Kur'an-ı Kerim meal tercümesi - Savahili Dilinde Tercüme - Abdullah Muhammed ve Nasır Hamiys

Sayfa numarası:close

external-link copy
106 : 4

وَٱسۡتَغۡفِرِ ٱللَّهَۖ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ غَفُورٗا رَّحِيمٗا

Na utake msamaha kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka katika hali zako zote. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe kwa wanaotarajia nyongeza za mema Yake na vipewa vya msamaha Wake, ni Mwingi wa huruma kwao. info
التفاسير:

external-link copy
107 : 4

وَلَا تُجَٰدِلۡ عَنِ ٱلَّذِينَ يَخۡتَانُونَ أَنفُسَهُمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُحِبُّ مَن كَانَ خَوَّانًا أَثِيمٗا

Na usiwatetee wanaozifanyia hiana nafsi zao kwa kumuasi Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na sifa za upungufu, Hampendi yule ambaye hiana yake imekuwa kubwa na dhambi zake zimekuwa nyingi. info
التفاسير:

external-link copy
108 : 4

يَسۡتَخۡفُونَ مِنَ ٱلنَّاسِ وَلَا يَسۡتَخۡفُونَ مِنَ ٱللَّهِ وَهُوَ مَعَهُمۡ إِذۡ يُبَيِّتُونَ مَا لَا يَرۡضَىٰ مِنَ ٱلۡقَوۡلِۚ وَكَانَ ٱللَّهُ بِمَا يَعۡمَلُونَ مُحِيطًا

Wao wanajificha na watu ili wasipate kuyaona matendo yao mabaya, wala hawajifichi na Mwenyezi Mungu Aliyetukuka wala hawamuonei haya, ilhali Yeye, Mtukufu wa mambo, Yupo na wao kwa ujuzi Wake, Anawaona wanapopanga, kipindi cha usiku, maneno Asiyoridhika nayo. Na Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Ameyazunguka(kwa ujuzi Kwake) maneno yao yote na vitendo vyao vyote, hakuna kitu chochote chenye kufichika Kwake. info
التفاسير:

external-link copy
109 : 4

هَٰٓأَنتُمۡ هَٰٓؤُلَآءِ جَٰدَلۡتُمۡ عَنۡهُمۡ فِي ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا فَمَن يُجَٰدِلُ ٱللَّهَ عَنۡهُمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ أَم مَّن يَكُونُ عَلَيۡهِمۡ وَكِيلٗا

Haya nyinyi, enyi Waumini, mnatoa hoja za kuwatetea hawa mahaini wa nafsi zao katika huu uhai wa kilimwengu. Basi, ni nani mwenyemuhoji Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, kwa kuwatetea wao Siku ya kufufuliwa na kuhesabiwa? Au ni nani atakayekuwa wakili wao Siku ya Kiyama? info
التفاسير:

external-link copy
110 : 4

وَمَن يَعۡمَلۡ سُوٓءًا أَوۡ يَظۡلِمۡ نَفۡسَهُۥ ثُمَّ يَسۡتَغۡفِرِ ٱللَّهَ يَجِدِ ٱللَّهَ غَفُورٗا رَّحِيمٗا

Na mwenye kufanya tendo baya au akajidhulumu nafsi yake kwa kufanya mambo yaliyo kinyume na hukumu ya Mwenyezi Mungu na sheria Yake, kisha akarudi kwa Mwenyezi Mungu kwa kujuta kwa aliyoyafanya akitaraji Amsamehe na dhambi zake Amsitirie, basi atamkuta Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa msamaha na ni mwingi wa huruma kwake. info
التفاسير:

external-link copy
111 : 4

وَمَن يَكۡسِبۡ إِثۡمٗا فَإِنَّمَا يَكۡسِبُهُۥ عَلَىٰ نَفۡسِهِۦۚ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلِيمًا حَكِيمٗا

Na Mwenye kufanya dhambi kwa kusudi, hakika huwa akijidhuru nafsi yake peke yake. Na Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, ni Mjuzi wa uhakika wa mambo ya waja Wake, ni Mwingi wa hekima katika hukumu Zake Azitowazo kwa waja Wake. info
التفاسير:

external-link copy
112 : 4

وَمَن يَكۡسِبۡ خَطِيٓـَٔةً أَوۡ إِثۡمٗا ثُمَّ يَرۡمِ بِهِۦ بَرِيٓـٔٗا فَقَدِ ٱحۡتَمَلَ بُهۡتَٰنٗا وَإِثۡمٗا مُّبِينٗا

Na mwenye kufanya kosa bila kukusudia au akatenda dhambi kwa kusudia kisha akamsingizia, yale aliyoyafanya, mtu asiye na hatia, atakuwa amebeba urongo na dhambi zilizo wazi. info
التفاسير:

external-link copy
113 : 4

وَلَوۡلَا فَضۡلُ ٱللَّهِ عَلَيۡكَ وَرَحۡمَتُهُۥ لَهَمَّت طَّآئِفَةٞ مِّنۡهُمۡ أَن يُضِلُّوكَ وَمَا يُضِلُّونَ إِلَّآ أَنفُسَهُمۡۖ وَمَا يَضُرُّونَكَ مِن شَيۡءٖۚ وَأَنزَلَ ٱللَّهُ عَلَيۡكَ ٱلۡكِتَٰبَ وَٱلۡحِكۡمَةَ وَعَلَّمَكَ مَا لَمۡ تَكُن تَعۡلَمُۚ وَكَانَ فَضۡلُ ٱللَّهِ عَلَيۡكَ عَظِيمٗا

Na lau si Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, kukuneemesha, ewe Mtume, kukurehemu kwa neema ya unabii na kukuhifadhi, kwa taufiki Yake, kwa wahyi Aliokuletea, wangaliazimia watu, miongoni mwa wale wanaozifanyia hiana nafsi zao, kukupotosha na njia ya haki. Na wao kwa kufanya hivyo, huwa hawampotoshi yoyote isipokuwa nafsi zao. Na hawawezi kukudhuru kwa kuwa Mwenyezi Mungu Amekuhifadhi, Amekuteremshia Qur’ani na Sunnah yenye kuifafanua, na Amekuongoza ukajua elimu ambayo hukuwa ukiijua hapo nyuma. Na fadhila za Mwenyezi Mungu Alizokuhusisha nazo ni jambo kubwa. info
التفاسير: