ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - មជ្ឈមណ្ឌលបកប្រែរ៉ូវ៉ាដ

លេខ​ទំព័រ:close

external-link copy
188 : 7

قُل لَّآ أَمۡلِكُ لِنَفۡسِي نَفۡعٗا وَلَا ضَرًّا إِلَّا مَا شَآءَ ٱللَّهُۚ وَلَوۡ كُنتُ أَعۡلَمُ ٱلۡغَيۡبَ لَٱسۡتَكۡثَرۡتُ مِنَ ٱلۡخَيۡرِ وَمَا مَسَّنِيَ ٱلسُّوٓءُۚ إِنۡ أَنَا۠ إِلَّا نَذِيرٞ وَبَشِيرٞ لِّقَوۡمٖ يُؤۡمِنُونَ

Sema: Siimilikii nafsi yangu manufaa wala madhara, isipokuwa apendavyo Mwenyezi Mungu. Na lau kuwa ninayajua ya ghaibu, ningalitenda mema sana, wala ubaya usingenigusa. Mimi si chochote ila ni mwonyaji na mbashiri kwa kaumu wanaoamini. info
التفاسير:

external-link copy
189 : 7

۞ هُوَ ٱلَّذِي خَلَقَكُم مِّن نَّفۡسٖ وَٰحِدَةٖ وَجَعَلَ مِنۡهَا زَوۡجَهَا لِيَسۡكُنَ إِلَيۡهَاۖ فَلَمَّا تَغَشَّىٰهَا حَمَلَتۡ حَمۡلًا خَفِيفٗا فَمَرَّتۡ بِهِۦۖ فَلَمَّآ أَثۡقَلَت دَّعَوَا ٱللَّهَ رَبَّهُمَا لَئِنۡ ءَاتَيۡتَنَا صَٰلِحٗا لَّنَكُونَنَّ مِنَ ٱلشَّٰكِرِينَ

Yeye ndiye aliyewaumba kutoka katika nafsi moja; na katika hiyo hiyo akamfanya mwenzi wake, ili ajitulize kwake. Na alipomuingilia, akabeba mimba nyepesi, akitembea nao. Anapokuwa mjamzito, wote wawili humwomba Mwenyezi Mungu, Mola wao Mlezi: Kama ukitupa mwana mwema hakika tutakuwa katika wanaoshukuru. info
التفاسير:

external-link copy
190 : 7

فَلَمَّآ ءَاتَىٰهُمَا صَٰلِحٗا جَعَلَا لَهُۥ شُرَكَآءَ فِيمَآ ءَاتَىٰهُمَاۚ فَتَعَٰلَى ٱللَّهُ عَمَّا يُشۡرِكُونَ

Basi alipowapa mwana mwema, wakamfanyia washirikina Mwenyezi Mungu katika kile kile alichowapa. Basi Mwenyezi Mungu ametukuka na huko kushirikisha kwao. info
التفاسير:

external-link copy
191 : 7

أَيُشۡرِكُونَ مَا لَا يَخۡلُقُ شَيۡـٔٗا وَهُمۡ يُخۡلَقُونَ

Ati wanashirikisha kisichoumba kitu, hali ya kuwa wao wanaumbwa? info
التفاسير:

external-link copy
192 : 7

وَلَا يَسۡتَطِيعُونَ لَهُمۡ نَصۡرٗا وَلَآ أَنفُسَهُمۡ يَنصُرُونَ

Wala hawawezi kuwanusuru wala wao wenyewe hawajinusuru. info
التفاسير:

external-link copy
193 : 7

وَإِن تَدۡعُوهُمۡ إِلَى ٱلۡهُدَىٰ لَا يَتَّبِعُوكُمۡۚ سَوَآءٌ عَلَيۡكُمۡ أَدَعَوۡتُمُوهُمۡ أَمۡ أَنتُمۡ صَٰمِتُونَ

Na mkiwaita kwenye uwongofu, hawawafuati. Ni mamoja kwenu ikiwa mtawaita au mkae kimya. info
التفاسير:

external-link copy
194 : 7

إِنَّ ٱلَّذِينَ تَدۡعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ عِبَادٌ أَمۡثَالُكُمۡۖ فَٱدۡعُوهُمۡ فَلۡيَسۡتَجِيبُواْ لَكُمۡ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ

Hakika wale mnaowaomba badala ya Mwenyezi Mungu ni waja mfano wenu nyinyi. Basi waombeni, nao wawaitikie ikiwa nyinyi ni wakweli. info
التفاسير:

external-link copy
195 : 7

أَلَهُمۡ أَرۡجُلٞ يَمۡشُونَ بِهَآۖ أَمۡ لَهُمۡ أَيۡدٖ يَبۡطِشُونَ بِهَآۖ أَمۡ لَهُمۡ أَعۡيُنٞ يُبۡصِرُونَ بِهَآۖ أَمۡ لَهُمۡ ءَاذَانٞ يَسۡمَعُونَ بِهَاۗ قُلِ ٱدۡعُواْ شُرَكَآءَكُمۡ ثُمَّ كِيدُونِ فَلَا تُنظِرُونِ

Je, wao wanayo miguu wanayotembea kwayo? Au wanayo mikono wanayokamata kwa nguvu kwayo? Au wanayo macho wanayoona kwayo? Au wanayo wanayosikia kwayo? Sema: Waiteni washirika wenu hao, kisha nifanyieni mimi njama, na wala msinipe muhula. info
التفاسير: