Kur'an-ı Kerim meal tercümesi - Savahili Dilinde Tercüme - Abdullah Muhammed ve Nasır Hamiys

Sayfa numarası:close

external-link copy
60 : 4

أَلَمۡ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ يَزۡعُمُونَ أَنَّهُمۡ ءَامَنُواْ بِمَآ أُنزِلَ إِلَيۡكَ وَمَآ أُنزِلَ مِن قَبۡلِكَ يُرِيدُونَ أَن يَتَحَاكَمُوٓاْ إِلَى ٱلطَّٰغُوتِ وَقَدۡ أُمِرُوٓاْ أَن يَكۡفُرُواْ بِهِۦۖ وَيُرِيدُ ٱلشَّيۡطَٰنُ أَن يُضِلَّهُمۡ ضَلَٰلَۢا بَعِيدٗا

Kwani hukujua, ewe Mtume, mambo ya wale wanafiki wenye kudai kuwa wameyaamini yale uliyoteremshiwa, nayo ni Qur’ani, na yale waliyoteremshiwa Mitume kabla yako, ilhali wao wanataka kuhukumiwa, katika ugomvi unaotokea baina yao, kwa sheria ya batili, isiyowekwa na Mwenyezi Mungu, na wao waliamrishwa kuikataa batili? Shetani anataka kuwaepusha na njia ya haki na kuwaweka mbali nayo kabisa. Katika aya hii kuna dalili kwamba Imani ya kweli inalazimu kufuata sheria ya Mwenyezi Mungu na kuitumia katika kutoa uamuzi juu ya kila jambo. Kwa hivyo, mwenye kudai kuwa ni Muumini na akachagua uamuzi wa Shetani juu ya uamuzi wa Mwenyezi Mungu, huwa ni Mrongo katika madai yake. info
التفاسير:

external-link copy
61 : 4

وَإِذَا قِيلَ لَهُمۡ تَعَالَوۡاْ إِلَىٰ مَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ وَإِلَى ٱلرَّسُولِ رَأَيۡتَ ٱلۡمُنَٰفِقِينَ يَصُدُّونَ عَنكَ صُدُودٗا

Na hawa wanaponasihiwa na kuambiwa, «Njooni kwenye yale yaliyoateremshwa na Mwenyezi Mungu na kwa Mtume na uongofu wake», utawaona wale wenye kudhihirisha Imani na kuficha ukafiri, wanakugeuka na kukupa mgongo. info
التفاسير:

external-link copy
62 : 4

فَكَيۡفَ إِذَآ أَصَٰبَتۡهُم مُّصِيبَةُۢ بِمَا قَدَّمَتۡ أَيۡدِيهِمۡ ثُمَّ جَآءُوكَ يَحۡلِفُونَ بِٱللَّهِ إِنۡ أَرَدۡنَآ إِلَّآ إِحۡسَٰنٗا وَتَوۡفِيقًا

Hali ya wanafiki hawa itakuwa namna gani, watakapofikiwa na misiba kwa sababu ya makosa yaliyotendwa na mikono yao kisha wakakujia, ewe Mtume, wakitoa udhuru na kukuhakikishia kwamba wao hawakuwa na malengo yoyote, kwa matendo yao hayo, isipokuwa ni kutenda wema na kuleta upatanishi baina ya wagomvi? info
التفاسير:

external-link copy
63 : 4

أُوْلَٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ يَعۡلَمُ ٱللَّهُ مَا فِي قُلُوبِهِمۡ فَأَعۡرِضۡ عَنۡهُمۡ وَعِظۡهُمۡ وَقُل لَّهُمۡ فِيٓ أَنفُسِهِمۡ قَوۡلَۢا بَلِيغٗا

Hao ndio ambao Mwenyezi Mungu Anaujua uhakika unafiki ulio ndani ya nyoyo zao. Basi jiepushe nao, uwaonye ubaya wa mambo waliyonayo na uwaambie maneno yenye kuwaathiri kwa njia ya kuwakemea. info
التفاسير:

external-link copy
64 : 4

وَمَآ أَرۡسَلۡنَا مِن رَّسُولٍ إِلَّا لِيُطَاعَ بِإِذۡنِ ٱللَّهِۚ وَلَوۡ أَنَّهُمۡ إِذ ظَّلَمُوٓاْ أَنفُسَهُمۡ جَآءُوكَ فَٱسۡتَغۡفَرُواْ ٱللَّهَ وَٱسۡتَغۡفَرَ لَهُمُ ٱلرَّسُولُ لَوَجَدُواْ ٱللَّهَ تَوَّابٗا رَّحِيمٗا

Hatukumtumiliza Mtume yoyote, miongoni mwa Mitume wetu, isipokuwa ni afuatwe kwa amri ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka na uamuzi Wake. Na lau kwamba hawa waliojidhulumu nafsi zao kwa kutenda mabaya, walikujia, ewe Mtume, katika uhai wako, hali ya kutubia na kumuomba Mwenyezi Mungu Awasamehe madhambi yao, nawe ukawaombea msamaha, wangalimkuta Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kukubali toba, ni Mwingi wa kurehemu. info
التفاسير:

external-link copy
65 : 4

فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤۡمِنُونَ حَتَّىٰ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيۡنَهُمۡ ثُمَّ لَا يَجِدُواْ فِيٓ أَنفُسِهِمۡ حَرَجٗا مِّمَّا قَضَيۡتَ وَيُسَلِّمُواْ تَسۡلِيمٗا

Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Anaapa kwa nafsi Yake tukufu, kwamba hawa hawataamini kikweli mpaka wakufanye wewe ni hakimu kwenye ugomvi unaotokea baina yao katika uhai wako na watake uamuzi wa Sunnah yako baada ya kufa kwako, kisha wasiingiwe na dhiki katika nafsi zao kwa matokeo ya hukumu yako, na wakwandame, pamoja na hivyo, kwa kukufuata kikamilifu. Kutoa uamuzi kulingana na aliyokuja nayo Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye, kutoka kwenye Qur’ani na Sunnah katika kila jambo katika mambo ya kimaisha, pamoja na kuridhika na kusalimu amri, ni miongoni mwa uthabiti Imani info
التفاسير: