Kur'an-ı Kerim meal tercümesi - Savahili Dili Tercüme - Ali Muhsin Al-Barvani

Al-Baqarah

external-link copy
1 : 2

الٓمٓ

Alif Lam Mim. info

Alif Lam Mim: Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala ameanzia kwa harufi hizi kuashiria moja katika miujiza ya Qur'ani Tukufu iliyo tungwa kwa harufi zile zile ambazo Waarabu wakitungia maneno yao, na juu ya hivyo wao wameemewa hawakuweza kuleta kitu mfano wa Qur'ani hii. Pia juu ya hivyo hizi harufi zinazindua ili upate kuzingatia yasemwayo.

التفاسير:

external-link copy
2 : 2

ذَٰلِكَ ٱلۡكِتَٰبُ لَا رَيۡبَۛ فِيهِۛ هُدٗى لِّلۡمُتَّقِينَ

Hiki ni Kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake; ni uwongofu kwa wachamungu, info

Hichi ndicho Kitabu kilicho kamilika, kisicho kuwa na dowa, nacho ni Qur'ani tunayo iteremsha isiyo tiliwa shaka yoyote na kila mwenye akili na mwenye insafu akajua kuwa inatoka kwa Mwenyezi Mungu. Wala haitilii shaka kuwa yasemwayo juu ya mambo na hukumu ni ya kweli tupu. Ndani ya Kitabu hichi upo uwongofu ulio kamilika kwa walio kuwa tayari kuitafuta Kweli, na wanajikinga na madhara na mambo ya kuwaletea adhabu.

التفاسير:

external-link copy
3 : 2

ٱلَّذِينَ يُؤۡمِنُونَ بِٱلۡغَيۡبِ وَيُقِيمُونَ ٱلصَّلَوٰةَ وَمِمَّا رَزَقۡنَٰهُمۡ يُنفِقُونَ

Ambao huyaamini ya ghaibu na hushika Sala, na hutoa katika tuliyo wapa. info

Na hawa ndio ambao, kwa kuazimia na kunyenyekea, wanayasadiki yale ya ghaibu wasio yaona kwa macho, wala kuyahisi kwa viungo, ambayo ni ya kuitakidiwa na kuaminiwa, kama mambo ya Malaika, Siku ya Akhera. Kwani msingi wa kushika Dini ni kuamini yaliyo ya ghaibu. Pia wakashika Swala vilivyo, kwa kumwelekea Mwenyezi Mungu na kumnyenyekea kikweli, na wale ambao wanatoa katika yale alio waruzuku Mwenyezi Mungu kwa ajili ya mambo ya kheri na mema.

التفاسير:

external-link copy
4 : 2

وَٱلَّذِينَ يُؤۡمِنُونَ بِمَآ أُنزِلَ إِلَيۡكَ وَمَآ أُنزِلَ مِن قَبۡلِكَ وَبِٱلۡأٓخِرَةِ هُمۡ يُوقِنُونَ

Na ambao wanayaamini yaliyo teremshwa kwako, na yaliyo teremshwa kabla yako; na Akhera wana yakini nayo. info

Na wale wanao isadiki Qur'ani ulio teremshiwa wewe (Muhammad) kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na yote yaliomo ndani yake katika mambo ya hukumu na khabari, na wakatenda yatakikanayo, na wakavisadiki Vitabu vya Mwenyezi Mungu walivyo teremshiwa Manabii na Mitume wa kabla yako, kama Taurati na Injili na vyenginevyo. Kwani risala za Mwenyezi Mungu zote zina asli moja, na hao wanatambulikana kuwa wanaamini Imani moja isiyo legalega ya Siku ya Kiyama na yatayo tokea ya Hisabu na Thawabu na Adhabu.

التفاسير:

external-link copy
5 : 2

أُوْلَٰٓئِكَ عَلَىٰ هُدٗى مِّن رَّبِّهِمۡۖ وَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡمُفۡلِحُونَ

Hao wapo juu ya uwongofu utokao kwa Mola wao Mlezi, na hao ndio walio fanikiwa. info

Hawa walio sifiwa kwa sifa zilizo tangulia, wamekua kwa kupata sababu za uwongofu wa Mwenyezi Mungu, na wamekaa imara juu ya hayo. Wao peke yao ndio walio fuzu watakao pata wayatakayo, na wayatamaniayo, nayo ni malipwa kwa kazi yao na juhudi yao, na kutimiza amri na kuepuka waliyo katazwa.

التفاسير: