa kwa mbingu zenye njia! info

Ninaapa kwa mbingu zenye njia zilizo wekwa baraabara.

التفاسير:

external-link copy
8 : 51

إِنَّكُمۡ لَفِي قَوۡلٖ مُّخۡتَلِفٖ

Hakika nyinyi bila ya shaka mmo katika kauli inayo khitalifiana. info

Kwamba nyinyi msemapo mnayo yasema ni maneno ya kugongana.

التفاسير:

external-link copy
9 : 51

يُؤۡفَكُ عَنۡهُ مَنۡ أُفِكَ

Anageuzwa kutokana na haki mwenye kugeuzwa. info

Huacha kuamini hiyo ahadi ya kweli na malipo yatakayo kuwa huyo anaye acha, kwa sababu amekhiari kufuata pumbao la nafsi yake kuliko akili yake.

التفاسير:

external-link copy
10 : 51

قُتِلَ ٱلۡخَرَّٰصُونَ

Wazushi wameangamizwa. info

Wameteketea waongo wanao sema katika khabari za Kiyama kuwa ni mambo ya dhana na kukisia tu, ambao kwamba wamezamishwa katika ujinga, wameghafilika na dalili za yakini.

التفاسير:

external-link copy
11 : 51

ٱلَّذِينَ هُمۡ فِي غَمۡرَةٖ سَاهُونَ

Ambao wameghafilika katika ujinga. info

Ambao kwamba wamezamishwa katika ujinga, wameghafilika na dalili za yakini.

التفاسير:

external-link copy
12 : 51

يَسۡـَٔلُونَ أَيَّانَ يَوۡمُ ٱلدِّينِ

Wanauliza: Ni lini hiyo siku ya malipo? info

Wanauliza kwa kejeli, kwa kuwa wanaona hayawi hayo: Lini itakuwa hiyo siku ya malipo?

التفاسير:

external-link copy
13 : 51

يَوۡمَ هُمۡ عَلَى ٱلنَّارِ يُفۡتَنُونَ

Hiyo ni siku watakayo adhibiwa Motoni. info

Siku watapo simamishwa Motoni wakichomwa!

التفاسير:

external-link copy
14 : 51

ذُوقُواْ فِتۡنَتَكُمۡ هَٰذَا ٱلَّذِي كُنتُم بِهِۦ تَسۡتَعۡجِلُونَ

Onjeni adhabu yenu! Haya ndiyo mliyo kuwa mkiyahimiza. info

Wataambiwa: Onjeni adhabu yenu hii ambayo duniani mlikuwa mkiihimiza iwe.

التفاسير:

external-link copy
15 : 51

إِنَّ ٱلۡمُتَّقِينَ فِي جَنَّٰتٖ وَعُيُونٍ

Hakika wachamngu watakuwa katika Mabustani na chemchem. info

Hakika walio mt'ii Mwenyezi Mungu na wakamkhofu watakuwa wananeemeka katika Mabustani na chemchem za Peponi ambazo haziwezi kusifika hakika yake.

التفاسير:

external-link copy
16 : 51

ءَاخِذِينَ مَآ ءَاتَىٰهُمۡ رَبُّهُمۡۚ إِنَّهُمۡ كَانُواْ قَبۡلَ ذَٰلِكَ مُحۡسِنِينَ

Wanapokea aliyo wapa Mola wao Mlezi. Kwa hakika hao walikuwa kabla ya haya wakifanya mema. info

Wakipokea thawabu na takrima wanazo pewa na Mola wao Mlezi. Hakika hao kabla ya hapo walikuwa duniani ni wenye kufanya mambo mazuri kwa kutimiza waliyo takiwa wayafanye.

التفاسير:

external-link copy
17 : 51

كَانُواْ قَلِيلٗا مِّنَ ٱلَّيۡلِ مَا يَهۡجَعُونَ

Walikuwa wakilala kidogo tu usiku. info

Walikuwa kulala kwao usiku ni kuchache, na wakikesha sana kwa ibada.

التفاسير:

external-link copy
18 : 51

وَبِٱلۡأَسۡحَارِ هُمۡ يَسۡتَغۡفِرُونَ

Na kabla ya alfajiri wakiomba maghfira. info

Na mwishoni mwa usiku walikuwa wakiomba maghfira.

التفاسير:

external-link copy
19 : 51

وَفِيٓ أَمۡوَٰلِهِمۡ حَقّٞ لِّلسَّآئِلِ وَٱلۡمَحۡرُومِ

Na katika mali yao ipo haki ya mwenye kuomba na asiye omba. info

Na katika mali yao wakiweka fungu maalumu lilio thibiti kwa ajili ya wenye haja, wanao omba na wanao jizuilia kuomba kwa kujiteta.

التفاسير:

external-link copy
20 : 51

وَفِي ٱلۡأَرۡضِ ءَايَٰتٞ لِّلۡمُوقِنِينَ

Na katika ardhi zipo Ishara kwa wenye yakini. info

Na katika ardhi zipo dalili nyingi zilizo wazi zinazo pelekea yakini, kwa mwenye kuitafuta njia.

التفاسير:

external-link copy
21 : 51

وَفِيٓ أَنفُسِكُمۡۚ أَفَلَا تُبۡصِرُونَ

Na pia katika nafsi zenu - Je! Hamwoni? info

Na hali kadhaalika katika nafsi zenu zipo Ishara zilizo wazi. Je! Mmeghafilika nazo, hamzioni?

التفاسير:

external-link copy
22 : 51

وَفِي ٱلسَّمَآءِ رِزۡقُكُمۡ وَمَا تُوعَدُونَ

Na katika mbingu ziko riziki zenu na mliyo ahidiwa. info

Na katika mbingu ipo amri ya riziki zenu na kukadiriwa mnayo ahidiwa.

التفاسير:

external-link copy
23 : 51

فَوَرَبِّ ٱلسَّمَآءِ وَٱلۡأَرۡضِ إِنَّهُۥ لَحَقّٞ مِّثۡلَ مَآ أَنَّكُمۡ تَنطِقُونَ

Basi naapa kwa Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, hakika haya ni kweli kama ilivyo kweli kuwa nyinyi mnasema. info

Basi naapa kwa Mola Mlezi wa mbingu na ardhi kwamba hakika yote hayo mnayo yakanya kuwa, yaani kufufuliwa, kulipwa, kuadhibiwa wanao kadhibisha, na kuwalipa thawabu wachamngu, yote hayo bila ya shaka ni ya kweli thaabiti kama hivyo kusema kwenu ambako hamna shaka nako kuwa mnasema.

التفاسير:

external-link copy
24 : 51

هَلۡ أَتَىٰكَ حَدِيثُ ضَيۡفِ إِبۡرَٰهِيمَ ٱلۡمُكۡرَمِينَ

Je! Imekufikia hadithi ya wageni wa Ibrahim wanao hishimiwa? info

Unakijua kisa cha Malaika, wageni wa hishima wa Ibrahim? Pale walipo ingia kwake na wakamtolea Salamu, na yeye akawajibu kwa Salamu, na kuwambia kuwa ni watu asio wajua.

التفاسير:

external-link copy
25 : 51

إِذۡ دَخَلُواْ عَلَيۡهِ فَقَالُواْ سَلَٰمٗاۖ قَالَ سَلَٰمٞ قَوۡمٞ مُّنكَرُونَ

Walipo ingia kwake wakasema: Salama! Na yeye akasema: Salama! Nyinyi ni watu nisio kujueni. info

Pale walipo ingia kwake na wakamtolea Salamu, na yeye akawajibu kwa Salamu, na kuwambia kuwa ni watu asio wajua.

التفاسير:

external-link copy
26 : 51

فَرَاغَ إِلَىٰٓ أَهۡلِهِۦ فَجَآءَ بِعِجۡلٖ سَمِينٖ

Akenda kwa ahali yake na akaja na ndama aliye nona. info

Akenda kwa mkewe naye ana khofu, akaja na ndama aliye nona.

التفاسير:

external-link copy
27 : 51

فَقَرَّبَهُۥٓ إِلَيۡهِمۡ قَالَ أَلَا تَأۡكُلُونَ

Akawakaribisha, akasema: Mbona hamli? info

Akawakaribisha, nao hawakula. Akasema kwa kuto wajua hakika yao: Mbona hamli?

التفاسير:

external-link copy
28 : 51

فَأَوۡجَسَ مِنۡهُمۡ خِيفَةٗۖ قَالُواْ لَا تَخَفۡۖ وَبَشَّرُوهُ بِغُلَٰمٍ عَلِيمٖ

Akahisi kuwaogopa katika nafsi yake. Wakasema: Usiwe na khofu, nao wakambashiria kupata kijana mwenye ilimu. info

Akahisi katika nafsi yake khofu kuwaogopa. Wakasema: Usiogope. Na wakampa bishara kuwa atapata mwana mwenye ilimu nzuri.

التفاسير:

external-link copy
29 : 51

فَأَقۡبَلَتِ ٱمۡرَأَتُهُۥ فِي صَرَّةٖ فَصَكَّتۡ وَجۡهَهَا وَقَالَتۡ عَجُوزٌ عَقِيمٞ

Ndipo mkewe akawaelekea, na huku anasema na akijipiga usoni kwa mastaajabu, na kusema: Mimi ni kikongwe na tasa! info

Akatokea mkewe akipiga kelele alipo isikia ile bishara, akijipiga uso wake kwa mkono wake, kwa kuona muhali hayo na kustaajabu, na akasema: Mimi ni kizee, na tasa. Itakuwaje nizae?

التفاسير:

external-link copy
30 : 51

قَالُواْ كَذَٰلِكِ قَالَ رَبُّكِۖ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلۡحَكِيمُ ٱلۡعَلِيمُ

Wakasema: Ndivyo vivyo hivyo alivyo sema Mola wako Mlezi. Hakika Yeye ni Mwenye hikima na Mwenye kujua. info

Wakasema: Hivyo ndivyo alivyo kwisha hukumu Mola wako Mlezi. Hakika Yeye ni Mwenye hikima katika kila anayo hukumu, ni Mwenye ujuzi ambaye hapana linalo fichikana kwake lolote.

التفاسير:

external-link copy
31 : 51

۞ قَالَ فَمَا خَطۡبُكُمۡ أَيُّهَا ٱلۡمُرۡسَلُونَ

AKASEMA: Basi ujumbe wenu ni nini, enyi mlio tumwa? info

Ibrahim akasema: Mna kazi gani tena baada ya khabari hii nzuri, enyi wajumbe?

التفاسير:

external-link copy
32 : 51

قَالُوٓاْ إِنَّآ أُرۡسِلۡنَآ إِلَىٰ قَوۡمٖ مُّجۡرِمِينَ

Wakasema: Hakika sisi tumetumwa kwa watu wakosefu, info

Wakasema: Kwa hakika sisi tumetumwa kwa kaumu iliyo pita kiasi katika uasi,

التفاسير:

external-link copy
33 : 51

لِنُرۡسِلَ عَلَيۡهِمۡ حِجَارَةٗ مِّن طِينٖ

Tuwatupie mawe ya udongo, info

Tuwatupie mawe ya udongo, ambayo hapana anaye yajua yalivyo ila Mwenyezi Mungu.

التفاسير:

external-link copy
34 : 51

مُّسَوَّمَةً عِندَ رَبِّكَ لِلۡمُسۡرِفِينَ

Yaliyo tiwa alama kutoka kwa Mola wako Mlezi kwa ajili ya wanao pindukia mipaka. info

Mawe hayo ni makhsusi na maalumu kwa Mola wako Mlezi kwa ajili ya wanao pindukia mipaka katika mambo machafu.

التفاسير:

external-link copy
35 : 51

فَأَخۡرَجۡنَا مَن كَانَ فِيهَا مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ

Kwa hivyo tutawatoa katika hao wale walio amini. info

Basi tukahukumu tuwatoea kwenye mji huo walio amini.

التفاسير:

external-link copy
36 : 51

فَمَا وَجَدۡنَا فِيهَا غَيۡرَ بَيۡتٖ مِّنَ ٱلۡمُسۡلِمِينَ

Lakini hatukupata humo ila nyumba moja tu yenye Waislamu! info

Lakini hatukukuta ila nyumba moja tu ndiyo ya Waislamu.

التفاسير:

external-link copy
37 : 51

وَتَرَكۡنَا فِيهَآ ءَايَةٗ لِّلَّذِينَ يَخَافُونَ ٱلۡعَذَابَ ٱلۡأَلِيمَ

Na tukaacha humo Ishara kwa ajili ya wanao iogopa adhabu chungu. info

Na katika mji huo tumeacha alama ya maangamizo ya watu wake, ili wapate kuzingatia wanayo ikhofu adhabu chungu.

التفاسير:

external-link copy
38 : 51

وَفِي مُوسَىٰٓ إِذۡ أَرۡسَلۡنَٰهُ إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ بِسُلۡطَٰنٖ مُّبِينٖ

Na katika khabari za Musa, tulipo mtuma kwa Firauni na hoja wazi. info

Na katika kisa cha Musa yapo mawaidha. Tulipo mtuma kwa Firauni, na tukatilia nguvu kwa kumpa ushahidi ulio wazi.

التفاسير:

external-link copy
39 : 51

فَتَوَلَّىٰ بِرُكۡنِهِۦ وَقَالَ سَٰحِرٌ أَوۡ مَجۡنُونٞ

Lakini alipuuza kwa sababu ya nguvu zake na akasema: Huyu ni mchawi au mwendawazimu! info

Firauni akapuuza kumuamini Musa kwa kutegemea ati nguvu zake. Akasema: Huyu ni mchawi au mwendawazimu!

التفاسير:

external-link copy
40 : 51

فَأَخَذۡنَٰهُ وَجُنُودَهُۥ فَنَبَذۡنَٰهُمۡ فِي ٱلۡيَمِّ وَهُوَ مُلِيمٞ

Basi tukamkamata yeye na majeshi yake na tukawatupa baharini, na yeye ndiye wa kulaumiwa. info

Tukamchukua yeye na hao anao jitapia kwao, tukawatumbukiza baharini, naye ni mwenye kuyatenda hayo ya ukafiri na inda anayo laumiwa kwayo.

التفاسير:

external-link copy
41 : 51

وَفِي عَادٍ إِذۡ أَرۡسَلۡنَا عَلَيۡهِمُ ٱلرِّيحَ ٱلۡعَقِيمَ

Na katika khabari za A'di tulipo wapelekea upepo wa kukata uzazi. info

Na katika kisa cha A'di yamo mawaidha pia. Tulipo wapelekea upepo usio kuwa na kheri yoyote.

التفاسير:

external-link copy
42 : 51

مَا تَذَرُ مِن شَيۡءٍ أَتَتۡ عَلَيۡهِ إِلَّا جَعَلَتۡهُ كَٱلرَّمِيمِ

Haukuacha chochote ulicho kifikia ila ulikifanya kama kilio nyambuka. info

Upepo huo haupiti kwa kitu chochote ila hukiacha kama fupa lilio nyambuka.

التفاسير:

external-link copy
43 : 51

وَفِي ثَمُودَ إِذۡ قِيلَ لَهُمۡ تَمَتَّعُواْ حَتَّىٰ حِينٖ

Na katika khabari za Thamudi walipo ambiwa: Jifurahisheni kwa muda mdogo tu. info

Na katika kisa cha Thamudi ipo Ishara. Walipo ambiwa: Stareheni katika majumba yenu kwa muda maalumu.

التفاسير:

external-link copy
44 : 51

فَعَتَوۡاْ عَنۡ أَمۡرِ رَبِّهِمۡ فَأَخَذَتۡهُمُ ٱلصَّٰعِقَةُ وَهُمۡ يَنظُرُونَ

Wakaasi amri ya Mola wao Mlezi. Basi uliwanyakua moto wa radi nao wanaona. info

Na katika kisa cha Thamudi ipo Ishara. Walipo ambiwa: Stareheni katika majumba yenu kwa muda maalumu. Wakajivuna na wakatakabari wasifuate amri ya Mola wao Mlezi. Basi radi ikawaangamiza nao wanaiona kwa macho yao inavyo tokea.

التفاسير:

external-link copy
45 : 51

فَمَا ٱسۡتَطَٰعُواْ مِن قِيَامٖ وَمَا كَانُواْ مُنتَصِرِينَ

Basi hawakuweza kusimama wala hawakuwa wenye kujitetea. info

Basi hawakuweza kuinuka. Wala hawakuweza kujipigania kuijikinga na adhabu.

التفاسير:

external-link copy
46 : 51

وَقَوۡمَ نُوحٖ مِّن قَبۡلُۖ إِنَّهُمۡ كَانُواْ قَوۡمٗا فَٰسِقِينَ

Na kaumu ya Nuhu hapo mbele. Hakika hao walikuwa watu wapotovu. info

Na kaumu ya Nuhu tuliihiliki kabla ya hawa. Hakika hao walikuwa watu walio toka nje ya ut'iifu wa Mwenyezi Mungu.

التفاسير:

external-link copy
47 : 51

وَٱلسَّمَآءَ بَنَيۡنَٰهَا بِأَيۡيْدٖ وَإِنَّا لَمُوسِعُونَ

Na mbingu tumezifanya kwa nguvu na uwezo na hakika Sisi bila ya shaka ndio twenye uwezo wa kuzitanua. info

Na mbingu tumeipanga kwa nguvu, na bila ya shaka Sisi ni waweza zaidi ya hayo.

التفاسير:

external-link copy
48 : 51

وَٱلۡأَرۡضَ فَرَشۡنَٰهَا فَنِعۡمَ ٱلۡمَٰهِدُونَ

Na ardhi tumeitandaza; basi watandazaji wazuri namna gani Sisi! info

Na ardhi tumeikunjua, na Sisi ni wenye kuitengeneza vizuri kama kitanda. Aya hii tukufu inaashiria maana za kitaalamu nyingi; miongoni mwazo ni kwamba Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taa'la ameumba ulimwengu huu mkunjufu kwa nguvu. Na Yeye ni Muweza kwa atakayo. Na maana ya mbingu katika Aya hii ni kila kilicho juu ya kitu na kikakifunika. Basi kila kilicho zunguka sayari na nyota na mkusanyiko wa jua katika sehemu hii inayo onekana ya ulimwengu kimetanda kupita inavyo kadirika na akili, wala haiwezi kupimika. Kwani masafa yao hukisiwa kwa mamilioni ya miaka ya mwangaza. Na mwaka mmoja wa mwangaza kwa ilivyo thibiti kwa ilimu za kisasa katika karne hii ya ishirini ni masafa yanayo kwenda mwangaza kwa mbio za kilomita 300,000 kwa nukta moja ya dakika. Na ibara ya Aya tukufu (Na hakika Sisi ndio twenye kuutanua) inaashiria hayo, yaani kutanda huko kwa ulimwengu kunako staajabisha tangu kuumbwa kwake. Kama vile vile kuwa kukunjuka huko kungali kunaendelea, na hayo sayansi ya sasa imethibitisha vile vile. Na imejuulikana kwa nadhariya ya kutanda ambayo katika mwanzo mwanzo wa karne hii imethibiti kuwa ni kweli kiilimu, na ufupi wake ni kuwa ulimwengu unaendelea kukua na kupanuka, na kila sayari za mbinguni zinajitenga wenyewe kwa wenyewe.

التفاسير:

external-link copy
49 : 51

وَمِن كُلِّ شَيۡءٍ خَلَقۡنَا زَوۡجَيۡنِ لَعَلَّكُمۡ تَذَكَّرُونَ

Na katika kila kitu tumeumba kwa jozi ili mzingatie. info

Na kila kitu tumekiumba namna mbili, yaani kwa jozi, ili mpate kukumbuka muuamini uwezo wetu.

التفاسير:

external-link copy
50 : 51

فَفِرُّوٓاْ إِلَى ٱللَّهِۖ إِنِّي لَكُم مِّنۡهُ نَذِيرٞ مُّبِينٞ

Basi kimbilieni kwa Mwenyezi Mungu, hakika mimi ni mwonyaji kwenu wa kubainisha nitokae kwake. info

Basi fanyeni haraka kuendea kwenye ut'iifu wa Mwenyezi Mungu.

التفاسير:

external-link copy
51 : 51

وَلَا تَجۡعَلُواْ مَعَ ٱللَّهِ إِلَٰهًا ءَاخَرَۖ إِنِّي لَكُم مِّنۡهُ نَذِيرٞ مُّبِينٞ

Wala msifanye kuwa kuna mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu. Hakika mimi ni mwonyaji kwenu wa kubainisha nitokae kwake. info

Wala msimfanye mungu mwengine kuwa pamoja na Mwenyezi Mungu. Hakika mimi nimekujieni kwa amri ya Mwenyezi Mungu kukuonyeni kwa uwazi matokeo ya ushirikina.

التفاسير:

external-link copy
52 : 51

كَذَٰلِكَ مَآ أَتَى ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِم مِّن رَّسُولٍ إِلَّا قَالُواْ سَاحِرٌ أَوۡ مَجۡنُونٌ

Basi ndio hivyo hivyo, hakuwajia kabla yao Mtume ila walisema: Huyu ni mchawi au mwendawazimu. info

Hivyo ndivyo ilivyo kuwa hali ya mataifa yote kwa Mitume wao. Hakuja Mtume kwa watu wa kabla ya kaumu yako ila walimwita: Mchawi au mwendawazimu.

التفاسير:

external-link copy
53 : 51

أَتَوَاصَوۡاْ بِهِۦۚ بَلۡ هُمۡ قَوۡمٞ طَاغُونَ

Je! Wameambizana kwa haya? Bali hawa ni watu waasi. info

Je! Mmeusiana, mmeambizana, nyinyi kwa nyinyi kusema hivyo ndio maana mnalirejea hilo kwa hilo? Bali hao ni watu walio pindukia mipaka, ndio wakawafikiana katika kuwashutumu Mitume!

التفاسير:

external-link copy
54 : 51

فَتَوَلَّ عَنۡهُمۡ فَمَآ أَنتَ بِمَلُومٖ

Basi waachilie mbali, nawe hulaumiwi. info

Basi wapuuzilie mbali hawa wenye inda! Wewe hulaumiki usipo wajibu kitu.

التفاسير:

external-link copy
55 : 51

وَذَكِّرۡ فَإِنَّ ٱلذِّكۡرَىٰ تَنفَعُ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ

Na kumbusha, kwani ukumbusho huwafaa Waumini. info

Wewe dumisha kukumbusha, kwani ukumbusho huwazidisha Waumini kufumbua macho na kuwa na nguvu za yakini.

التفاسير:

external-link copy
56 : 51

وَمَا خَلَقۡتُ ٱلۡجِنَّ وَٱلۡإِنسَ إِلَّا لِيَعۡبُدُونِ

Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi. info

Wala sikuwaumba majini na watu kwa jambo la kuniletea Mimi manufaa, bali ili waniabudu, na kuniabudu Mimi ni manufaa kwao.

التفاسير:

external-link copy
57 : 51

مَآ أُرِيدُ مِنۡهُم مِّن رِّزۡقٖ وَمَآ أُرِيدُ أَن يُطۡعِمُونِ

Na sitaki kwao riziki, wala sitaki wanilishe.Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kuruzuku, Mwenye nguvu, Madhubuti. info

Sitaki kwao riziki, kwani Mimi si mhitaji kwa walimwengu wote; wala sitaki wanilishe, kwani Mimi ndiye ninaye lisha, wala silishwi.

التفاسير:

external-link copy
58 : 51

إِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلرَّزَّاقُ ذُو ٱلۡقُوَّةِ ٱلۡمَتِينُ

Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kuruzuku, Mwenye nguvu, Madhubuti. info

Hakika Mwenyezi Mungu peke yake, ndiye mdhamini wa kuwapa riziki waja wake, na Yeye ndiye Mwenye nguvu, Aliye imara, hashindiki.

التفاسير:

external-link copy
59 : 51

فَإِنَّ لِلَّذِينَ ظَلَمُواْ ذَنُوبٗا مِّثۡلَ ذَنُوبِ أَصۡحَٰبِهِمۡ فَلَا يَسۡتَعۡجِلُونِ

Hakika walio dhulumu wana fungu lao la adhabu kama fungu la wenzao. Basi wasinihimize. info

Hakika hao walio jidhulumu nafsi zao kwa ukafiri na kukanusha wana fungu lao la adhabu mfano wa fungu la wenzao katika kaumu zilizo kwisha pita. Basi wasifanye haraka kuhimiza adhabu ishuke kabla ya wakati wake.

التفاسير:

external-link copy
60 : 51

فَوَيۡلٞ لِّلَّذِينَ كَفَرُواْ مِن يَوۡمِهِمُ ٱلَّذِي يُوعَدُونَ

Ole wao walio ikanusha siku yao waliyo ahidiwa. info

Basi maangamio yatawapata wenye kuikataa siku yao waliyo ahidiwa, kwa sababu ya shida na vitisho viliomo katika siku hiyo.

التفاسير: