Vertaling van de betekenissen Edele Qur'an - Swahili vertaling - Abdoellah Mohammed en Nasser Khamees

Pagina nummer:close

external-link copy
58 : 7

وَٱلۡبَلَدُ ٱلطَّيِّبُ يَخۡرُجُ نَبَاتُهُۥ بِإِذۡنِ رَبِّهِۦۖ وَٱلَّذِي خَبُثَ لَا يَخۡرُجُ إِلَّا نَكِدٗاۚ كَذَٰلِكَ نُصَرِّفُ ٱلۡأٓيَٰتِ لِقَوۡمٖ يَشۡكُرُونَ

Na ardhi nzuri, ikiteremkiwa na mvua, inatoa mimea kwa idhini ya Mwenyezi Mungu na matakwa Yake, ikiwa mizuri na kwa njia ya wepesi. Hivyo ndivyo alivyo Muumini, zikiteremka aya za Mwenyezi Mungu kwake, hunufaika nazo na huzalisha kwake maisha mema. Ama ardhi ya chumvi iliyo mbovu; hiyo haitoi mimea isipokuwa mibovu isiyokuwa na faida, tena kwa shida, na haitoi mimea mizuri. Hivyo ndivyo alivyo kafiri, hanufaiki kwa aya za Mwenyezi Mungu. Mfano wa sampuli hiyo nzuri katika kueleza, ndiyo namna tunavyoleta hoja na dalili mbalimbali kuthibitisha haki kwa watu wanaozishukuru neema za Mwenyezi Mungu na wanaomtii. info
التفاسير:

external-link copy
59 : 7

لَقَدۡ أَرۡسَلۡنَا نُوحًا إِلَىٰ قَوۡمِهِۦ فَقَالَ يَٰقَوۡمِ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ مَا لَكُم مِّنۡ إِلَٰهٍ غَيۡرُهُۥٓ إِنِّيٓ أَخَافُ عَلَيۡكُمۡ عَذَابَ يَوۡمٍ عَظِيمٖ

Hakika tulimtuma Nūḥ kwa watu wake, ili awalinganie kwenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu, kutakasika na sifa pungufu ni Kwake, na kumtakasia ibada, akasema, «Enyi watu wangu, muabuduni Mwenyezi Mungu, Peke Yake, na mumnyenyekee kwa kumtii, nyinyi hamna Mola anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Yeye, Aliyetukuka na kuwa juu, mtakasieni ibada. Msipofanya na mkasalia kwenye kuabudu masanamu yenu, hakika mimi nawaogopea msishukiwe na adhabu ya Siku ambayo shida yenu itakuwa kubwa, nayo ni Siku ya Kiyama.» info
التفاسير:

external-link copy
60 : 7

قَالَ ٱلۡمَلَأُ مِن قَوۡمِهِۦٓ إِنَّا لَنَرَىٰكَ فِي ضَلَٰلٖ مُّبِينٖ

Mabwana wao na wakubwa wao walisema, «Sisi tunaitakidi, ewe Nūḥ, wewe uko kwenye upotevu waziwazi uko kando ya njia sawa.» info
التفاسير:

external-link copy
61 : 7

قَالَ يَٰقَوۡمِ لَيۡسَ بِي ضَلَٰلَةٞ وَلَٰكِنِّي رَسُولٞ مِّن رَّبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ

Nūḥ Akasema, «Enyi watu wangu, mimi si mpotevu katika jambo lolote kwa njia yoyote, lakini mimi ni mjumbe kutoka Mola wa viumbe wote; Mola wangu na Mola wenu na Mola wa viumbe wote. info
التفاسير:

external-link copy
62 : 7

أُبَلِّغُكُمۡ رِسَٰلَٰتِ رَبِّي وَأَنصَحُ لَكُمۡ وَأَعۡلَمُ مِنَ ٱللَّهِ مَا لَا تَعۡلَمُونَ

«Nawafikishia nyinyi lile niliotumwa nalo kutoka kwa Mola wangu, na wapa ushauri kwa kuwaonya na adhabu ya Mwenyezi Mungu na kuwapa bishara njema ya malipo yake mema, na mimi nayajua, kuhusu sheria Yake, msiyoyajua. info
التفاسير:

external-link copy
63 : 7

أَوَعَجِبۡتُمۡ أَن جَآءَكُمۡ ذِكۡرٞ مِّن رَّبِّكُمۡ عَلَىٰ رَجُلٖ مِّنكُمۡ لِيُنذِرَكُمۡ وَلِتَتَّقُواْ وَلَعَلَّكُمۡ تُرۡحَمُونَ

«Je imewafanya nyinyi muone ajabu kwa kuwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Ameteremsha kwenu yale ambayo yatawakumbusha mambo yenye kheri kwenu, kwa ulimi wa mtu miongoni mwenu, mnaoujua ukoo wake na ukweli wake, ili awaogopeshe adhabu ya Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, na mateso Yake, na ili mujikinge na hasira Zake kwa kumuamini na kwa kutarajia kufaulu kupata rehema Zake na malipo Yake mema mengi? info
التفاسير:

external-link copy
64 : 7

فَكَذَّبُوهُ فَأَنجَيۡنَٰهُ وَٱلَّذِينَ مَعَهُۥ فِي ٱلۡفُلۡكِ وَأَغۡرَقۡنَا ٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَآۚ إِنَّهُمۡ كَانُواْ قَوۡمًا عَمِينَ

Basi walimkanusha Nūḥ, tukamuokoa na wale walioamini pamoja na yeye katika jahazi, na tukawazamisha makafiri waliokanusha hoja zetu zilizowazi. Wao walikuwa vipofu wa nyoyo kwa kutoiona haki. info
التفاسير:

external-link copy
65 : 7

۞ وَإِلَىٰ عَادٍ أَخَاهُمۡ هُودٗاۚ قَالَ يَٰقَوۡمِ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ مَا لَكُم مِّنۡ إِلَٰهٍ غَيۡرُهُۥٓۚ أَفَلَا تَتَّقُونَ

Hakika tulimtuma, kwenda kwa watu wa kabila la 'Ād, ndugu yao Hūd, walipoabudu masanamu badala ya Mwenyezi Mungu, akawaambia, «Muabuduni Mwenyezi Mungu, Peke Yake, hamna mola anayestahiki kuabudiwa isipokuwaYeye, Aliyetukuka na kuwa juu, mtakasieni ibada. Je, hamuiogopi adhabu ya Mwenyezi Mungu na hasira Zake kwenu?» info
التفاسير:

external-link copy
66 : 7

قَالَ ٱلۡمَلَأُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِن قَوۡمِهِۦٓ إِنَّا لَنَرَىٰكَ فِي سَفَاهَةٖ وَإِنَّا لَنَظُنُّكَ مِنَ ٱلۡكَٰذِبِينَ

Wakasema wale viongozi waliokufuru katika watu wa Hūd, «Sisi tunajua kwamba wewe, kwa kutuita sisi kuacha kuabudu waungu wetu na kumuabudu Mwenyezi Mungu, Peke Yake, ni mpungufu wa akili, na sisi tunaamini kwamba wewe, kwa hayo usemayo, ni katika wale wanaomzuluia Mwenyezi Mungu warongo.» info
التفاسير:

external-link copy
67 : 7

قَالَ يَٰقَوۡمِ لَيۡسَ بِي سَفَاهَةٞ وَلَٰكِنِّي رَسُولٞ مِّن رَّبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ

Hūd akasema, «Enyi watu wangu, sina upungufu katika akili yangu, isipokuwa mimi ni mjumbe kutoka kwa Mola wa viumbe wote. info
التفاسير: