Bản dịch ý nghĩa nội dung Qur'an - 斯瓦西里语翻译 - 阿卜杜拉·穆罕默德和纳索尔·胡麦斯

Số trang:close

external-link copy
51 : 30

وَلَئِنۡ أَرۡسَلۡنَا رِيحٗا فَرَأَوۡهُ مُصۡفَرّٗا لَّظَلُّواْ مِنۢ بَعۡدِهِۦ يَكۡفُرُونَ

Na tukiupeleka kwenye mashamba yao ya nafaka na mimea yao upepo wenye kuharibu, wakaiona mimea yao imeharibika kwa upepo huo, ikawa imekuwa rangi ya manjano baada ya kuwa rangi ya kijani, wangalikaa baada ya kuiona wakimkufuru Mwenyezi Mungu na kuzikanusha neema Zake. info
التفاسير:

external-link copy
52 : 30

فَإِنَّكَ لَا تُسۡمِعُ ٱلۡمَوۡتَىٰ وَلَا تُسۡمِعُ ٱلصُّمَّ ٱلدُّعَآءَ إِذَا وَلَّوۡاْ مُدۡبِرِينَ

Kwa hakika wewe, ewe Mtume, humsikilizishi yule ambaye moyo wake umekufa au mashikio yake yamezibana yakawa hayaisikii haki. Basi usibabaike wala usisikitike kwa kukataa kukuamini hawa washirikina, kwani wao ni kama viziwi na wafu, hawasikii wala hawahisi hata kama wako mbele yako, basi itakuwa vipi iwapo hawako na wewe na wamekupa mgongo. info
التفاسير:

external-link copy
53 : 30

وَمَآ أَنتَ بِهَٰدِ ٱلۡعُمۡيِ عَن ضَلَٰلَتِهِمۡۖ إِن تُسۡمِعُ إِلَّا مَن يُؤۡمِنُ بِـَٔايَٰتِنَا فَهُم مُّسۡلِمُونَ

Na hukuwa wewe, ewe mtume, ni mwenye kumuongoza yule aliyefanywa kipofu na Mwenyezi Mungu asiione njia ya uongofu. Utakayemsikilizisha akanufaika kwa kusikia si mwingine isipokuwa yule anayeziamini aya zetu, basi hao ni wenye kuandama na kufuata amri ya Mwenyezi Mungu. info
التفاسير:

external-link copy
54 : 30

۞ ٱللَّهُ ٱلَّذِي خَلَقَكُم مِّن ضَعۡفٖ ثُمَّ جَعَلَ مِنۢ بَعۡدِ ضَعۡفٖ قُوَّةٗ ثُمَّ جَعَلَ مِنۢ بَعۡدِ قُوَّةٖ ضَعۡفٗا وَشَيۡبَةٗۚ يَخۡلُقُ مَا يَشَآءُۚ وَهُوَ ٱلۡعَلِيمُ ٱلۡقَدِيرُ

Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Ndiye Ambaye Amewaumba kwa maji ya udhaifu na unyonge, nayo ni tone la manii, kisha akaleta, baada ya udhaifu wa utoto, nguvu za utu uzima, kisha akaleta, baada ya nguvu hizi, udhaifu wa uzee na ukongwe. Anaumba Anachotaka cha udhaifu na nguvu. Na Yeye Ndiye Mjuzi wa viumbe Vyake, Ndiye Muweza wa kila kitu. info
التفاسير:

external-link copy
55 : 30

وَيَوۡمَ تَقُومُ ٱلسَّاعَةُ يُقۡسِمُ ٱلۡمُجۡرِمُونَ مَا لَبِثُواْ غَيۡرَ سَاعَةٖۚ كَذَٰلِكَ كَانُواْ يُؤۡفَكُونَ

Na siku kitakapokuja Kiyama na Atakapo Mwenyezi Mungu kuwafufua viumbe kutoka makaburini mwao, wataapa washirikina kwamba hawakukaa duniani isipokuwa kipindi kifupi cha wakati. Watasema urongo katika kiapo chao kama walivyokuwa wakisema urongo duniani na wakiikataa haki ambayo Mitume walikuja nayo. info
التفاسير:

external-link copy
56 : 30

وَقَالَ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡعِلۡمَ وَٱلۡإِيمَٰنَ لَقَدۡ لَبِثۡتُمۡ فِي كِتَٰبِ ٱللَّهِ إِلَىٰ يَوۡمِ ٱلۡبَعۡثِۖ فَهَٰذَا يَوۡمُ ٱلۡبَعۡثِ وَلَٰكِنَّكُمۡ كُنتُمۡ لَا تَعۡلَمُونَ

Na watasema wale waliopewa elimu na imani ya Mwenyezi Mungu, miongoni mwa Malaika, Mitume na Waumini, «Mlikuwa mmekaa katika kile Alichokiandika Mwenyezi Mungu, kutokana na ujuzi Wake uliotangulia, kuanzia siku mliyoumbwa mpaka mkafufuliwa. Basi hii ndio Siku ya Ufufuzi, lakini nyinyi mlikuwa hamjui, ndipo mkaikataa duniani na mkaikanusha.» info
التفاسير:

external-link copy
57 : 30

فَيَوۡمَئِذٖ لَّا يَنفَعُ ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ مَعۡذِرَتُهُمۡ وَلَا هُمۡ يُسۡتَعۡتَبُونَ

Basi Siku ya Kiyama, hazitawafaa madhalimu nyudhuru zao wazitowazo, na hawatatakiwa wamridhishe Mwenyezi Mungu kwa kutubia na kutii, isipokuwa watateswa kwa makosa yao na maasia yao. info
التفاسير:

external-link copy
58 : 30

وَلَقَدۡ ضَرَبۡنَا لِلنَّاسِ فِي هَٰذَا ٱلۡقُرۡءَانِ مِن كُلِّ مَثَلٖۚ وَلَئِن جِئۡتَهُم بِـَٔايَةٖ لَّيَقُولَنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ إِنۡ أَنتُمۡ إِلَّا مُبۡطِلُونَ

Hakika tuliwafafanulia watu, katika hii Qur’ani, kila mfano ili kuwasimamishia hoja na kuthibitisha kuwa Mwenyezi Mungu ni Mmoja, Aliyetukuka na kuwa juu. Na lau ungaliwajia na hoja yoyote yenye kuonyesha ukweli wako, wale waliokukanusha wangalisema kukwambia, «Hamkuwa nyinyi, ewe Mtume na wafuasi wako, isipokuwa ni warongo katika yale mambo mnayotuletea.» info
التفاسير:

external-link copy
59 : 30

كَذَٰلِكَ يَطۡبَعُ ٱللَّهُ عَلَىٰ قُلُوبِ ٱلَّذِينَ لَا يَعۡلَمُونَ

Mfano wa muhuri huu, Mwenyezi Mungu Anapiga muhuri juu ya nyoyo za wasioujua uhakika wa kile unachowaletea, ewe Mtume, kutoka kwa Mwenyezi Mungu kutokana na mazingatio haya na miujiza iliyo waziwazi. info
التفاسير:

external-link copy
60 : 30

فَٱصۡبِرۡ إِنَّ وَعۡدَ ٱللَّهِ حَقّٞۖ وَلَا يَسۡتَخِفَّنَّكَ ٱلَّذِينَ لَا يُوقِنُونَ

Basi vumilia, ewe Mtume, kwa yale yanayokupata ya makero ya watu wako kwako na kukukanusha kwao, kwani ahadi ya Mwenyezi Mungu kwako ya ushindi, uthabiti na malipo mema ni kweli isiyo na shaka. Na wasikubabaishe wakakuweka kando na Dini yako wale wasiokuwa na yakini ya Agizo (la Siku ya Kiyama) na wasioamini kufufuliwa na malipo. info
التفاسير: