Vertaling van de betekenissen Edele Qur'an - Swahili vertaling - Abdoellah Mohammed en Nasser Khamees

Pagina nummer:close

external-link copy
52 : 7

وَلَقَدۡ جِئۡنَٰهُم بِكِتَٰبٖ فَصَّلۡنَٰهُ عَلَىٰ عِلۡمٍ هُدٗى وَرَحۡمَةٗ لِّقَوۡمٖ يُؤۡمِنُونَ

Hakika tumewaletea makafiri Qur’ani tuliyokuteremshia wewe, ewe Mtume, tuliyoibainisha, inayokusanya elimu kubwa, yenye kuongoza, kutoa kwenye upotevu, kupeleka kwenye njia ya usawa, hali ya kuwa ni rehema kwa watu wanaomuamini Mwenyezi Mungu na kuzitumia sheria Zake. Amewahusu wenye kuamini kwa kuwataja, bila ya wengine, ni kwamba wao ndio wenye kunufaika nayo info
التفاسير:

external-link copy
53 : 7

هَلۡ يَنظُرُونَ إِلَّا تَأۡوِيلَهُۥۚ يَوۡمَ يَأۡتِي تَأۡوِيلُهُۥ يَقُولُ ٱلَّذِينَ نَسُوهُ مِن قَبۡلُ قَدۡ جَآءَتۡ رُسُلُ رَبِّنَا بِٱلۡحَقِّ فَهَل لَّنَا مِن شُفَعَآءَ فَيَشۡفَعُواْ لَنَآ أَوۡ نُرَدُّ فَنَعۡمَلَ غَيۡرَ ٱلَّذِي كُنَّا نَعۡمَلُۚ قَدۡ خَسِرُوٓاْ أَنفُسَهُمۡ وَضَلَّ عَنۡهُم مَّا كَانُواْ يَفۡتَرُونَ

Kwani kuna wanachokingojea makafiri isipokuwa mateso, ambayo ndiyo kikomo cha mambo yao, waliyoahidiwa katika Qur’ani? Siku kitakapokuja kikomo cha mambo yao, cha kuhesabiwa, kulipwa na mateso Siku ya Kiyama, watasema makafiri walioiacha Qur’ani na wakaikanusha duniani, «Sasa imetubainikia kwamba Mitume wa Mola wetu wamekuja na haki na wametupa ushauri mzuri. Je, tunaweza kupata marafiki na waombezi wapate kutuombea kwa Mola wetu? Au tunaweza kupewa nafasi ya kurudi duniani mara nyingine tupate kufanya matendo ya kumfanya Mwenyezi Mungu Awe radhi na sisi? Hakika wamepata hasara nafsi zao kwa kuingia Motoni na kukaa milele humo, na vimewaondokea vile ambavyo walikuwa wakiviabudu badala ya Mwenyezi Mungu na yale ambayo walikuwa wakiyazua miongoni mwa yale ambayo Shetani alikuwa akiwaadi nayo. info
التفاسير:

external-link copy
54 : 7

إِنَّ رَبَّكُمُ ٱللَّهُ ٱلَّذِي خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٖ ثُمَّ ٱسۡتَوَىٰ عَلَى ٱلۡعَرۡشِۖ يُغۡشِي ٱلَّيۡلَ ٱلنَّهَارَ يَطۡلُبُهُۥ حَثِيثٗا وَٱلشَّمۡسَ وَٱلۡقَمَرَ وَٱلنُّجُومَ مُسَخَّرَٰتِۭ بِأَمۡرِهِۦٓۗ أَلَا لَهُ ٱلۡخَلۡقُ وَٱلۡأَمۡرُۗ تَبَارَكَ ٱللَّهُ رَبُّ ٱلۡعَٰلَمِينَ

Hakika Mola wenu, enyi watu, ni Yule Aliyeanzisha mbingu na ardhi kutoka kwenye 'adam (hali ya kutokuwako) kwa Siku Sita, kisha Akalingana, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, juu ya 'Arsh, -yaani : Alikuwa juu- mlingano unaonasibiana na utukufu na ukubwa Wake. Yeye , kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, Anauingiza usiku kwenye mchana ukaufinika mpaka mwangaza wake ukaondoka, na Anauingiza usiku kwenye mchana mpaka giza lake likaondoka. Na daima kila mojawapo, kati ya viwili hivyi, kinafuata kingine kwa kasi. Na Yeye, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, Ndiye Aliyeumba jua, mwezi na nyota zikiwa zinamtii Yeye, Anazipelekesha, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, vile Anavyotaka, nazo ni miongoni mwa alama kubwa za Mwenyezi Mungu. Jua utanabahi kwamba ni wake Yeye, kutakasika na sifa za upungufu na kutukuka ni Kwake, uumbaji wote, na ni Yake Yeye amri yote. Ametukuka Mwenyezi Mungu, umeendelea ukuu Wake na Ameepukana na kila upungufu, Bwana wa viumbe wote. info
التفاسير:

external-link copy
55 : 7

ٱدۡعُواْ رَبَّكُمۡ تَضَرُّعٗا وَخُفۡيَةًۚ إِنَّهُۥ لَا يُحِبُّ ٱلۡمُعۡتَدِينَ

Muombeni, enyi Waumini, Mola wenu, kwa kujidhalilisha Kwake, kwa siri na kwa dhahiri.Na maombi yawe kwa unyenyekevu na yawe mbali na kujionyesha.Hakika Mwenyezi Mungu Hawapendi wanaokiuka mipaka ya sheria Zake. Na ukiukaji mkubwa ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu, kama vile kuwaomba wafu, masanamu na wengineo mfano wao wasiokuwa Mwenyezi Mungu. info
التفاسير:

external-link copy
56 : 7

وَلَا تُفۡسِدُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ بَعۡدَ إِصۡلَٰحِهَا وَٱدۡعُوهُ خَوۡفٗا وَطَمَعًاۚ إِنَّ رَحۡمَتَ ٱللَّهِ قَرِيبٞ مِّنَ ٱلۡمُحۡسِنِينَ

Wala msilete katika ardhi aina yoyote ya uharibifu, baada ya Mwenyezi Mungu kuitengeneza kwa kutuma Mitume, amani iwashukie, na kuimarika kwa utiifu wa Mwenyezi Mungu. Na muombeni Yeye, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, mkimtakasia maombi yenu, kwa kuogopa mateso Yake na kuwa na matumaini kupata malipo Yake mazuri. Hakika rehema ya Mwenyezi Mungu iko karibu na wenye kufanya wema. info
التفاسير:

external-link copy
57 : 7

وَهُوَ ٱلَّذِي يُرۡسِلُ ٱلرِّيَٰحَ بُشۡرَۢا بَيۡنَ يَدَيۡ رَحۡمَتِهِۦۖ حَتَّىٰٓ إِذَآ أَقَلَّتۡ سَحَابٗا ثِقَالٗا سُقۡنَٰهُ لِبَلَدٖ مَّيِّتٖ فَأَنزَلۡنَا بِهِ ٱلۡمَآءَ فَأَخۡرَجۡنَا بِهِۦ مِن كُلِّ ٱلثَّمَرَٰتِۚ كَذَٰلِكَ نُخۡرِجُ ٱلۡمَوۡتَىٰ لَعَلَّكُمۡ تَذَكَّرُونَ

Na Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Ndiye Anayetuma upepo mzuri mororo wenye kubashiria mvua ambayo upepo huo unaisukuma kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na hapo viumbe vikangiwa na furaha kwa hiyo rehema ya Mwenyezi Mungu. Na pindi ifikapo wakati ambapo upepo umebeba mawingu yaliyobebeshwa mvua, Mwenyezi Mungu Huyapeleka kwa upepo huo ili kuihuisha nchi iliyopigwa na ukame ardhi yake na kukauka miti yake na mimea yake ya nafaka, Mwenyezi Mungu hapo Akaiteremsha, kwa mawingu hayo, mvua, Akaitoa kwayo nyasi, miti na mimea ya nafaka, na miti ikarudi kujaa sampuli ya matunda. Kama tunavyoihuisha ardhi hii kwa mvua, vilevile tutawatoa wafu kutoka makabarini mwao baada ya kutoweka kwao, ili muwaidhike na mchukulie dalili juu ya upweke wa Mwenyezi Mungu na uwezo Wake wa kufufua. info
التفاسير: