Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli kuwa anawaadhibu watu duniani, basi hapana shaka adhabu yake ingeli enea. Na asingeli muacha juu ya mgongo wa ardhi hata mnyama mmoja, kwa kuwa wote wametenda madhambi. Lakini anaakhirisha kuwaadhibu mpaka siku maalumu, nayo ni Siku ya Kiyama. Basi ukifika muda wao walio wekewa atawalipa kwa uangalizi kaamili. Kwani Yeye ni Mwenye kuviona vitendo vya waja wake; hafichikiwi na kitu chochote katika hivyo. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujua kushinda wote.