Wakashikilia katika itikadi zao, na wakazua baina ya Mwenyezi Mungu na majini, ambao hawawaoni, kuwa ati yapo makhusiano ya nasaba. Na bila ya shaka hao majini walikwisha jua kuwa makafiri watahudhurishwa mbele ya Mwenyezi Mungu ili wapate malipo yao yasiyo kimbilika.
Enyi makafiri! Hakika nyinyi, na hao mnao waabudu badala ya Mwenyezi Mungu - Nyinyi kwa kuwaabudu kwenu badala yake Yeye, hamtampoteza yeyote kwa upotovu wenu. Isipo kuwa yule ambaye tangu hapo Mwenyezi Mungu Mtukufu anamjua ni katika watu wa Motoni, na huko ataingia.
Nawe watazame, na uangalie vyema adhabu gani na mateso yatakayo wapata kwa kwenda kinyume nawe na kukukadhibisha. Basi watakuja ona kwa macho yao zitakavyo shindwa safu zao, na wataona nusura ya Mwenyezi Mungu inavyo wafikia Waumini.