قرآن کریم کے معانی کا ترجمہ - سواحلی ترجمہ - علی محسن البروانی

صفحہ نمبر:close

external-link copy
19 : 35

وَمَا يَسۡتَوِي ٱلۡأَعۡمَىٰ وَٱلۡبَصِيرُ

Na kipofu na mwenye kuona hawalingani. info

Hawawezi kulingana wakawa sawa:- asiye hidika kuifuata Haki kwa ujinga wake na mwenye kufuata Njia ya uwongofu kwa ujuzi wake; wala uwongo na kweli; wala kivuli na upepo umoto

التفاسير:

external-link copy
20 : 35

وَلَا ٱلظُّلُمَٰتُ وَلَا ٱلنُّورُ

Wala giza na mwangaza. info

Hawawezi kulingana wakawa sawa:- asiye hidika kuifuata Haki kwa ujinga wake na mwenye kufuata Njia ya uwongofu kwa ujuzi wake; wala uwongo na kweli; wala kivuli na upepo umoto

التفاسير:

external-link copy
21 : 35

وَلَا ٱلظِّلُّ وَلَا ٱلۡحَرُورُ

Wala kivuli na joto. info

Hawawezi kulingana wakawa sawa:- asiye hidika kuifuata Haki kwa ujinga wake na mwenye kufuata Njia ya uwongofu kwa ujuzi wake; wala uwongo na kweli; wala kivuli na upepo umoto

التفاسير:

external-link copy
22 : 35

وَمَا يَسۡتَوِي ٱلۡأَحۡيَآءُ وَلَا ٱلۡأَمۡوَٰتُۚ إِنَّ ٱللَّهَ يُسۡمِعُ مَن يَشَآءُۖ وَمَآ أَنتَ بِمُسۡمِعٖ مَّن فِي ٱلۡقُبُورِ

Wala hawalingani walio hai na maiti. Hakika Mwenyezi Mungu humsikilizisha amtakaye. Wala wewe si wa kuwasikilizisha walio makaburini. info
التفاسير:

external-link copy
23 : 35

إِنۡ أَنتَ إِلَّا نَذِيرٌ

Hukuwa wewe ila ni mwonyaji. info

Wewe huna jukumu ila la kufikisha Ujumbe na kuonya tu.

التفاسير:

external-link copy
24 : 35

إِنَّآ أَرۡسَلۡنَٰكَ بِٱلۡحَقِّ بَشِيرٗا وَنَذِيرٗاۚ وَإِن مِّنۡ أُمَّةٍ إِلَّا خَلَا فِيهَا نَذِيرٞ

Hakika Sisi tumekutuma wewe kwa Haki, kuwa ni mbashiri na mwonyaji. Na hapana umma wowote ila ulipata mwonyaji kati yao. info

Ewe Nabii! Hakika Sisi tumekutuma wewe uwafikishie watu wote hii Dini ya Haki, ukiwabashiria Pepo wenye kuamini, na ukiwaonya kwa adhabu ya Moto wanao ikataa hii Dini. Na hapana kaumu yoyote katika kaumu zilizo pita ila walijiwa na mtu kutokana na Mwenyezi Mungu wa kuwahadharisha na adhabu yake.

التفاسير:

external-link copy
25 : 35

وَإِن يُكَذِّبُوكَ فَقَدۡ كَذَّبَ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡ جَآءَتۡهُمۡ رُسُلُهُم بِٱلۡبَيِّنَٰتِ وَبِٱلزُّبُرِ وَبِٱلۡكِتَٰبِ ٱلۡمُنِيرِ

Na wakikukanusha basi walikwisha wakanusha walio kuwa kabla yao. Mitume wao waliwajia kwa dalili wazi wazi na kwa maandiko na Kitabu chenye nuru. info

Na ikiwa kaumu yako wanakukadhibisha wewe basi walio kuwa kabla yao waliwakadhibisha Mitume wao vile vile. Na wao waliwaletea miujiza iliyo wazi, na Maandiko ya Mola Mlezi na Kitabu chenye nuru kwa ajili ya kuwaongoza Njia ya kuokoka duniani na Akhera.

التفاسير:

external-link copy
26 : 35

ثُمَّ أَخَذۡتُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْۖ فَكَيۡفَ كَانَ نَكِيرِ

Kisha nikawakamata walio kufuru. Basi kuchukia kwangu kulikuwaje? info

Kisha nikawashika walio kufuru kwa mshiko mkali. Basi hebu angalia kulikuwaje kuchukia kwangu kwa vitendo vyao, na ghadhabu yangu juu yao!

التفاسير:

external-link copy
27 : 35

أَلَمۡ تَرَ أَنَّ ٱللَّهَ أَنزَلَ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءٗ فَأَخۡرَجۡنَا بِهِۦ ثَمَرَٰتٖ مُّخۡتَلِفًا أَلۡوَٰنُهَاۚ وَمِنَ ٱلۡجِبَالِ جُدَدُۢ بِيضٞ وَحُمۡرٞ مُّخۡتَلِفٌ أَلۡوَٰنُهَا وَغَرَابِيبُ سُودٞ

Je! Huoni kwamba Mwenyezi Mungu ameteremsha maji kutoka mbinguni, na kwayo tumeyatoa matunda yenye rangi mbali mbali. Na katika milima imo mistari myeupe na myekundu yenye rangi mbali mbali, na myeusi sana. info

Ewe mwenye akili! Huoni kwamba Mwenyezi Mungu anayateremsha maji kutoka mbinguni, na kwa maji hayo anatoa mazao yanayo khitalifiana rangi zake? Mengine ni mekundu na manjano, na matamu na machungu, mazuri na mabaya. Na katika milima, ipo milima yenye njia na mistari myeupe na myekundu, yenye kukhitalifiana pia kwa kukoza na kufifia. Ya kustaajabisha kitaalamu katika Aya hii tukufu sio tu kwa kukhitalifiana rangi mbali mbali katika milima, ambazo zinatokana na hizo sehemu za maadini zilizo fanya majabali, kama vile chuma huonyesha rangi yake nyekundu, na manganese na makaa ya mawe huonekana kwa rangi nyeusi, au shaba ambayo hudhihirisha rangi ya kijani n.k. Lakini ya kustaajabisha khasa ni kuunganisha baina ya kutoa matunda ya namna mbali mbali na hali miti yake inanyweshwa maji yale yale, na kuumbwa milima myekundu, na myeupe, na myeusi, na yote yana asli moja kwa kuundwa kwake. Wataalamu wa ilimu za t'abaka za ardhi, Jiolojia, wanaita Magma. Na hii Magma moja inapo chomoza pahala mbali mbali katika ardhi, na penye vina mbali mbali (kwenda chini) katika ardhi kutoka juu basi hupatikana khitilafu katika muundo wake na hukusanyika kwa kurindika kuwa ni milima yenye maadini ya rangi mbali mbali. Na huu basi mwendo wa Mwenyezi Mungu ni mmoja. Kwani hakika asli ni moja, na matawi ndiyo yanakhitalifiana kwa kuonekana. Na katika haya yanapatikana manufaa na faida kwa binaadamu.

التفاسير:

external-link copy
28 : 35

وَمِنَ ٱلنَّاسِ وَٱلدَّوَآبِّ وَٱلۡأَنۡعَٰمِ مُخۡتَلِفٌ أَلۡوَٰنُهُۥ كَذَٰلِكَۗ إِنَّمَا يَخۡشَى ٱللَّهَ مِنۡ عِبَادِهِ ٱلۡعُلَمَٰٓؤُاْۗ إِنَّ ٱللَّهَ عَزِيزٌ غَفُورٌ

Na katika watu, na wanyama, na mifugo, pia rangi zao zinakhitalifiana. Kwa hakika wanao mcha Mwenyezi Mungu miongoni mwa waja wake ni wanazuoni. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye kusamehe. info

Na miongoni mwa watu na wanyama, na mifugo, yaani ngamia, ng'ombe, kondoo na mbuzi, kadhaalika zipo khitilafu katika sura, ukubwa na rangi. Na hawazingatii huu muumbo wa ajabu na wakamwogopa aliye umba ila wanazuoni ambao wanatambua siri ya uumbaji wake. Hakika Mwenyezi Mungu Mwenye kushinda anaogopwa na Waumini, naye ni Mwingi wa kuwafutia madhambi yao wanao rejea kwake. Baada ya kueleza kukhitalifiana matunda, na milima, na watu, na wanyama, na mifugo, inaashiriwa kuwa juu ya khitilafu hizi zinazo onekana baina ya hali hizi zote, upo umoja wa asli. Kwani hayo matunda yanatokana na maji yale yale. Na milima inatokana na Magma moja. Kadhaalika khitilafu za rangi, na watu, na wanyama, na mifugo, hazidhihiri katika tone za manii ambavyo vyote hivyo vimetoka mwanzo wake. Na lau hizo tone zingeli chunguzwa kwa darubini ya Maikroskopu kisingeli onekana kitu cha kuonyesha hizo khitilafu zitazo kuwa. Kwani hizo ni siri zilioko ndani yake katika zinazo itwa Genes (Jiinz). Na labda haya pia yanaonyesha kuwa sifa za kurithi ziliomo katika asli ya mimea, na wanyama, na binaadamu, zinalindwa katika maumbile yake, na hazigeuki kwa tabia ya pahala au chakula.

التفاسير:

external-link copy
29 : 35

إِنَّ ٱلَّذِينَ يَتۡلُونَ كِتَٰبَ ٱللَّهِ وَأَقَامُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَأَنفَقُواْ مِمَّا رَزَقۡنَٰهُمۡ سِرّٗا وَعَلَانِيَةٗ يَرۡجُونَ تِجَٰرَةٗ لَّن تَبُورَ

Hakika wale wanao soma Kitabu cha Mwenyezi Mungu, na wakashika Swala, na wakatoa kwa siri na kwa dhaahiri katika tulivyo waruzuku, hao hutaraji biashara isiyo bwaga. info

Hakika wanao soma Kitabu cha Mwenyezi Mungu, kwa kukizingatia na kukitenda, na wakashika Swala kwa mujibu itakikanavyo na wakatoa kwa siri na kwa kuonekana baadhi ya alicho waruzuku Mwenyezi Mungu, wanataraji kwa hayo kufanya na Mwenyezi Mungu biashara isiyo anguka faida yake.

التفاسير:

external-link copy
30 : 35

لِيُوَفِّيَهُمۡ أُجُورَهُمۡ وَيَزِيدَهُم مِّن فَضۡلِهِۦٓۚ إِنَّهُۥ غَفُورٞ شَكُورٞ

Ili Yeye awalipe ujira wao kwa ukamilifu, na awazidishie kutokana na fadhila zake. Hakika Yeye ni Mwenye kusamehe Mwenye shukrani. info

Ili Mwenyezi Mungu awalipe ujira wao, na awazidishie juu yake kutokana na fadhila yake kwa anavyo waongezea mema yao na kuwafutia maovu yao. Yeye ni Msamehevu, Mwingi wa kufutia makosa ya kujikwaa, Mwenye kushukuru, Mwingi wa kushukuru kwa ut'iifu wa waja.

التفاسير: