Bản dịch ý nghĩa nội dung Qur'an - 斯瓦西里语翻译 - 阿里·穆哈辛·拜拉瓦尼

Fatir

external-link copy
1 : 35

ٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِ فَاطِرِ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ جَاعِلِ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةِ رُسُلًا أُوْلِيٓ أَجۡنِحَةٖ مَّثۡنَىٰ وَثُلَٰثَ وَرُبَٰعَۚ يَزِيدُ فِي ٱلۡخَلۡقِ مَا يَشَآءُۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ

Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, Muumba wa mbingu na ardhi, aliye wafanya Malaika kuwa wajumbe wenye mbawa, mbili-mbili, na tatu- tatu, na nne-nne. Huzidisha katika kuumba apendavyo. Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza juu ya kila kitu. info

Anaye stahiki sifa njema ni Mwenyezi Mungu peke yake. Yeye ndiye aliye zifanya mbingu na ardhi zikawa bila ya kuwapo ruwaza ya kuigia mfano wake. Naye ndiye aliye wajaalia Malaika kuwa ni wajumbe kuwatuma kwa viumbe vyake. Wao hao wana mbawa za idadi mbali mbali, mbili-mbili, tatu-tatu, na nne-nne. Yeye huzidisha katika kuumba kwake kama atakavyo kuzidisha. Hashindwi na kitu. Hakika Mwenyezi Mungu ana uweza mkubwa juu ya kila kitu.

التفاسير:

external-link copy
2 : 35

مَّا يَفۡتَحِ ٱللَّهُ لِلنَّاسِ مِن رَّحۡمَةٖ فَلَا مُمۡسِكَ لَهَاۖ وَمَا يُمۡسِكۡ فَلَا مُرۡسِلَ لَهُۥ مِنۢ بَعۡدِهِۦۚ وَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ

Rehema ambayo Mwenyezi Mungu anawafungulia watu hapana wa kuizuia. Na anayo izuia hapana wa kuipeleka isipo kuwa Yeye. Naye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hikima. info

Mwenyezi Mungu akipeleka rehema kwa watu, rehema yoyote ile iwayo, ikiwa ni mvua, au neema, au amani, au hikima - hapana mtu yeyote awezaye kuwazuilia na kuwanyima. Na chochote katika hivyo akikizuilia Yeye basi hapana mmoja awezaye kukifungulia isipo kuwa Yeye Mwenyewe. Na Yeye ndiye Mwenye kushinda ambaye hashindwi. Mwenye hikima asiye kosea.

التفاسير:

external-link copy
3 : 35

يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ ٱذۡكُرُواْ نِعۡمَتَ ٱللَّهِ عَلَيۡكُمۡۚ هَلۡ مِنۡ خَٰلِقٍ غَيۡرُ ٱللَّهِ يَرۡزُقُكُم مِّنَ ٱلسَّمَآءِ وَٱلۡأَرۡضِۚ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَۖ فَأَنَّىٰ تُؤۡفَكُونَ

Enyi watu! Kumbukeni neema za Mwenyezi Mungu juu yenu. Ati yupo muumba mwengine asiye kuwa Mwenyezi Mungu anaye kupeni riziki kutoka mbinguni na kwenye ardhi? Hapana mungu ila Yeye tu. Basi wapi mnako geuzwa? info

Enyi watu! Kumbukeni neema za Mwenyezi Mungu zilio juu yenu, kwa kuzishukuru na kutimiza haki yake. Na mkiri hayo yaliyo tokea ndani ya nafsi zenu, ya kwamba hapana muumba isipo kuwa Mwenyezi Mungu ambaye anakuruzukuni kutoka mbinguni kwa zinavyo viteremsha, na kutoka kwenye ardhi kwa vinavyo toka humo, ambavyo vinakuleteeni uhai wenu. Hapana mungu isipo kuwa Yeye anaye waruzuku waja wake. Basi yawaje mnavyo geuzwa mkaacha Tawhidi ya Muumba wenu na Mwenye kukuruzukuni mkaendea kumshirikisha katika ibada yake?

التفاسير: