Ewe mwanaadamu! Kitu gani kilicho kukhadaa wewe na Mola wako Mlezi Mtukufu hata ukafanya jeuri ya kwenda kumuasi? (Ni dhaahiri kuwa Sayyid Abdulla bin Ali bin Nassir aliye tunga utenzi wa Kiswahili maarufu uitwao Al Inkishaf aliiwaza Aya hii alipo tunga ubeti huu: Moyo wangu nini huzundukani Likughurielo hela ni nni? Hunelezi nami kalibaini Liwapo na sura nisikataye )
Siku ambayo nafsi haitakuwa na mamlaka yoyote juu ya nafsi ya kuifaa au kuidhuru; na amri yote siku hiyo itakuwa ni ya Mwenyezi Mungu peke yake!