ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - មជ្ឈមណ្ឌលបកប្រែរ៉ូវ៉ាដ

លេខ​ទំព័រ:close

external-link copy
12 : 7

قَالَ مَا مَنَعَكَ أَلَّا تَسۡجُدَ إِذۡ أَمَرۡتُكَۖ قَالَ أَنَا۠ خَيۡرٞ مِّنۡهُ خَلَقۡتَنِي مِن نَّارٖ وَخَلَقۡتَهُۥ مِن طِينٖ

(Mwenyezi Mungu) akasema, "Ni nini kilichokuzuia kusujudu nilipokuamrisha?" Akasema, "Mimi ni bora zaidi kumliko yeye. Uliniumba kwa moto, naye ulimuumba kwa udongo." info
التفاسير:

external-link copy
13 : 7

قَالَ فَٱهۡبِطۡ مِنۡهَا فَمَا يَكُونُ لَكَ أَن تَتَكَبَّرَ فِيهَا فَٱخۡرُجۡ إِنَّكَ مِنَ ٱلصَّٰغِرِينَ

Akasema, "Basi teremka kutoka humo! Haikufalii kufanya kiburi humo. Basi toka! Hakika wewe ni miongoni mwa walio duni." info
التفاسير:

external-link copy
14 : 7

قَالَ أَنظِرۡنِيٓ إِلَىٰ يَوۡمِ يُبۡعَثُونَ

Akasema, "Nipe muhula mpaka siku watakapofufuliwa." info
التفاسير:

external-link copy
15 : 7

قَالَ إِنَّكَ مِنَ ٱلۡمُنظَرِينَ

Akasema, "Hakika wewe ni miongoni mwa waliopewa muhula." info
التفاسير:

external-link copy
16 : 7

قَالَ فَبِمَآ أَغۡوَيۡتَنِي لَأَقۡعُدَنَّ لَهُمۡ صِرَٰطَكَ ٱلۡمُسۡتَقِيمَ

Akasema: Kwa kuwa umenipotosha, basi hakika nitawakalia katika Njia yako iliyonyooka. info
التفاسير:

external-link copy
17 : 7

ثُمَّ لَأٓتِيَنَّهُم مِّنۢ بَيۡنِ أَيۡدِيهِمۡ وَمِنۡ خَلۡفِهِمۡ وَعَنۡ أَيۡمَٰنِهِمۡ وَعَن شَمَآئِلِهِمۡۖ وَلَا تَجِدُ أَكۡثَرَهُمۡ شَٰكِرِينَ

Kisha nitawajia kwa mbele yao na kwa nyuma yao na kuliani kwao kwote na kushotoni kwao kwote. Wala hutawakuta wengi wao wenye shukrani. info
التفاسير:

external-link copy
18 : 7

قَالَ ٱخۡرُجۡ مِنۡهَا مَذۡءُومٗا مَّدۡحُورٗاۖ لَّمَن تَبِعَكَ مِنۡهُمۡ لَأَمۡلَأَنَّ جَهَنَّمَ مِنكُمۡ أَجۡمَعِينَ

Akasema: Toka humo ilhali umeshutumiwa, umefukuzwa. Hapana shaka atakayekufuata miongoni mwao, basi nitaijaza Jahannam kwa nyinyi nyote. info
التفاسير:

external-link copy
19 : 7

وَيَٰٓـَٔادَمُ ٱسۡكُنۡ أَنتَ وَزَوۡجُكَ ٱلۡجَنَّةَ فَكُلَا مِنۡ حَيۡثُ شِئۡتُمَا وَلَا تَقۡرَبَا هَٰذِهِ ٱلشَّجَرَةَ فَتَكُونَا مِنَ ٱلظَّٰلِمِينَ

Na wewe, Adam! Kaa wewe na mkeo Bustanini humo, na kuleni kwayo mpendapo. Wala msiukaribie mti huu, basi mkawa katika madhalimu. info
التفاسير:

external-link copy
20 : 7

فَوَسۡوَسَ لَهُمَا ٱلشَّيۡطَٰنُ لِيُبۡدِيَ لَهُمَا مَا وُۥرِيَ عَنۡهُمَا مِن سَوۡءَٰتِهِمَا وَقَالَ مَا نَهَىٰكُمَا رَبُّكُمَا عَنۡ هَٰذِهِ ٱلشَّجَرَةِ إِلَّآ أَن تَكُونَا مَلَكَيۡنِ أَوۡ تَكُونَا مِنَ ٱلۡخَٰلِدِينَ

Basi Shetani akawatia wasiwasi ili awafichulie tupu zao walizofichwa, na akasema: hakuwakataza Mola wenu Mlezi mti huu isipokuwa mkaja kuwa Malaika, au mkawa katika wanaoishi milele. info
التفاسير:

external-link copy
21 : 7

وَقَاسَمَهُمَآ إِنِّي لَكُمَا لَمِنَ ٱلنَّٰصِحِينَ

Naye akawaapia: Hakika mimi ni miongoni wa wanaowanasihi. info
التفاسير:

external-link copy
22 : 7

فَدَلَّىٰهُمَا بِغُرُورٖۚ فَلَمَّا ذَاقَا ٱلشَّجَرَةَ بَدَتۡ لَهُمَا سَوۡءَٰتُهُمَا وَطَفِقَا يَخۡصِفَانِ عَلَيۡهِمَا مِن وَرَقِ ٱلۡجَنَّةِۖ وَنَادَىٰهُمَا رَبُّهُمَآ أَلَمۡ أَنۡهَكُمَا عَن تِلۡكُمَا ٱلشَّجَرَةِ وَأَقُل لَّكُمَآ إِنَّ ٱلشَّيۡطَٰنَ لَكُمَا عَدُوّٞ مُّبِينٞ

Basi akawatumbukiza kwa hadaa. Na walipouonja ule mti, tupu zao zikawafichukia na wakaanza kujibandikia katika majani ya Bustani hiyo. Na Mola wao Mlezi akawaita, "Je, sikuwakataza mti huo, na kuwaambia ya kwamba hakika Shetani kwenu ni adui wa dhahiri?" info
التفاسير: