Vertaling van de betekenissen Edele Qur'an - Swahili vertaling - Abdoellah Mohammed en Nasser Khamees

Pagina nummer:close

external-link copy
97 : 17

وَمَن يَهۡدِ ٱللَّهُ فَهُوَ ٱلۡمُهۡتَدِۖ وَمَن يُضۡلِلۡ فَلَن تَجِدَ لَهُمۡ أَوۡلِيَآءَ مِن دُونِهِۦۖ وَنَحۡشُرُهُمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ عَلَىٰ وُجُوهِهِمۡ عُمۡيٗا وَبُكۡمٗا وَصُمّٗاۖ مَّأۡوَىٰهُمۡ جَهَنَّمُۖ كُلَّمَا خَبَتۡ زِدۡنَٰهُمۡ سَعِيرٗا

Na yoyote yule ambaye Mwenyezi Mungu Anamuongoza ndiye mwenye kuongoka kwenye haki, na yoyote yule ambaye Yeye Anampoteza, Akamdhili na Akamuachia yeye na nafsi yake basi huyo hakuna mwenye kumuongoza badala ya Mwenyezi Mungu. Hawa wapotevu Mwenyezi Mungu Atawafufua Siku ya Kiyama na Awakusanye kwa nyuso zao hali wakiwa hawaoni wala hawatamki wala hawasikii. Mwisho wao ni moto wa Jahanamu wenye kuwaka, kila kutuliapo kuwaka kwake na kuzimika mroromo wake, tunawazidishia moto wenye kuwaka na kuroroma. info
التفاسير:

external-link copy
98 : 17

ذَٰلِكَ جَزَآؤُهُم بِأَنَّهُمۡ كَفَرُواْ بِـَٔايَٰتِنَا وَقَالُوٓاْ أَءِذَا كُنَّا عِظَٰمٗا وَرُفَٰتًا أَءِنَّا لَمَبۡعُوثُونَ خَلۡقٗا جَدِيدًا

Adhabu hii iliyosifiwa ni mateso kwa washirikina kwa sababu ya kukanausha kwao aya za Mwenyezi Mungu na hoja Zake, kukanusha kwao Mitume Wake waliowaita kumuabudu Yeye na kule kusema kwao kwa njia ya kukataa, waamrishwapo kuamini kuwa kuna Ufufuzi, «Tutakapokufa na tukawa mifupa iliyochakaa na vipande vilivyotengeka mbalimbali, je tutafufuliwa baada yake hali ya kuwa ni viumbe vipya?» info
التفاسير:

external-link copy
99 : 17

۞ أَوَلَمۡ يَرَوۡاْ أَنَّ ٱللَّهَ ٱلَّذِي خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ قَادِرٌ عَلَىٰٓ أَن يَخۡلُقَ مِثۡلَهُمۡ وَجَعَلَ لَهُمۡ أَجَلٗا لَّا رَيۡبَ فِيهِ فَأَبَى ٱلظَّٰلِمُونَ إِلَّا كُفُورٗا

Je, kwani wameghafilika hawa washirikina, wasiangalie na kujuwa kwamba Mwenyezi Mungu, Aliyeumba mbingu na ardhi na viumbe vilivyomo ndani yake bila ya mfano uliotangulia, ni muweza wa kuumba mfano wao baada ya kumalizika kwao? Mwenyezi Mungu Amewaekea washirikina hawa wakati maalumu wa kufa kwao na kuadhibiwa, hapana shaka wakati huo utawafikia. Na pamoja na uwazi wa haki na dalili Zake walikataa washirikina isipokuwa ni kuikanusha Dini ya Mwenyezi Mungu, Aliyeshinda na kutukuka. info
التفاسير:

external-link copy
100 : 17

قُل لَّوۡ أَنتُمۡ تَمۡلِكُونَ خَزَآئِنَ رَحۡمَةِ رَبِّيٓ إِذٗا لَّأَمۡسَكۡتُمۡ خَشۡيَةَ ٱلۡإِنفَاقِۚ وَكَانَ ٱلۡإِنسَٰنُ قَتُورٗا

Sema, ewe Mtume, kuwaambia hawa washirikina, «Lau nyinyi mnamiliki hazina za rehema ya Mola wangu ambazo hazimaliziki wala hazitoeki, basi mungalizifanyia ubahili msitoe katika hizo kuwapa wengine kwa kuchelea zisimalizike mkawa mafukara.» Na ni katika tabia ya binadamu kuwa yeye ni mgumu wa kile kilicho mkononi mwake, isipokuwa yule aliyehifadhiwa na Mwenyezi Mungu. info
التفاسير:

external-link copy
101 : 17

وَلَقَدۡ ءَاتَيۡنَا مُوسَىٰ تِسۡعَ ءَايَٰتِۭ بَيِّنَٰتٖۖ فَسۡـَٔلۡ بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ إِذۡ جَآءَهُمۡ فَقَالَ لَهُۥ فِرۡعَوۡنُ إِنِّي لَأَظُنُّكَ يَٰمُوسَىٰ مَسۡحُورٗا

Na hakika tulimpa Mūsā miujiza tisa iliyo waziwazi, yenye kutolea ushahidi wa ukweli wa unabii wake, nayo ni fimbo, mkono, ukame, upungufu wa matunda, mafuriko, nzige, chawa, vyura na damu. Basi waulize Mayahudi, ewe Mtume, suala la kuthibitisha, pale Mūsā alipowajia mababu zao na miujiza iliyo wazi, Fir'awn akasema kumwambia Mūsā, «Mimi nadhani, ewe Mūsā, kwamba wewe ni mchawi uliodanganywa na kutekwa akili yako kwa vitendo hivyo vya ajabu unavyovileta.» info
التفاسير:

external-link copy
102 : 17

قَالَ لَقَدۡ عَلِمۡتَ مَآ أَنزَلَ هَٰٓؤُلَآءِ إِلَّا رَبُّ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ بَصَآئِرَ وَإِنِّي لَأَظُنُّكَ يَٰفِرۡعَوۡنُ مَثۡبُورٗا

Mūsā akamjibu, «Umeshajua kwa yakini, ewe Fir'awn, kwamba hakuiteremsha miujiza hiyo tisa yenye kuutolea ishahidi unabii wangu isipokuwa Mola wa mbingu na ardhi, ipate kuwa ni dalili ambazo wenye busara watazitumia kuonyesha upweke wa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka katika uola Wake na uungu Wake, na mimi nina yakini kwamaba wewe, ewe Fir'awn, ni mwenye kuangamia, kulaaniwa na kushindwa.» info
التفاسير:

external-link copy
103 : 17

فَأَرَادَ أَن يَسۡتَفِزَّهُم مِّنَ ٱلۡأَرۡضِ فَأَغۡرَقۡنَٰهُ وَمَن مَّعَهُۥ جَمِيعٗا

Hapo Fir'awn akataka kumbabaisha Mūsā na kumtoa pamoja na Wana wa Isrāīl kwenye ardhi ya Misri, tukamuanagamiza baharini yeye na askari waliokuwa pamoja na yeye kwa kuwatesa. info
التفاسير:

external-link copy
104 : 17

وَقُلۡنَا مِنۢ بَعۡدِهِۦ لِبَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ ٱسۡكُنُواْ ٱلۡأَرۡضَ فَإِذَا جَآءَ وَعۡدُ ٱلۡأٓخِرَةِ جِئۡنَا بِكُمۡ لَفِيفٗا

Na tukasema, baada ya kuangamia Fir’awn na askari wake, kuwaambia Wana wa Isrāīl, «Kaeni ardhi ya Sham. Na itakapo kuja Siku ya Kiyama, tutawaleta nyote kutoka makaburini mwenu kufika kwenye kisimamo cha kuhesabiwa.» info
التفاسير: