Bản dịch ý nghĩa nội dung Qur'an - 斯瓦西里语翻译 - 阿里·穆哈辛·拜拉瓦尼

Số trang:close

external-link copy
84 : 18

إِنَّا مَكَّنَّا لَهُۥ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَءَاتَيۡنَٰهُ مِن كُلِّ شَيۡءٖ سَبَبٗا

Sisi tulimtilia nguvu katika ardhi na tukampa njia za kila kitu. info

Tumemtilia nguvu amri yake katika ardhi, akiendesha humo mambo kwa mazingatio yake na utawala wake. Na tukampa ujuzi mwingi kwa njia ambazo kwazo akiweza kuongoza mambo.

التفاسير:

external-link copy
85 : 18

فَأَتۡبَعَ سَبَبًا

Basi akaifuata njia. info

Kwa kutumia njia hizo aliweza kueneza madaraka yake katika ardhi, na akafuata njia mpaka akafika huko magharibi kunako kuchwa jua.

التفاسير:

external-link copy
86 : 18

حَتَّىٰٓ إِذَا بَلَغَ مَغۡرِبَ ٱلشَّمۡسِ وَجَدَهَا تَغۡرُبُ فِي عَيۡنٍ حَمِئَةٖ وَوَجَدَ عِندَهَا قَوۡمٗاۖ قُلۡنَا يَٰذَا ٱلۡقَرۡنَيۡنِ إِمَّآ أَن تُعَذِّبَ وَإِمَّآ أَن تَتَّخِذَ فِيهِمۡ حُسۡنٗا

Hata alipo fika machwea-jua aliliona linatua katika checmchem yenye matope meusi. Na hapo akawakuta watu. Tukasema: Ewe Dhul-Qarnaini! Ama uwaadhibu au watwae kwa wema. info

Akenda mpaka akafika pahala mbali huko upande wa magharibi, akalikuta jua kwa linavyo onekana kwa macho kama kwamba linazama pahala penye chemchem ya maji ya moto na matope meusi. Na karibu ya chemchem hii Dhul- Qarnaini aliwakuta watu makafiri. Mwenyezi Mungu akamtia moyoni mwake afanye mojapo ya mambo mawili: Ama awaite kwenye Imani, na hili kwa hakika ni jambo zuri; au awapige vita ikiwa hawakuitikia wito wa Imani.

التفاسير:

external-link copy
87 : 18

قَالَ أَمَّا مَن ظَلَمَ فَسَوۡفَ نُعَذِّبُهُۥ ثُمَّ يُرَدُّ إِلَىٰ رَبِّهِۦ فَيُعَذِّبُهُۥ عَذَابٗا نُّكۡرٗا

Akasema: Ama aliye dhulumu basi tutamuadhibu, na kisha atarudishwa kwa Mola wake Mlezi amuadhibu adhabu isiyo juulikana. info

Dhul-Qarnaini akawatangazia: Katika wao aliye jidhulumu nafsi yake kwa kubakia katika ushirikina, basi amestahiki adhabu ya duniani kutokana naye, na kisha atarejea kwa Mola wake Mlezi. Naye atamuadhibu adhabu kali wasio ijua.

التفاسير:

external-link copy
88 : 18

وَأَمَّا مَنۡ ءَامَنَ وَعَمِلَ صَٰلِحٗا فَلَهُۥ جَزَآءً ٱلۡحُسۡنَىٰۖ وَسَنَقُولُ لَهُۥ مِنۡ أَمۡرِنَا يُسۡرٗا

Na ama aliye amini na akatenda mema basi atapata malipo mazuri. Nasi tutamwambia lilio jepesi katika amri yetu. info

Na ama mwenye kumuitikia, na akamuamini Mola wake Mlezi, na akatenda mema, basi atapata malipo mazuri Akhera, na hapa duniani tunamchukulia kwa upole na wepesi.

التفاسير:

external-link copy
89 : 18

ثُمَّ أَتۡبَعَ سَبَبًا

Kisha akaifuata njia. info

Kisha Dhul-Qarnaini akaendelea vile vile huku akiomba tawfiki ya Mwenyezi Mungu, na akafuata njia ya kufikilia matokea jua upande wa mashariki.

التفاسير:

external-link copy
90 : 18

حَتَّىٰٓ إِذَا بَلَغَ مَطۡلِعَ ٱلشَّمۡسِ وَجَدَهَا تَطۡلُعُ عَلَىٰ قَوۡمٖ لَّمۡ نَجۡعَل لَّهُم مِّن دُونِهَا سِتۡرٗا

Hata alipo fika matokeo ya jua aliliona linawachomozea watu tusio wawekea pazia la kuwakinga nalo. info

Hata akafika linapo chomoza jua, kwa ionekanavyo kwa macho, mwisho wa majenzi. Akawaona watu wanaishi katika ushenzi kabisa. Hawana hata cha kuwasitiri na joto.

التفاسير:

external-link copy
91 : 18

كَذَٰلِكَۖ وَقَدۡ أَحَطۡنَا بِمَا لَدَيۡهِ خُبۡرٗا

Ndio hivyo hivyo. Na Sisi tulizijua vilivyo khabari zake zote. info

Na kama Dhul-Qarnaini alivyo waita watu wa magharibi waje kuamini basi kadhaalika aliwaita hawa, na akenda nao mwendo ule ule wake wa mwanzo.

التفاسير:

external-link copy
92 : 18

ثُمَّ أَتۡبَعَ سَبَبًا

Kisha akaifuata njia. info

Kisha akaendelea vile vile akitumia mbinu alizo msahilishia Mwenyezi Mungu za kumpa tawfiki, akishika njia baina ya mashariki na magharibi.

التفاسير:

external-link copy
93 : 18

حَتَّىٰٓ إِذَا بَلَغَ بَيۡنَ ٱلسَّدَّيۡنِ وَجَدَ مِن دُونِهِمَا قَوۡمٗا لَّا يَكَادُونَ يَفۡقَهُونَ قَوۡلٗا

Hata alipo fika baina ya milima miwili, alikuta nyuma yake watu ambao takriban hawakuwa wanafahamu lolote. info

Mpaka akafika - katika safari yake ya tatu - pahala mbali baina ya milima miwili mirefu...Na huko akakuta watu ambao hawafahamu wanalo ambiwa ila kwa uzito na mashaka. Hiyo ngome au boma baina ya milima miwili iliyo tajwa katika maelezo ya juu ni milima ya Azarbajan na Arminia, na kauli nyingine ni kaskazini ya mwisho katika jimbo la Turkistan.

التفاسير:

external-link copy
94 : 18

قَالُواْ يَٰذَا ٱلۡقَرۡنَيۡنِ إِنَّ يَأۡجُوجَ وَمَأۡجُوجَ مُفۡسِدُونَ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَهَلۡ نَجۡعَلُ لَكَ خَرۡجًا عَلَىٰٓ أَن تَجۡعَلَ بَيۡنَنَا وَبَيۡنَهُمۡ سَدّٗا

Wakasema: Ewe Dhul-Qarnaini! Hakika Juju-wa-maajuju wanafanya uharibifu katika nchi. Basi je, tukulipe ujira ili utujengee baina yetu na wao ngome? info

Walipo ziona nguvu zake na uwezo wake wakamtaka awasimamishie ngome ya kuwalinda na Juju-wa-maajuju. Nao hao ni watu wanao waonea maya, na wanawafisidia na kuwaharibia nchi yao. Na wao walikuwa watayari wamlipe ujira kwa kazi hiyo.

التفاسير:

external-link copy
95 : 18

قَالَ مَا مَكَّنِّي فِيهِ رَبِّي خَيۡرٞ فَأَعِينُونِي بِقُوَّةٍ أَجۡعَلۡ بَيۡنَكُمۡ وَبَيۡنَهُمۡ رَدۡمًا

Akasema: Yale Mola wangu aliyo niwezesha ni bora zaidi. Lakini nyinyi nisaidieni kwa nguvu zenu. Nitakujengeeni kizuizi baina yenu na wao. info

Akawajibu kwa kuwaambia: Mali na madaraka aliyo nijaalia Mwenyezi Mungu ni bora zaidi kuliko hayo mnayo taka kunipa. Akaanza kusimamisha hiyo ngome, na akawataka wamsaidie kama wawezavyo kwa watu na zana ili awatimizie wayatakayo.

التفاسير:

external-link copy
96 : 18

ءَاتُونِي زُبَرَ ٱلۡحَدِيدِۖ حَتَّىٰٓ إِذَا سَاوَىٰ بَيۡنَ ٱلصَّدَفَيۡنِ قَالَ ٱنفُخُواْۖ حَتَّىٰٓ إِذَا جَعَلَهُۥ نَارٗا قَالَ ءَاتُونِيٓ أُفۡرِغۡ عَلَيۡهِ قِطۡرٗا

Nileteeni vipande vya chuma. Hata alipo ijaza nafasi iliyo kati ya milima miwili, akasema: Vukuteni. Hata alipo kifanya (chuma) kama moto akasema: Nileteeni shaba iliyo yayuka niimwagie. info

Akawataka wamkusanyie vipande vya chuma. Wakakusanya kama alivyo taka. Akajenga kwa hivyo ngome ndefu iliyo lingana na kingo za milima hiyo miwili. Kisha akawaamrisha wawashe moto, wakauwasha, mpaka chuma kikayayuka. Tena akamimina juu yake shaba iliyo kwisha yayushwa; ikawa ngome madhubuti, haipitiki.

التفاسير:

external-link copy
97 : 18

فَمَا ٱسۡطَٰعُوٓاْ أَن يَظۡهَرُوهُ وَمَا ٱسۡتَطَٰعُواْ لَهُۥ نَقۡبٗا

Basi hawakuweza kuukwea, wala hawakuweza kuutoboa. info

Basi wale mahasidi hawakuweza kulikwea lile boma, jinsi lilivyo kwenda juu, wala kulitoboa kwa ugumu wake.

التفاسير: