Vertaling van de betekenissen Edele Qur'an - Swahili vertaling - Abdoellah Mohammed en Nasser Khamees

Pagina nummer:close

external-link copy
59 : 17

وَمَا مَنَعَنَآ أَن نُّرۡسِلَ بِٱلۡأٓيَٰتِ إِلَّآ أَن كَذَّبَ بِهَا ٱلۡأَوَّلُونَۚ وَءَاتَيۡنَا ثَمُودَ ٱلنَّاقَةَ مُبۡصِرَةٗ فَظَلَمُواْ بِهَاۚ وَمَا نُرۡسِلُ بِٱلۡأٓيَٰتِ إِلَّا تَخۡوِيفٗا

Hakuna kilichotuzuia kuteremsha miujiza ambayo washirikina waliitaka isipokuwa ni kwamba ummah waliowatangulia waliikanusha, Mwenyezi Mungu Aliwajibu kwa waliyotaka wakakanusha na wakaangamia. Na tuliwapa Thamūd, nao ni watu wa Ṣāliḥ, miujiza iliyo wazi, nayo ni ngamia, wakaikanusha na tukawaangamiza. Na huku kutuma kwetu Mitume wakiwa na alama, mazingatio na miujiza tuliyoipitisha kwenye mikono yao, hakukuwa isipokuwa ni kuwatisha waja wapate kuzingatia na wakumbuke. info
التفاسير:

external-link copy
60 : 17

وَإِذۡ قُلۡنَا لَكَ إِنَّ رَبَّكَ أَحَاطَ بِٱلنَّاسِۚ وَمَا جَعَلۡنَا ٱلرُّءۡيَا ٱلَّتِيٓ أَرَيۡنَٰكَ إِلَّا فِتۡنَةٗ لِّلنَّاسِ وَٱلشَّجَرَةَ ٱلۡمَلۡعُونَةَ فِي ٱلۡقُرۡءَانِۚ وَنُخَوِّفُهُمۡ فَمَا يَزِيدُهُمۡ إِلَّا طُغۡيَٰنٗا كَبِيرٗا

Kumbuka, ewe Mtume, pindi tulipokwambia kwamba Mola wako Amewazunguka watu kwa ujuzi na uweza. Na hatukuijaalia ndoto tuliyokuonyesha waziwazi usiku wa isrā’ (kwenda Bayt al- Maqdis) na mi'rāj (kupaa kwenda mbinguni) miongoni mwa maajabu ya viumbe isipokuwa ni kuwatahini watu. Na tunawatisha washirikina kwa aina mbalimbali za adhabu na miujiza, lakini kuwatisha huko hakuwaongezei isipokuwa ni kuendelea zaidi kwenye ukafiri na upotevu. info
التفاسير:

external-link copy
61 : 17

وَإِذۡ قُلۡنَا لِلۡمَلَٰٓئِكَةِ ٱسۡجُدُواْ لِأٓدَمَ فَسَجَدُوٓاْ إِلَّآ إِبۡلِيسَ قَالَ ءَأَسۡجُدُ لِمَنۡ خَلَقۡتَ طِينٗا

Na ukumbuke neno tulilowaambia Malaika wamsujudie Ādam kwa kumwamkia na kumuhishimu, wakamsujudia wote isipokuwa Iblisi, alifanya kiburi na akakataa kusujudu, na huku akisema kwa njia ya kupinga na kujiona, «Je, nimsujudie huyu dhaifu aliyeumbwa kwa udongo?» info
التفاسير:

external-link copy
62 : 17

قَالَ أَرَءَيۡتَكَ هَٰذَا ٱلَّذِي كَرَّمۡتَ عَلَيَّ لَئِنۡ أَخَّرۡتَنِ إِلَىٰ يَوۡمِ ٱلۡقِيَٰمَةِ لَأَحۡتَنِكَنَّ ذُرِّيَّتَهُۥٓ إِلَّا قَلِيلٗا

Iblisi akasema akionesha ujasiri wake na ukafiri kwa Mwenyezi Mungu, «Unamuona kiumbe huyu uliyemfadhilisha juu yangu? Ukinibakisha hai mpaka Siku ya Kiyama nitawatawala wale wanaozalikana na yeye kwa kuwapoteza na kuwaharibu isipokuwa wale waliotakaswa katika Imani, nao ni wachache.» info
التفاسير:

external-link copy
63 : 17

قَالَ ٱذۡهَبۡ فَمَن تَبِعَكَ مِنۡهُمۡ فَإِنَّ جَهَنَّمَ جَزَآؤُكُمۡ جَزَآءٗ مَّوۡفُورٗا

Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Akasema Akimuonya Iblisi na wafuasi wake, «Enda! Yoyote mwenye kukufuata miongoni mwa kizazi cha Ādam, basi mateso yako na mateso yao ndani ya moto wa Jahanamu ni mengi. info
التفاسير:

external-link copy
64 : 17

وَٱسۡتَفۡزِزۡ مَنِ ٱسۡتَطَعۡتَ مِنۡهُم بِصَوۡتِكَ وَأَجۡلِبۡ عَلَيۡهِم بِخَيۡلِكَ وَرَجِلِكَ وَشَارِكۡهُمۡ فِي ٱلۡأَمۡوَٰلِ وَٱلۡأَوۡلَٰدِ وَعِدۡهُمۡۚ وَمَا يَعِدُهُمُ ٱلشَّيۡطَٰنُ إِلَّا غُرُورًا

«Na uwalaghai wale unaoweza kuwalaghai miongoni mwao kwa kuwaita kuniasi, na uwakusanyie askari zako unaowaweza, kati ya kila aliye juu ya kipando na anayetembea kwa miguu, na ujishirikishe nao katika mali yao wanayoyachuma kwa njia za haramu, na ujishirikishe nao katika watoto wao kwa kuwapambia uzinifu na uasi na kwenda kinyume na maamrisho ya Mwenyezi Mungu mpaka uenee uchafu na uharibifu, na uwaahidi wafuasi wako, miongoni mwa wale wanaozalikana na Ādam, ahadi za urongo, na kila ahadi za Shetani ni ubatilifu na udanganyifu. info
التفاسير:

external-link copy
65 : 17

إِنَّ عِبَادِي لَيۡسَ لَكَ عَلَيۡهِمۡ سُلۡطَٰنٞۚ وَكَفَىٰ بِرَبِّكَ وَكِيلٗا

«Hakika waja wangu Waumini waliyotakaswa ambao walinitii, wewe huna uwezo wa kuwapoteza.» Na inatosha kuwa Mola wako , ewe Mtume, kuwa Ndiye Mwenye kuwalinda na kuwahifadhi Waumini kutokana na vitimbi vya Shetani na udanganyifu wake. info
التفاسير:

external-link copy
66 : 17

رَّبُّكُمُ ٱلَّذِي يُزۡجِي لَكُمُ ٱلۡفُلۡكَ فِي ٱلۡبَحۡرِ لِتَبۡتَغُواْ مِن فَضۡلِهِۦٓۚ إِنَّهُۥ كَانَ بِكُمۡ رَحِيمٗا

Mola wenu, enyi watu, Ndiye Anayewaendeshea vyombo vya kusafiria baharini ili mtafute riziki ya Mwenyezi Mungu katika safari zenu na biashara zenu. Hakika Mwenyezi Mungu , kutakata na sifa za upungufu ni Kwake, ni Mwingi wa huruma kwa waja Wake. info
التفاسير: