Vertaling van de betekenissen Edele Qur'an - De Swahili vertaling - Ali Mohsen Al-Barwani

Pagina nummer:close

external-link copy
70 : 2

قَالُواْ ٱدۡعُ لَنَا رَبَّكَ يُبَيِّن لَّنَا مَا هِيَ إِنَّ ٱلۡبَقَرَ تَشَٰبَهَ عَلَيۡنَا وَإِنَّآ إِن شَآءَ ٱللَّهُ لَمُهۡتَدُونَ

Wakasema: Tuombee kwa Mola wako Mlezi atupambanulie ni yupi? Hakika tunaona ng'ombe wamefanana. Na kwa yakini, Inshaallah, Mwenyezi Mungu akipenda, tutaongoka. info

Tena wakashikilia kuuliza kwao, wakasema: Tuombee kwa Mola wako Mlezi atupambanulie khasa huyo ni yupi? Kwani ng'ombe wanatudanganyikia sisi, hatujui. Na Inshallah, Mwenyezi Mungu akipenda, sisi tutaongokewa tumjue.

التفاسير:

external-link copy
71 : 2

قَالَ إِنَّهُۥ يَقُولُ إِنَّهَا بَقَرَةٞ لَّا ذَلُولٞ تُثِيرُ ٱلۡأَرۡضَ وَلَا تَسۡقِي ٱلۡحَرۡثَ مُسَلَّمَةٞ لَّا شِيَةَ فِيهَاۚ قَالُواْ ٱلۡـَٰٔنَ جِئۡتَ بِٱلۡحَقِّۚ فَذَبَحُوهَا وَمَا كَادُواْ يَفۡعَلُونَ

Akasema: Yeye anasema: Kuwa huyo ni Ng'ombe asiye tiwa kazini kulima Ardhi wala kumwagia maji mimea, mzima, hana baka. Wakasema: Sasa umeleta haki. Basi wakamchinja, na walikaribia kuwa wasifanye hayo. info

Musa akawambia: Mwenyezi Mungu anasema kuwa Ng'ombe huyo bado hajatiwa kazini kwa kulima wala kumwagia maji shambani kwa ajili ya makulima. Naye hana ila yoyote, mzima kabisa, wala katika mwili wake hana kibaka chochote, wote ni wa rangi moja. Hapo tena wakamwambia: Sasa umepambanua vilivyo. Wakamtafuta Ng'ombe mwenye sifa hizo wakamchinja. Na walikuwa wamekaribia wasifanye hayo kwa kukithiri masuala yao na wingi wa kushikilia kwao.

التفاسير:

external-link copy
72 : 2

وَإِذۡ قَتَلۡتُمۡ نَفۡسٗا فَٱدَّٰرَٰءۡتُمۡ فِيهَاۖ وَٱللَّهُ مُخۡرِجٞ مَّا كُنتُمۡ تَكۡتُمُونَ

Na mlipo muuwa mtu, kisha mkakhitalifiana kwayo, na Mwenyezi Mungu ni mwenye kuyatoa hayo mliyo kuwa mkiyaficha. info

Na kumbukeni siku mlipo muuwa mtu, mkakhasimiana wenyewe kwa wenyewe, mkautetea ukhalifu, mkawa mkituhumiana kwa mauwaji, na hali Mwenyezi Mungu anaijua hakika, na ataikashifu na kuidhihirisha juu ya kuificha kwenu.

التفاسير:

external-link copy
73 : 2

فَقُلۡنَا ٱضۡرِبُوهُ بِبَعۡضِهَاۚ كَذَٰلِكَ يُحۡيِ ٱللَّهُ ٱلۡمَوۡتَىٰ وَيُرِيكُمۡ ءَايَٰتِهِۦ لَعَلَّكُمۡ تَعۡقِلُونَ

Tukasema: Mpigeni kwa kipande chake (huyo Ng'ombe). Ndivyo hivi Mwenyezi Mungu huwahuisha wafu; na anakuonyesheni Ishara zake ili mpate kufahamu. info

Tukakwambieni kwa ulimi wa Musa: Chukueni kipande cha nyama ya huyo Ng'ombe mumpige nacho, nanyi mkafanya hivyo. Mwenyezi Mungu akamfufua huyo aliye uliwa akataja jina la aliye muuwa, na kisha akafa tena. Na huo ulikuwa ni muujiza wa Mwenyezi Mungu kwa ajili ya Musa. Kwani Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu, na kwa uwezo wake huu ndivyo anavyo huisha maiti Siku ya Kiama. Na anakuonyesheni dalili za uwezo wake ili mpate kufahamu na kuzingatia haya. Mwandishi mmoja wa zama zetu, marehemu Sh. Abdul Wahhab Annajjar ametaja kwamba kauli ya Mwenyezi Mungu: "Mpigeni kwa kipande chake" maana yake kipande cha aliye uwawa. Na makusudio ya kufufuka kwake ni kumtolea kisasi, kwa kuwa kupigwa kwa kiungo cha mwenye kuuliwa humpelekea muuwaji kuungama, na mara nyingi kumwona tu aliye uwawa humpelekea mwenye kuuwa kuungama. Na inakuwa kisa hichi ni mbali na lile jambo la kuchinja, na kuamrisha Mwenyezi Mungu Mtukufu kuchinja; na kwamba kuamrisha Mwenyezi Mungu Mtukufu wamchinje Ng'ombe ni kwa ajili ya kumla. Na katika haya pana mafunzo ya nafsi kwao, kwani hawa walikuwa pamoja na Wamisri ambao wakimwona Ng'ombe ni mtakatifu, na yalikuwa kwao mabaki ya haya ya kumtukuza Ng'ombe kwa dalili ya kuwa waliabudu sanamu la ndama baada ya hayo. Ikawa hapana budi kung'oa mabaki yake katika nafsi zao kwa kuwalazimisha kumchinja Ng'ombe. Ndio ikawa ile amri ya kuchinja, na yakatokea majadiliano na kukawa kule kusitasita kwao, na mwisho wakamchinja, na walikaribia wasichinje.

التفاسير:

external-link copy
74 : 2

ثُمَّ قَسَتۡ قُلُوبُكُم مِّنۢ بَعۡدِ ذَٰلِكَ فَهِيَ كَٱلۡحِجَارَةِ أَوۡ أَشَدُّ قَسۡوَةٗۚ وَإِنَّ مِنَ ٱلۡحِجَارَةِ لَمَا يَتَفَجَّرُ مِنۡهُ ٱلۡأَنۡهَٰرُۚ وَإِنَّ مِنۡهَا لَمَا يَشَّقَّقُ فَيَخۡرُجُ مِنۡهُ ٱلۡمَآءُۚ وَإِنَّ مِنۡهَا لَمَا يَهۡبِطُ مِنۡ خَشۡيَةِ ٱللَّهِۗ وَمَا ٱللَّهُ بِغَٰفِلٍ عَمَّا تَعۡمَلُونَ

Kisha nyoyo zenu zikawa ngumu baada ya hayo, hata zikawa kama mawe au ngumu zaidi; kwani kuna mawe yanayo timbuka mito, na kuna mengine yanayo pasuka yakatoka maji ndani yake, na kuna mengine huanguka kwa sababu ya khofu ya Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na mnayo yafanya. info

Tena nyinyi baada ya miujiza na ishara hizi zote hamkukubali wala hamkunyooka, wala nyoyo zenu hazikulainika na kunyenyekea. Bali zikawa zimekacha na ngumu, na zikabakia vile vile na ugumu wake na ushupavu wake, kama jiwe gumu katika ule ukakamavu wake, bali hizo nyoyo zenu zimeshinda jiwe kwa ugumu. Kwani yapo mawe yanayo athirika na kulainika. Yapo mawe yanayo timbuka maji yakawa mito, na yapo mawe yanayo pasuka na yakatoka maji kama chemchem, na yapo mawe kwa uwezo wa Mwenyezi yanayo nyenyekea kufuata mapenzi ya Mwenyezi Mungu yakaporomoka kutoka juu ya milima kama apendavyo Mwenyezi Mungu Mtukufu. Ama hizo nyoyo zenu,nyinyi Mayahudi, haziathiriki wala hazilainiki. Ole wenu kwa hayo! Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na vitendo vyenu, naye atakupeni adhabu kwa namna mbali mbali za adhabu, ikiwa hamtoshukuru kwa neema mlizo pewa.

التفاسير:

external-link copy
75 : 2

۞ أَفَتَطۡمَعُونَ أَن يُؤۡمِنُواْ لَكُمۡ وَقَدۡ كَانَ فَرِيقٞ مِّنۡهُمۡ يَسۡمَعُونَ كَلَٰمَ ٱللَّهِ ثُمَّ يُحَرِّفُونَهُۥ مِنۢ بَعۡدِ مَا عَقَلُوهُ وَهُمۡ يَعۡلَمُونَ

Mnatumai watakuaminini na hali baadhi yao walikuwa wakisikia maneno ya Mwenyezi Mungu, kisha wakayabadili baada ya kuwa wameyafahamu, na hali wanajua? info

Haikufaliini enyi Waumini kutumai ya kuwa Mayahudi wataiamini Dini yenu na wakufuateni nyinyi, na ilhali katika makundi yao mbali mbali zimekusanyika sifa mbovu zinazo waweka mbali na kuiamini Haki. Walikuwapo baadhi miongoni mwao (nao ni wale Makohani) walio kuwa wakiyasikia maneno ya Mwenyezi Mungu katika Taurati, na wakiyafahamu vilivyo, kisha makusudi wakiyageuza na hali wanajua kuwa ni kweli, na kuwa vitabu vya Mwenyezi Mungu vilivyo teremshwa haijuzu kuvigeuza.

التفاسير:

external-link copy
76 : 2

وَإِذَا لَقُواْ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ قَالُوٓاْ ءَامَنَّا وَإِذَا خَلَا بَعۡضُهُمۡ إِلَىٰ بَعۡضٖ قَالُوٓاْ أَتُحَدِّثُونَهُم بِمَا فَتَحَ ٱللَّهُ عَلَيۡكُمۡ لِيُحَآجُّوكُم بِهِۦ عِندَ رَبِّكُمۡۚ أَفَلَا تَعۡقِلُونَ

Na wanapo kutana na wale walio amini husema: Tumeamini. Na wanapo kuwa peke yao, wao kwa wao, husema: Mnawaambia aliyo kufunulieni Mwenyezi Mungu ili wapate kukuhojieni mbele ya Mola wenu Mlezi? Basi hamfahamu nyinyi? info

Na kilikuwapo kikundi kingine miongoni mwa wanaafiki wao wakikutana na walio amini husema kwa kuwakhadaa: Tunaamini kuwa nyinyi mnafuata Haki, na kuwa Muhammad ni Nabii aliye tajwa sifa zake katika Taurati. Na wakiwa peke yao na wenzao hulaumiana kwa kughafilika kwa baadhi yao, kwa vile ndimi zao zilivyo teleza katika kuwakhadaa Waumini kuwapa maneno ambayo yatawapa faida makhasimu zao, na wala si lazima katika udanganyifu, wakawatajia yaliyomo katika Taurati ya kueleza kwa sifa kuja kwa Muhammad na kwa hivyo itakuwa hoja juu yao Siku ya Kiyama.

التفاسير: