Vertaling van de betekenissen Edele Qur'an - De Swahili vertaling - Ali Mohsen Al-Barwani

At-Tawbah

external-link copy
1 : 9

بَرَآءَةٞ مِّنَ ٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦٓ إِلَى ٱلَّذِينَ عَٰهَدتُّم مِّنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ

Huku ni kujitoa Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwenye jukumu la maagano na mlio ahidiana nao katika washirikina. info

Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanajitoa katika dhima, wala jukumu lolote, na wale washirikina mlio peana nao ahadi, na wao wakavunja hayo mlio ahidiana nao.

التفاسير:

external-link copy
2 : 9

فَسِيحُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ أَرۡبَعَةَ أَشۡهُرٖ وَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّكُمۡ غَيۡرُ مُعۡجِزِي ٱللَّهِ وَأَنَّ ٱللَّهَ مُخۡزِي ٱلۡكَٰفِرِينَ

Basi tembeeni katika nchi miezi mine, na jueni kwamba nyinyi hamwezi kumshinda Mwenyezi Mungu, na kwamba Mwenyezi Mungu ndiye anaye wahizi makafiri. info

Basi nyinyi washirikina, mna amani kwa muda wa miezi mine, kuanzia tangazo hili, mzunguke mtakako katika muda huu. Lakini jueni kuwa popote mlipo nyinyi mko chini ya utawala wa Mwenyezi Mungu, na nyinyi hamuwezi kumshinda Yeye. Na mjue kuwa Mwenyezi Mungu amewaandikia hizaya iwapate hao wanao pinga.

التفاسير:

external-link copy
3 : 9

وَأَذَٰنٞ مِّنَ ٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦٓ إِلَى ٱلنَّاسِ يَوۡمَ ٱلۡحَجِّ ٱلۡأَكۡبَرِ أَنَّ ٱللَّهَ بَرِيٓءٞ مِّنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ وَرَسُولُهُۥۚ فَإِن تُبۡتُمۡ فَهُوَ خَيۡرٞ لَّكُمۡۖ وَإِن تَوَلَّيۡتُمۡ فَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّكُمۡ غَيۡرُ مُعۡجِزِي ٱللَّهِۗ وَبَشِّرِ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ بِعَذَابٍ أَلِيمٍ

Na ni tangazo kutokana na Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa wote siku ya Hija Kubwa kwamba Mwenyezi Mungu na Mtume wake hawana jukumu lolote kwa washirikina. Basi mkitubu itakuwa kheri kwenu, na mkigeuka basi jueni kuwa nyinyi hamumshindi Mwenyezi Mungu. Na wabashirie makafiri kuwa watapata adhabu chungu. info

Na hili ni Tangazo linalo toka kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake kuwatangazia watu wote wanapo jumuika siku ya Hija Kubwa ya kwamba:- Hakika Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanajitoa katika dhima, au jukumu, yoyote katika mapatano na washirikina walio fanya khiana. Basi enyi washirikina, mlio vunja ahadi! Mkirudi mkaacha kumshirikisha Mwenyezi Mungu, itakuwa kheri kwenu hapa duniani na kesho Akhera. Lakini mkipuuza na mkabakia hivyo hivyo mlivyo, basi jueni kuwa nyinyi mngali chini ya utawala wa Mwenyezi Mungu. Ewe Mtume! Waonye makafiri wote kuwa ipo adhabu kali yenye uchungu.

التفاسير:

external-link copy
4 : 9

إِلَّا ٱلَّذِينَ عَٰهَدتُّم مِّنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ ثُمَّ لَمۡ يَنقُصُوكُمۡ شَيۡـٔٗا وَلَمۡ يُظَٰهِرُواْ عَلَيۡكُمۡ أَحَدٗا فَأَتِمُّوٓاْ إِلَيۡهِمۡ عَهۡدَهُمۡ إِلَىٰ مُدَّتِهِمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ يُحِبُّ ٱلۡمُتَّقِينَ

Isipo kuwa washirikina ambao mliahidiana nao kisha wasikupunguzieni chochote, wala hawakumsaidia yeyote dhidi yenu, basi hao watimizieni ahadi yao mpaka muda wao. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wacha-Mungu. info

Ama wale washirikina mlio ahidiana nao na wakatimiza ahadi zao, wala hawakuacha chochote katika hayo, wala hawakumsaidia yeyote dhidi yenu, basi watimizieni ahadi zao mpaka mwisho na mzihishimu...Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wacha-Mungu wenye kutimiza ahadi zao.

التفاسير:

external-link copy
5 : 9

فَإِذَا ٱنسَلَخَ ٱلۡأَشۡهُرُ ٱلۡحُرُمُ فَٱقۡتُلُواْ ٱلۡمُشۡرِكِينَ حَيۡثُ وَجَدتُّمُوهُمۡ وَخُذُوهُمۡ وَٱحۡصُرُوهُمۡ وَٱقۡعُدُواْ لَهُمۡ كُلَّ مَرۡصَدٖۚ فَإِن تَابُواْ وَأَقَامُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتَوُاْ ٱلزَّكَوٰةَ فَخَلُّواْ سَبِيلَهُمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٞ

Na ikisha miezi mitukufu basi wauweni washirikina popote mwakutapo, na washikeni na wazungukeni, na wavizieni katika kila njia. Lakini wakitubu, wakashika Sala, na wakatoa Zaka, basi waachilieni. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu. info

Ukimalizika muda wa amani, yaani miezi mine, basi wauweni washirikina walio vunja ahadi katika kila pahala. Na watieni nguvuni, wazungukeni kwa kuwafungia njia, na wavizieni katika kila njia. Wakitubu wakaacha ukafiri wao, na wakafuata hukumu za Uislamu, kwa kushika Swala, na kutoa Zaka, basi nyinyi hamna sababu ya kuwashambulia, kwa kuwa wamekwisha ingia katika Dini ya Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mkubwa wa Kusamehe kwa anaye tubu, na Mwenye rehema kunjufu kwa waja wake.

التفاسير:

external-link copy
6 : 9

وَإِنۡ أَحَدٞ مِّنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ ٱسۡتَجَارَكَ فَأَجِرۡهُ حَتَّىٰ يَسۡمَعَ كَلَٰمَ ٱللَّهِ ثُمَّ أَبۡلِغۡهُ مَأۡمَنَهُۥۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمۡ قَوۡمٞ لَّا يَعۡلَمُونَ

Na ikiwa mmoja wapo katika washirikina akikuomba ulinzi, basi mpe ulinzi apate kusikia maneno ya Mwenyezi Mungu. Kisha mfikishe pahala pake pa amani. Haya ni kwa kuwa hao ni watu wasiojua kitu. info

Ewe Mtume! Mmoja wapo katika washirikina ulio amrishwa uwapige vita, akikutaka amani ili apate kusikia wito wako, basi mpe amani mpaka asikie maneno ya Mwenyezi Mungu. Akiingia katika Uislamu basi huyo ni mwenzenu. Na akitoingia mpeleke mpaka afike pahala pa amani kwake. Na haya ya kumpa ulinzi na amani mwenye kuomba ili asikie maneno ya Mwenyezi Mungu ni kwa sababu ya ule ujinga wake wa kutoujua Uislamu ulio kwisha dhihiri, na ile hamu yake ya kutaka kuujua.

التفاسير: