Përkthimi i kuptimeve të Kuranit Fisnik - Përkthimi suahilisht - Abdullah Muhammed dhe Nasir Khamis

Numri i faqes:close

external-link copy
196 : 7

إِنَّ وَلِـِّۧيَ ٱللَّهُ ٱلَّذِي نَزَّلَ ٱلۡكِتَٰبَۖ وَهُوَ يَتَوَلَّى ٱلصَّٰلِحِينَ

«Hakika mtegemewa wangu ni Mwenyezi Mungu Ambaye Anasimamia kunihifadhi na kunipa ushindi. Yeye Ndiye Ambaye Aliniteremshia Qur’ani kwa haki na Yeye Anawasimamia walio wema miongoni mwa waja wake na anawapa ushindi juu ya maadui zao na Haachi kuwasaidia.» info
التفاسير:

external-link copy
197 : 7

وَٱلَّذِينَ تَدۡعُونَ مِن دُونِهِۦ لَا يَسۡتَطِيعُونَ نَصۡرَكُمۡ وَلَآ أَنفُسَهُمۡ يَنصُرُونَ

Na wale waungu ambao nyinyi mnawaomba, enyi washirikina, badala ya Mwenyezi Mungu, hawawezi kuwanusuru nyinyi wala kuzinusuru nafsi zao. info
التفاسير:

external-link copy
198 : 7

وَإِن تَدۡعُوهُمۡ إِلَى ٱلۡهُدَىٰ لَا يَسۡمَعُواْۖ وَتَرَىٰهُمۡ يَنظُرُونَ إِلَيۡكَ وَهُمۡ لَا يُبۡصِرُونَ

Na iwapo mtawaita, enyi washirikina, hao waungu wenu kwenye kulingana sawa na haki hawatasikia mwito wenu. Na utawaona, ewe Mtume, waungu wa hawa washirikina miongoni mwa wenye kuabudu mizimu, wanakuelekea kama wanaokutazama na hali wao hawaoni kwa kuwa wao hawana macho wala busara. info
التفاسير:

external-link copy
199 : 7

خُذِ ٱلۡعَفۡوَ وَأۡمُرۡ بِٱلۡعُرۡفِ وَأَعۡرِضۡ عَنِ ٱلۡجَٰهِلِينَ

Kubali, ewe Nabii, wewe na wafuasi wako kiwango cha kati cha tabia za watu na vitendo vyao, wala usitake kutoka kwao mambo magumu ili wasije wakachukia; na amrisha kwa kila neno jema na kitendo kizuri; na jiepushe na kushindana na mafidhuli na usijisawazishe na wajinga wenye uchache wa akili. info
التفاسير:

external-link copy
200 : 7

وَإِمَّا يَنزَغَنَّكَ مِنَ ٱلشَّيۡطَٰنِ نَزۡغٞ فَٱسۡتَعِذۡ بِٱللَّهِۚ إِنَّهُۥ سَمِيعٌ عَلِيمٌ

Na iwapo utashikwa na hasira, ewe Nabii, zitokazo kwa Shetani au ukahisi, kutoka kwake, wasiwasi au ulegevu wa kufanya mema au himizo la kufanya ovu, basi tafuta himaya kwa Mola wako kwa kujilinda Kwake. Kwani Yeye ni Msikizi wa kila neno ni Mjuzi wa kila kitendo. info
التفاسير:

external-link copy
201 : 7

إِنَّ ٱلَّذِينَ ٱتَّقَوۡاْ إِذَا مَسَّهُمۡ طَٰٓئِفٞ مِّنَ ٱلشَّيۡطَٰنِ تَذَكَّرُواْ فَإِذَا هُم مُّبۡصِرُونَ

Hakika wale wanaomcha Mwenyezi Mungu miongoni mwa viumbe wake, kwa kuogopa mateso Yake kwa kuzitekeleza faradhi Zake na kuyaepuka makatazo Yake, likiwapata tukio lolote la wasiwasi wa Shetani, wanayakumbuka yale Aliyowalazimisha Mwenyezi Mungu juu yao ya kumtii na kutubia Kwake, na punde si punde wanakomeka na kumuasi Mwenyezi Mungu wakiwa kwenye hoja ya wazi, wenye kufuata amri ya Mwenyezi Mungu na wenye kumuasi Shetani. info
التفاسير:

external-link copy
202 : 7

وَإِخۡوَٰنُهُمۡ يَمُدُّونَهُمۡ فِي ٱلۡغَيِّ ثُمَّ لَا يُقۡصِرُونَ

Na ndugu wa mashetani, nao ni wapotofu miongoni mwa wapotevu wa wanadamu ambao mashetani wanawasukuma kwenye upotevu na upotofu. Na mashetani wa kijini hawaachi nafasi iwapite katika kuwasukuma kwao mashetani wa kibinadamu kwenye upotofu. Na mashetani wa kibinadamu hawaachi nafasi iwapite katika kuyafanya yale ambayo mashetani wa kijini wanayafanyia ushawishi. info
التفاسير:

external-link copy
203 : 7

وَإِذَا لَمۡ تَأۡتِهِم بِـَٔايَةٖ قَالُواْ لَوۡلَا ٱجۡتَبَيۡتَهَاۚ قُلۡ إِنَّمَآ أَتَّبِعُ مَا يُوحَىٰٓ إِلَيَّ مِن رَّبِّيۚ هَٰذَا بَصَآئِرُ مِن رَّبِّكُمۡ وَهُدٗى وَرَحۡمَةٞ لِّقَوۡمٖ يُؤۡمِنُونَ

Na usipowajia, ewe Mtume, washirikina hawa na aya wanasema, «Si uitunge na uizue wewe mwenyewe.» Waambie, ewe Mtume, «Hili si langu, na haifai kwangu mimi nilifanye. Kwa kuwa Mwenyezi Mungu Ameniamuru kufuata wahyi nilioletewa kutoka Kwake. Nao ni hii Qur’ani ninayowasomea, inayokusanya hoja na dalili zinazotoka kwa Mola wenu na yenye ufafanuzi, inayoongoza Waumini kwenye njia iliyolingana sawa, na ni rehema ambayo kwayo Mwenyezi Mungu Anawarehemu waja Wake Waumini. info
التفاسير:

external-link copy
204 : 7

وَإِذَا قُرِئَ ٱلۡقُرۡءَانُ فَٱسۡتَمِعُواْ لَهُۥ وَأَنصِتُواْ لَعَلَّكُمۡ تُرۡحَمُونَ

Na isomwapo Qur’ani isikilizeni, enyi watu, na mnyamaze ili muielewe kwa matarajio kwamba Mwenyezi Mungu Awarehamu kwayo. info
التفاسير:

external-link copy
205 : 7

وَٱذۡكُر رَّبَّكَ فِي نَفۡسِكَ تَضَرُّعٗا وَخِيفَةٗ وَدُونَ ٱلۡجَهۡرِ مِنَ ٱلۡقَوۡلِ بِٱلۡغُدُوِّ وَٱلۡأٓصَالِ وَلَا تَكُن مِّنَ ٱلۡغَٰفِلِينَ

Na mtaje Mola wako, ewe Mtume, ndani ya nafsi yako kwa kumnyenyekea Mwenyezi Mungu na kumdhalilikia, hali ya kumcha Yeye moyoni, na umuombe kwa namna ya kati na kati baina ya kutoa sauti na kuifanya chini, katika mwanzo wa mchana na mwisho wake, na usiwe ni miongoni mwa wenye kughafilika kumtaja Mwenyezi Mungu na kupumbaa katika nyakati zao zinginezo. info
التفاسير:

external-link copy
206 : 7

إِنَّ ٱلَّذِينَ عِندَ رَبِّكَ لَا يَسۡتَكۡبِرُونَ عَنۡ عِبَادَتِهِۦ وَيُسَبِّحُونَهُۥ وَلَهُۥ يَسۡجُدُونَۤ۩

Hakika wale waliyoko mbele ya Mola Wako miongoni mwa Malaika hawafanyi kiburi kwa kuacha kumuabudu Mwenyezi Mungu, bali wao wanaandama amri Zake, wanamtakasa mchana na usiku na wanamwepusha na mambo yasiyonasibiana na Yeye, na Yeye Peke Yake wanamsujudia. info
التفاسير: