Përkthimi i kuptimeve të Kuranit Fisnik - Përkthimi suahilisht - Abdullah Muhammed dhe Nasir Khamis

Al-A'raf

external-link copy
1 : 7

الٓمٓصٓ

«Alif, Lām, Mīm, Ṣād.» Yametangulia maneno kuhusu herufi zilizokatwa na kutengwa mwanzo wa sura ya Al-Baqarah. info
التفاسير:

external-link copy
2 : 7

كِتَٰبٌ أُنزِلَ إِلَيۡكَ فَلَا يَكُن فِي صَدۡرِكَ حَرَجٞ مِّنۡهُ لِتُنذِرَ بِهِۦ وَذِكۡرَىٰ لِلۡمُؤۡمِنِينَ

Hii Qur’ani ni Kitabu kitukufu, Mwenyezi Mungu Amekiteremsha kwako, ewe Mtume. Basi pasiwe na shaka katika kifua chako kwamaba imeteremshwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Na usiwe na wasiwasi katika kuifikisha kwa watu na kuwaonya nayo. Tumeiteremsha kwako ili uwatishe nayo makafiri na uwakumbushe Waumini. info
التفاسير:

external-link copy
3 : 7

ٱتَّبِعُواْ مَآ أُنزِلَ إِلَيۡكُم مِّن رَّبِّكُمۡ وَلَا تَتَّبِعُواْ مِن دُونِهِۦٓ أَوۡلِيَآءَۗ قَلِيلٗا مَّا تَذَكَّرُونَ

Yafuateni, enyi watu, hayo yaliyoteremshwa kutoka kwa Mola wenu miongoni mwa Qur’ani na Sunnah(mafundisho ya Mtume) kwa kufuata maamrisho na kuepuka makatazo Na wala msiwafuate wategemewa badala ya Mwenyezi Mungu, kama mashetani na wasomi wa Kiyahudi na watawa wa Kinaswara. Hakika nyinyi ni mara chache mnapowaidhika na kuzingatia na mkarudi kwenye haki. info
التفاسير:

external-link copy
4 : 7

وَكَم مِّن قَرۡيَةٍ أَهۡلَكۡنَٰهَا فَجَآءَهَا بَأۡسُنَا بَيَٰتًا أَوۡ هُمۡ قَآئِلُونَ

Na miji mingi tuliwaangamiza watu wake kwa sababu ya kwenda kinyume kwao na Mitume wetu na kuwakanusha. Hilo likawaletea utwevu wa duniani uliounganishwa na unyonge wa Akhera. Basi adhabu yetu iliwajia, wakati mwingine wakiwa wamelala usiku, na wakati mwingine wakiwa wamelala mchana. Mwenyezi Mungu Amezihusu nyakati mbili hizi kwa kuwa ni nyakati za utulivu na mapumziko. Hivyo basi, kuja kwa adhabu kwenye nyakati mbili hizi kunababaisha zaidi na adhabu yenyewe huwa ni kali zaidi. info
التفاسير:

external-link copy
5 : 7

فَمَا كَانَ دَعۡوَىٰهُمۡ إِذۡ جَآءَهُم بَأۡسُنَآ إِلَّآ أَن قَالُوٓاْ إِنَّا كُنَّا ظَٰلِمِينَ

Basi hawakuwa na neno la kunena ilipoteremka adhabu isipokuwa ni kukubali kwao kwamba walifanya madhambi na walikosea na kwamaba wao wanastahili kupata adhabu iliyowashukia. info
التفاسير:

external-link copy
6 : 7

فَلَنَسۡـَٔلَنَّ ٱلَّذِينَ أُرۡسِلَ إِلَيۡهِمۡ وَلَنَسۡـَٔلَنَّ ٱلۡمُرۡسَلِينَ

Basi tutawauliza, tena tutawauliza, wale watu waliopelekewa Mitume, «Mliwajibu vipi Mitume wetu?» Na tutawauliza, tene tutawauliza, wale Mitume kuhusu kuufikisha kwao ujumbe wa Mola wao na namna walivyojibiwa na wale watu waliotumwa kwao. info
التفاسير:

external-link copy
7 : 7

فَلَنَقُصَّنَّ عَلَيۡهِم بِعِلۡمٖۖ وَمَا كُنَّا غَآئِبِينَ

Tutawaelezea, tena tutawaelezea, viumbe wote yale waliyoyatenda, kutokana na ujuzi wetu wa vitendo vyao ulimwenguni katika yale tuliyowaamrisha na tuliyowakataza. Na wala hatukwa mbali na wao katika hali yoyote ile. info
التفاسير:

external-link copy
8 : 7

وَٱلۡوَزۡنُ يَوۡمَئِذٍ ٱلۡحَقُّۚ فَمَن ثَقُلَتۡ مَوَٰزِينُهُۥ فَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡمُفۡلِحُونَ

Na kuvipima vitendo vya watu Siku ya Kiyama kutakuwa ni kwa mizani ya kikweli, kwa usawa na uhaki ambao hauna maonevu. Basi yoyote yule ambaye mizani za vitendo vyake zitakuwa nzito, kwa wingi wa mema yake, hao ndio watakaofaulu. info
التفاسير:

external-link copy
9 : 7

وَمَنۡ خَفَّتۡ مَوَٰزِينُهُۥ فَأُوْلَٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ خَسِرُوٓاْ أَنفُسَهُم بِمَا كَانُواْ بِـَٔايَٰتِنَا يَظۡلِمُونَ

Na yoyote yule ambaye mizani za vitendo vyake zitakuwa nyepesi, kwa wingi wa maovu yake, hao ndio waliopoteza bahati yao ya kupata radhi ya Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, kwa sababu ya kukiuka kwao mipaka kwa kuzikanusha aya za Mwenyezi Mungu , Aliyetukuka, na kukosa kuzifuata. info
التفاسير:

external-link copy
10 : 7

وَلَقَدۡ مَكَّنَّٰكُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَجَعَلۡنَا لَكُمۡ فِيهَا مَعَٰيِشَۗ قَلِيلٗا مَّا تَشۡكُرُونَ

Kwa hakika tumewapa utulivu, enyi watu, katika ardhi, na tumewaekea humo vitu mtakavyovitumia katika maisha yenu miongoni mwa vyakula na vinywaji; na pamoja na hayo, shukrani zenu juu ya neema za Mola wenu ni chache. info
التفاسير:

external-link copy
11 : 7

وَلَقَدۡ خَلَقۡنَٰكُمۡ ثُمَّ صَوَّرۡنَٰكُمۡ ثُمَّ قُلۡنَا لِلۡمَلَٰٓئِكَةِ ٱسۡجُدُواْ لِأٓدَمَ فَسَجَدُوٓاْ إِلَّآ إِبۡلِيسَ لَمۡ يَكُن مِّنَ ٱلسَّٰجِدِينَ

Na kwa hakika, tumwaneemesha nyinyi kwa kumuumba chanzo chenu - naye ni baba yenu Ādam- kutokana na kutokuwako kamwe, kisha tukamtia sura ya umbo lake lililo bora kuliko lile la viumbe wengi. Kisha tuliwaamuru Malaika wetu, amani iwashukie, wamsujudie kwa ajili ya kumtukuza na kumuheshimu na kuonyesha ubora wa Ādam. Nao wakamsujudia wote, isipokuwa Iblisi, ambaye alikuwa pamoja na wao, hakuwa ni miongoni mwa wenye kumsujudia Ādam kwa kumuhusudu kwa heshima hii kubwa aliyopewa. info
التفاسير: