ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - មជ្ឈមណ្ឌលបកប្រែរ៉ូវ៉ាដ

Al-A'raf

external-link copy
1 : 7

الٓمٓصٓ

Alif Laam Miim Swaad info
التفاسير:

external-link copy
2 : 7

كِتَٰبٌ أُنزِلَ إِلَيۡكَ فَلَا يَكُن فِي صَدۡرِكَ حَرَجٞ مِّنۡهُ لِتُنذِرَ بِهِۦ وَذِكۡرَىٰ لِلۡمُؤۡمِنِينَ

Kitabu kilichoteremshwa kwako, basi isiwe dhiki yoyote katika kifua chako kwa sababu yake, ili uonye kwacho, na kiwe ni ukumbusho kwa Waumini. info
التفاسير:

external-link copy
3 : 7

ٱتَّبِعُواْ مَآ أُنزِلَ إِلَيۡكُم مِّن رَّبِّكُمۡ وَلَا تَتَّبِعُواْ مِن دُونِهِۦٓ أَوۡلِيَآءَۗ قَلِيلٗا مَّا تَذَكَّرُونَ

Yafuateni yale yaliyoteremshwa kwenu kutoka kwa Mola wenu Mlezi, wala msifuate marafiki wasaidizi wowote badala yake. Ni machache mnayoyakumbuka. info
التفاسير:

external-link copy
4 : 7

وَكَم مِّن قَرۡيَةٍ أَهۡلَكۡنَٰهَا فَجَآءَهَا بَأۡسُنَا بَيَٰتًا أَوۡ هُمۡ قَآئِلُونَ

Na ni miji mingapi tuliyoiangamiza, ikaifikia adhabu yetu usiku au walipokuwa wamelala adhuhuri. info
التفاسير:

external-link copy
5 : 7

فَمَا كَانَ دَعۡوَىٰهُمۡ إِذۡ جَآءَهُم بَأۡسُنَآ إِلَّآ أَن قَالُوٓاْ إِنَّا كُنَّا ظَٰلِمِينَ

Basi haukuwa mwito wao wakati ilipowajia adhabu yetu, isipokuwa walisema, "Hakika sisi tulikuwa madhalimu." info
التفاسير:

external-link copy
6 : 7

فَلَنَسۡـَٔلَنَّ ٱلَّذِينَ أُرۡسِلَ إِلَيۡهِمۡ وَلَنَسۡـَٔلَنَّ ٱلۡمُرۡسَلِينَ

Na hakika tutawauliza wale waliotumiwa Ujumbe, na pia hakika tutawauliza hao Wajumbe. info
التفاسير:

external-link copy
7 : 7

فَلَنَقُصَّنَّ عَلَيۡهِم بِعِلۡمٖۖ وَمَا كُنَّا غَآئِبِينَ

Tena hakika tutawasimulia kwa elimu. Wala Sisi si kwamba hatukuwepo. info
التفاسير:

external-link copy
8 : 7

وَٱلۡوَزۡنُ يَوۡمَئِذٍ ٱلۡحَقُّۚ فَمَن ثَقُلَتۡ مَوَٰزِينُهُۥ فَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡمُفۡلِحُونَ

Na kipimo Siku hiyo kitakuwa kwa haki. Kwa hivyo yule ambaye vipimo vyake vitakuwa vizito, basi hao ndio waliofaulu. info
التفاسير:

external-link copy
9 : 7

وَمَنۡ خَفَّتۡ مَوَٰزِينُهُۥ فَأُوْلَٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ خَسِرُوٓاْ أَنفُسَهُم بِمَا كَانُواْ بِـَٔايَٰتِنَا يَظۡلِمُونَ

Na yule ambaye vipimo vyake vitakuwa hafifu, basi hao ndio waliozihasirisha nafsi zao kwa sababu ya vile walivyokuwa wakizifanyia Ishara zetu udhalimu. info
التفاسير:

external-link copy
10 : 7

وَلَقَدۡ مَكَّنَّٰكُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَجَعَلۡنَا لَكُمۡ فِيهَا مَعَٰيِشَۗ قَلِيلٗا مَّا تَشۡكُرُونَ

Na hakika tumewaimarisha katika dunia, na tukawajalia humo njia za kupatia maisha. Ni kidogo tu mnavyoshukuru. info
التفاسير:

external-link copy
11 : 7

وَلَقَدۡ خَلَقۡنَٰكُمۡ ثُمَّ صَوَّرۡنَٰكُمۡ ثُمَّ قُلۡنَا لِلۡمَلَٰٓئِكَةِ ٱسۡجُدُواْ لِأٓدَمَ فَسَجَدُوٓاْ إِلَّآ إِبۡلِيسَ لَمۡ يَكُن مِّنَ ٱلسَّٰجِدِينَ

Na hakika tuliwaumba, kisha tukawatia sura, kisha tukawaambia Malaika, "Msujudieni Adam." Basi wakasujudu isipokuwa Iblisi, hakuwa miongoni mwa waliosujudu. info
التفاسير: