ترجمة معاني القرآن الكريم - الترجمة السواحلية - علي محسن البرواني

سورة الإنفطار - Al-Infitar

external-link copy
1 : 82

إِذَا ٱلسَّمَآءُ ٱنفَطَرَتۡ

Mbingu itapo chanika! info

Itakapo pasuka mbingu,

التفاسير:

external-link copy
2 : 82

وَإِذَا ٱلۡكَوَاكِبُ ٱنتَثَرَتۡ

Na nyota zitapo tawanyika! info

Na nyota zitakapo pukutika na kutawanyika,

التفاسير:

external-link copy
3 : 82

وَإِذَا ٱلۡبِحَارُ فُجِّرَتۡ

Na bahari zitakapo pasuliwa! info

Na bahari zikafurika na kuingiliana kwa kuondoka viziwizi baina yao,

التفاسير:

external-link copy
4 : 82

وَإِذَا ٱلۡقُبُورُ بُعۡثِرَتۡ

Na makaburi yatapo fukuliwa! info

Na makaburi yakafunuliwa na wakatoka maiti walio kuwamo,

التفاسير:

external-link copy
5 : 82

عَلِمَتۡ نَفۡسٞ مَّا قَدَّمَتۡ وَأَخَّرَتۡ

Hapo kila nafsi itajua ilicho tanguliza, na ilicho bakisha nyuma. info

Hapo basi kila nafsi itajua nini kheri au shari iliyo tanguliza na iliyo chelewesha.

التفاسير:

external-link copy
6 : 82

يَٰٓأَيُّهَا ٱلۡإِنسَٰنُ مَا غَرَّكَ بِرَبِّكَ ٱلۡكَرِيمِ

Ewe mwanaadamu! Nini kilicho kughuri ukamwacha Mola wako Mlezi Mtukufu? info

Ewe mwanaadamu! Kitu gani kilicho kukhadaa wewe na Mola wako Mlezi Mtukufu hata ukafanya jeuri ya kwenda kumuasi? (Ni dhaahiri kuwa Sayyid Abdulla bin Ali bin Nassir aliye tunga utenzi wa Kiswahili maarufu uitwao Al Inkishaf aliiwaza Aya hii alipo tunga ubeti huu: Moyo wangu nini huzundukani Likughurielo hela ni nni? Hunelezi nami kalibaini Liwapo na sura nisikataye )

التفاسير:

external-link copy
7 : 82

ٱلَّذِي خَلَقَكَ فَسَوَّىٰكَ فَعَدَلَكَ

Aliye kuumba, akakuweka sawa, akakunyoosha! info

Mungu wako huyo ndiye aliye kuumba nawe hukuwa chochote, akakuumba na viungo vya kukuletea manufaa, akakufanya umenyooka kwa umbo sawa sawa.

التفاسير:

external-link copy
8 : 82

فِيٓ أَيِّ صُورَةٖ مَّا شَآءَ رَكَّبَكَ

Katika sura yoyote aliyo ipenda akakujenga. info

Akakujenga na akakuleta katika sura yoyote aliyo itaka.

التفاسير:

external-link copy
9 : 82

كَلَّا بَلۡ تُكَذِّبُونَ بِٱلدِّينِ

Sivyo hivyo! Bali nyinyi mnaikanusha Siku ya Malipo. info

Hamwachi? Bali nyinyi mnakadhibisha malipo ya Siku ya Kiyama!

التفاسير:

external-link copy
10 : 82

وَإِنَّ عَلَيۡكُمۡ لَحَٰفِظِينَ

Na hakika bila ya shaka wapo walinzi juu yenu, info

Na hakika wapo juu yenu Malaika walinzi, ambao ni waheshimiwa kwetu,

التفاسير:

external-link copy
11 : 82

كِرَامٗا كَٰتِبِينَ

Waandishi wenye hishima, info

Wanasajili vitendo vyenu vyote mvitendavyo, vya kheri na shari.

التفاسير:

external-link copy
12 : 82

يَعۡلَمُونَ مَا تَفۡعَلُونَ

Wanayajua mnayo yatenda. info

Wanayajua mnayo yafanya ya kheri na ya shari

التفاسير:

external-link copy
13 : 82

إِنَّ ٱلۡأَبۡرَارَ لَفِي نَعِيمٖ

Hakika wema bila ya shaka watakuwa katika neema, info

Hakika wale walio ni wa kweli katika Imani yao wapo katika neema kubwa.

التفاسير:

external-link copy
14 : 82

وَإِنَّ ٱلۡفُجَّارَ لَفِي جَحِيمٖ

Na hakika waovu bila ya shaka watakuwa Motoni; info

Na hakika walio iacha amri ya Mwenyezi bila ya shaka watakuwa katika Moto unao unguza,

التفاسير:

external-link copy
15 : 82

يَصۡلَوۡنَهَا يَوۡمَ ٱلدِّينِ

Wataingia humo Siku ya Malipo. info

Wataingia humo Siku ya Malipo.

التفاسير:

external-link copy
16 : 82

وَمَا هُمۡ عَنۡهَا بِغَآئِبِينَ

Na hawatoacha kuwamo humo. info

Na wala hawatatoka katika Jahannamu!

التفاسير:

external-link copy
17 : 82

وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا يَوۡمُ ٱلدِّينِ

Na nini kitakacho kujuulisha Siku ya Malipo ni siku gani? info

Na nini kitakujuvya ni nini hiyo Siku ya Malipo, na mambo yake yamepindukia ujuzi wako na fikra zako?

التفاسير:

external-link copy
18 : 82

ثُمَّ مَآ أَدۡرَىٰكَ مَا يَوۡمُ ٱلدِّينِ

Tena nini kitakacho kujuulisha Siku ya Malipo ni siku gani? info

Tena ni nini kitacho kujuvya ni nini hiyo Siku ya Malipo kwa vitisho vyake na shida zake?

التفاسير:

external-link copy
19 : 82

يَوۡمَ لَا تَمۡلِكُ نَفۡسٞ لِّنَفۡسٖ شَيۡـٔٗاۖ وَٱلۡأَمۡرُ يَوۡمَئِذٖ لِّلَّهِ

Siku ambayo nafsi haitakuwa na madaraka yoyote juu ya nafsi; na amri yote siku hiyo ni ya Mwenyezi Mungu tu. info

Siku ambayo nafsi haitakuwa na mamlaka yoyote juu ya nafsi ya kuifaa au kuidhuru; na amri yote siku hiyo itakuwa ni ya Mwenyezi Mungu peke yake!

التفاسير: