Kur'an-ı Kerim meal tercümesi - Savahili Dilinde Tercüme - Abdullah Muhammed ve Nasır Hamiys

Sayfa numarası:close

external-link copy
7 : 4

لِّلرِّجَالِ نَصِيبٞ مِّمَّا تَرَكَ ٱلۡوَٰلِدَانِ وَٱلۡأَقۡرَبُونَ وَلِلنِّسَآءِ نَصِيبٞ مِّمَّا تَرَكَ ٱلۡوَٰلِدَانِ وَٱلۡأَقۡرَبُونَ مِمَّا قَلَّ مِنۡهُ أَوۡ كَثُرَۚ نَصِيبٗا مَّفۡرُوضٗا

Wanaume, wadogo na wakubwa, wana fungu lililopasishwa na Mwenyezi Mungu katika mali yalioachwa na wazazi wawili au jamaa wa karibu, yawe ni kidogo mali hayo au ni mengi, katika mafungu maalumu yaliyo wazi yaliyofaradhiwa na Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka na kushinda, kwa hawa wanaume na pia wanawake. info
التفاسير:

external-link copy
8 : 4

وَإِذَا حَضَرَ ٱلۡقِسۡمَةَ أُوْلُواْ ٱلۡقُرۡبَىٰ وَٱلۡيَتَٰمَىٰ وَٱلۡمَسَٰكِينُ فَٱرۡزُقُوهُم مِّنۡهُ وَقُولُواْ لَهُمۡ قَوۡلٗا مَّعۡرُوفٗا

Watakapohudhuria, kikao chakugawanywa urithi, jamaa wa maiti wa karibu wasiokuwa na haki ya kurithi au waliofiwa na baba zao nao ni wadogo au wasiokuwa na mali, basi wapeni chochote katika mali hayo, kwa njia ya kuwapumbaza, kabla mali hayajagawanywa kwa wenyewe. Na waambieni neno zuri lisilokuwa chafu wala baya. info
التفاسير:

external-link copy
9 : 4

وَلۡيَخۡشَ ٱلَّذِينَ لَوۡ تَرَكُواْ مِنۡ خَلۡفِهِمۡ ذُرِّيَّةٗ ضِعَٰفًا خَافُواْ عَلَيۡهِمۡ فَلۡيَتَّقُواْ ٱللَّهَ وَلۡيَقُولُواْ قَوۡلٗا سَدِيدًا

Na waogope wale ambao lau watakufa na wataacha nyuma yao watoto wadogo madhaifu, wakawachelea dhuluma na kupotea, basi na wamchunge Mwenyezi Mungu juu ya wale mayatima na wengineo walio chini ya mikono yao. Nako ni kuwahifadhia mali yao, kuwalea vizuri na kuwaondolea ya kuwaudhi. Na wawaambie maneno yanayolingana na usawa na wema. info
التفاسير:

external-link copy
10 : 4

إِنَّ ٱلَّذِينَ يَأۡكُلُونَ أَمۡوَٰلَ ٱلۡيَتَٰمَىٰ ظُلۡمًا إِنَّمَا يَأۡكُلُونَ فِي بُطُونِهِمۡ نَارٗاۖ وَسَيَصۡلَوۡنَ سَعِيرٗا

Wale wanaozifuja mali za mayatima wakawa wazichukua pasi na haki, hakika wanakula Moto utakaowaka matumboni mwao Siku ya Kiyama; wataungia Moto ambao watalisikia joto lake. info
التفاسير:

external-link copy
11 : 4

يُوصِيكُمُ ٱللَّهُ فِيٓ أَوۡلَٰدِكُمۡۖ لِلذَّكَرِ مِثۡلُ حَظِّ ٱلۡأُنثَيَيۡنِۚ فَإِن كُنَّ نِسَآءٗ فَوۡقَ ٱثۡنَتَيۡنِ فَلَهُنَّ ثُلُثَا مَا تَرَكَۖ وَإِن كَانَتۡ وَٰحِدَةٗ فَلَهَا ٱلنِّصۡفُۚ وَلِأَبَوَيۡهِ لِكُلِّ وَٰحِدٖ مِّنۡهُمَا ٱلسُّدُسُ مِمَّا تَرَكَ إِن كَانَ لَهُۥ وَلَدٞۚ فَإِن لَّمۡ يَكُن لَّهُۥ وَلَدٞ وَوَرِثَهُۥٓ أَبَوَاهُ فَلِأُمِّهِ ٱلثُّلُثُۚ فَإِن كَانَ لَهُۥٓ إِخۡوَةٞ فَلِأُمِّهِ ٱلسُّدُسُۚ مِنۢ بَعۡدِ وَصِيَّةٖ يُوصِي بِهَآ أَوۡ دَيۡنٍۗ ءَابَآؤُكُمۡ وَأَبۡنَآؤُكُمۡ لَا تَدۡرُونَ أَيُّهُمۡ أَقۡرَبُ لَكُمۡ نَفۡعٗاۚ فَرِيضَةٗ مِّنَ ٱللَّهِۗ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلِيمًا حَكِيمٗا

Mwenyezi Mungu Anawausia na kuwaamrisha, kuhusu wana wenu atakapokufa mmoja wenu na akaacha watoto wa kiume na wa kike, kwamba urithi wote ni wao: mtoto wa kiume atapata mfano wa fungu la watoto wawili wa kike, iwapo itakuwa hakuna mawarithi wengine isipokuwa ni wao tu. Iwapo atawaacha watoto wa kike peke yao, basi watoto wa kike wawili au zaidi watapata theluthi mbili ya alichokiacha.. Na iwapo mrithi ni binti mmoja, basi atapata nusu ya mali, na wazazi wawili wa maiti, kila mmoja atapata sudusi. Hii ni iwapo maiti ana mtoto wa kiume au wa kike, mmoja au zaidi. Iwapo maiti hana mwana, na wakawa mawarithi wake ni wazazi wake wawili, basi mamake atapata theluthi na babake atapata kilichosalia. Na iwapo maiti ana ndugu, wawili au zaidi, wawe ni wanawake au ni wanaume, basi mamake atapata sudusi, baba atapata kilichosalia na ndugu hawatapata kitu. Mgawanyo huu wa mali yalioachwa hufanyika baada ya kutoa wasia aliousia maiti katika kiwango cha theluthi, au baada ya kutoa deni adaiwalo. Baba zenu na watoto wenu ambao wamepangiwa kurithi, hamjui ni yupi katika wao mwenye manufaaa ya ukaribu zaidi na nyinyi katika dunia yenu na Akhera yenu. Kwa hivyo, msimfanye mmoja kati yao ni bora kuliko mwengine. Hili mliousiwa nalo limefaradhiwa kwenu na Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa viumbe Wake, ni Mwenye hekima katika Sheria Alizowaekea. info
التفاسير: