Bản dịch ý nghĩa nội dung Qur'an - 斯瓦西里语翻译 - 阿卜杜拉·穆罕默德和纳索尔·胡麦斯

Số trang:close

external-link copy
6 : 30

وَعۡدَ ٱللَّهِۖ لَا يُخۡلِفُ ٱللَّهُ وَعۡدَهُۥ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَعۡلَمُونَ

Mwenyezi Mungu Amewaahidi Waumini, ahadi ya kukata isiyoenda kinyume, kuwapa ushindi Warumi juu ya Wafursi wenye kuabudu masanamu. Lakini wengi wa makafiri wa Makkah hawajui kwamba kile Alichokiahidi Mwenyezi Mungu ni kweli, info
التفاسير:

external-link copy
7 : 30

يَعۡلَمُونَ ظَٰهِرٗا مِّنَ ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا وَهُمۡ عَنِ ٱلۡأٓخِرَةِ هُمۡ غَٰفِلُونَ

Wanayoyajua wao ni mambo yaliyofunuka wazi ya dunia na pambo lake, na wao kuhusu mambo ya Akhera na yale yanayowafaa huko wameghafilika, hawayafikirii. info
التفاسير:

external-link copy
8 : 30

أَوَلَمۡ يَتَفَكَّرُواْ فِيٓ أَنفُسِهِمۗ مَّا خَلَقَ ٱللَّهُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ وَمَا بَيۡنَهُمَآ إِلَّا بِٱلۡحَقِّ وَأَجَلٖ مُّسَمّٗىۗ وَإِنَّ كَثِيرٗا مِّنَ ٱلنَّاسِ بِلِقَآيِٕ رَبِّهِمۡ لَكَٰفِرُونَ

Kwani hawakufikiri, hawa wakanushaji Mitume wa Mwenyezi Mungu na kukutana na Yeye, vile Mwenyezi Mungu Alivyowaumba, na kuwa wao Amewaumba na hawakuwa kitu chochote? Mwenyezi Mungu hakuumba mbingu na ardhi na vilivyo baina yake isipokuwa ni kwa ajili ya kusimamisha uadilifu, malipo mema na mateso na kutolea ushahidi upweke Wake na uweza Wake. Na kwa muda uliotajwa wa kukomea kwake nao ni Siku ya Kiyama. Na kwa hakika, wengi wa watu ni wenye kukataa na kukanusha kwa ujinga wao wa kutojua kuwa marejeo yao ni kwa Mwenyezi Mungu baada ya kutoweka kwao na kwa kughafilika kwao na Akhera. info
التفاسير:

external-link copy
9 : 30

أَوَلَمۡ يَسِيرُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَيَنظُرُواْ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡۚ كَانُوٓاْ أَشَدَّ مِنۡهُمۡ قُوَّةٗ وَأَثَارُواْ ٱلۡأَرۡضَ وَعَمَرُوهَآ أَكۡثَرَ مِمَّا عَمَرُوهَا وَجَآءَتۡهُمۡ رُسُلُهُم بِٱلۡبَيِّنَٰتِۖ فَمَا كَانَ ٱللَّهُ لِيَظۡلِمَهُمۡ وَلَٰكِن كَانُوٓاْ أَنفُسَهُمۡ يَظۡلِمُونَ

Basi si waende hawa wanaomkanusha Mwenyezi Mungu, wanaoghafilika na Akhera, mwendo wa kufikiria na kuzingatia, wakapata kuona yalikuwa namna gani malipo ya ummah waliowakanusha Mitume wa Mwenyezi Mungu, kama vile kina ‘Ād na Thamūd? Hakika walikuwa wana nguvu zaidi kuliko wao kimiili na wana uwezo zaidi wa kustarehe na maisha, kwa kuwa waliilima ardhi na kuipanda mimea, na wakajenga majumba ya fahari na wakayakalia, hivyo basi waliuamirisha ulimwengu wao kuliko vile watu wa Makkah walivyouamirisha ulimwengu wao, na kusiwafalie kitu kule kuamirisha kwao wala urefu wa maisha yao. Na Mitume wao waliwajia na hoja waziwazi na dalili zenye kung’ara, wakawakanusha na Mwenyezi Mungu Akawaangamiza. Na Hakuwadhulumu kwa huko kuwaangamiza, isipokuwa wao wenyewe walijidhulumu wenyewe kwa kufanya ushirikina na kuasi. info
التفاسير:

external-link copy
10 : 30

ثُمَّ كَانَ عَٰقِبَةَ ٱلَّذِينَ أَسَٰٓـُٔواْ ٱلسُّوٓأَىٰٓ أَن كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ وَكَانُواْ بِهَا يَسۡتَهۡزِءُونَ

Kisha ulikuwa mwisho wa waovu, miongoni mwa madhalimu na makafiri, ni mbaya zaidi na muovu zaidi, kwa kumkanusha kwao Mwenyezi Mungu na kuzifanyia shere aya Zake ambazo Aliziteremsha kwa Mitume Wake. info
التفاسير:

external-link copy
11 : 30

ٱللَّهُ يَبۡدَؤُاْ ٱلۡخَلۡقَ ثُمَّ يُعِيدُهُۥ ثُمَّ إِلَيۡهِ تُرۡجَعُونَ

Mwenyezi Mungu, Peke Yake, Ndiye Aliyepwekeka kwa kuanzisha uumbaji viumbe vyote. Na Yeye Ndiye Anayeweza, Peke Yake, kuvirudisha mara nyingine, kisha Kwake Yeye watarejea viumbe wote, Amlipe aliye mwema kwa wema wake na aliye mbaya kwa ubaya wake. info
التفاسير:

external-link copy
12 : 30

وَيَوۡمَ تَقُومُ ٱلسَّاعَةُ يُبۡلِسُ ٱلۡمُجۡرِمُونَ

Na Siku ambayo Kiyama kitasimama wahalifu watakata tamaa ya kuokoka na adhabu, na utawapata wao mshangao utakaokata hoja zao. info
التفاسير:

external-link copy
13 : 30

وَلَمۡ يَكُن لَّهُم مِّن شُرَكَآئِهِمۡ شُفَعَٰٓؤُاْ وَكَانُواْ بِشُرَكَآئِهِمۡ كَٰفِرِينَ

Na washirikina , Siku hiyo, hawatokuwa na waombezi kati ya waungu wao waliokuwa wakiwaabudu badala ya Mwenyezi Mungu, bali wao, hao waungu, watajiepusha nao na wao watajiepusha nao. Maombezi ni ya Mwenyezi Mungu Peke Yake, na hayatafutwi kutoka kwa mwingine. info
التفاسير:

external-link copy
14 : 30

وَيَوۡمَ تَقُومُ ٱلسَّاعَةُ يَوۡمَئِذٖ يَتَفَرَّقُونَ

Na Siku ambayo Kiyama kitasimama, watatengana watu wa Imani na watu wa ukafiri, info
التفاسير:

external-link copy
15 : 30

فَأَمَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ فَهُمۡ فِي رَوۡضَةٖ يُحۡبَرُونَ

Ama waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, wenye kufanya matendo mema, watakuwa Peponi ambapo watakirimiwa, watafurahishwa na wataneemeshwa. info
التفاسير: